Tanzania Nchi Ya Ajabu Ajabu Tu, Kodi Ya Gari Unalonunua Japan Au Kwingine Iko juu Kuliko Bei ya Gari Lenyewe.

chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
2,340
2,000
Wakuu
Ukijaribu kuangalia kwa umakini mfumo wetu wa kodi ni wakijinga sana na hautotusogeza mbele.
Gari kwa Tanzania ni Anasa tena anasa kubwa sana.
Unanunua gari milioni tano eti uandae na kodi milioni tano nyingine.
Hii sio sawa na walioweka hiyo kanuni kwenye kikokotoo naona wao haliwagusi.
Watu wanaponunua magari kikubwa yawe yale yenye ubora tayari mzunguko wa mafuta utaongezeka na huko wewe kama serikali utakusanya kodi pia ya kutosha.
Kodi inapokua juu ndio maana watu hawanunui magari na hapo wigo wa mapato unapungua kisa uzembe uzembe tu.
 
Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,370

Wana discourage tusitununue screpa mkuu
Wakipunguza kodi barabarani itakuwa vituko
Japani kuna gari hadi ya dola 600

Watanzania tunsvyopenda cheap barabara zitajaa mikebe
 
leroy

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
1,214

Wataalam wa masuala ya uchumi na kodi hawaishauri serikali vizuri. Endapo wangelegeza ushuru kidogo katika magari, watu wengi wangemiliki magari, hivyo serikali ingefaidi ushuru wa kila mwaka na kuongeza wigo wa mapato kupitia kodi katika bidhaa nyinginezo mfano mafuta, vipuri n.k.

(economies of scale-focuses on the cost/benefit advantage that arises when there is a higher level of production/consumption of one good.)
 
Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
32,560
2,000
Wana discourage tusitununue screpa mkuu
Wakipunguza kodi barabarani itakuwa vituko
Japani kuna gari hadi ya dola 600

Watanzania tunsvyopenda cheap barabara zitajaa mikebe
Sasa si ndiyo tutanunua magari ya kueleweka mzee baba?

Maana kama ninanunua gari ya $10000 na kodi yake $10000 si nitaziwekaa pamoja nichukue kitu cha maana.

Nimeona nchi zenye kodi ndogo ya magari Africa Toyota unahesabu barabarani.
 
Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,370
2,000
Sasa si ndiyo tutanunua magari ya kueleweka mzee baba?

Maana kama ninanunua gari ya $10000 na kodi yake $10000 si nitaziwekaa pamoja nichukue kitu cha maana.

Nimeona nchi zenye kodi ndogo ya magari Africa Toyota unahesabu barabarani.
Kwa akili za mtanzania sifikiri kama watakuwa wanawaza kama wewe mkuu

Ni mtazamo tu chief
 
Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
9,146
2,000
Ndiyo maana Serikali ya hii nchi haifanikiwi. Wanapenda kuvuna wasipopanda. Hadi waache dhuluma kama hizi ndipo watafanikiwa. Yaani wenzao wabuni magari halafu wao ndiyo watake kula kuliko waliobuni na kutengeneza
 
fredericko

JF-Expert Member
Apr 27, 2014
2,282
2,000
Hivi ile kampuni ya mzee mengi ya ku assemble magari imefikia wapi ❓ au ndio tuhamie Kigali kujibebea Volkswagen maana Jiwe hawezi kuyatoza Kodi kubwa magari ya best yake kagame
 
Wazolee

JF-Expert Member
Sep 1, 2018
1,414
2,000
Tunanunua magari chakavu sababu pesa nyingi inaenda kwenye ushuru, ingekuwa ushuru uko chini;
1. Yangenunuliwa magari mapya/bora zaidi
2. Uchafuzi wa mazingira ungepungua
3. Screpa mtaani zingepungua
4. Ajali barabarani zingepungua
5. Uhakika wa safari ungekuwa mkubwa
6. Wigo wa mapato ungepanuka
7. Na mengine kibao......
Kwa kuongezea Malawi, Zambia,Burundi,Congo na Rwanda wangekuwa wanakuja kununua magali katika show room za hapa Tanzania badala ya kuagiza moja kwa moja Japan
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom