Tanzania: Nchi pekee ambayo wapinzani wananajisi utawala wa sheria

Maramla

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
581
642
_Na Mwamba wa Kaskazini_

Nimefuatilia masuala kadhaa katika siku mbili hizi nikashindwa hata kushangaa.

Tanzania mwezi huu inatekeleza kitendo kikubwa sana cha demokrasia ambapo wananchi watachagua viongozi wao wa ngazi za chini kabisa; aina ya demokrasia ambayo hata katika baadhi ya nchi za Ulaya haipo.

Kituko sasa ni wapinzani wetu tunaowapenda sana na tuliowaamini sana kuwa ni watu wanaoenzi demokrasia, lakini loh wemeanza kuonesha usanii katika uchaguzi huu.

Yaani watu wanalilia utawala wa sheria lakini hawataki kuona sheria zinafuatwa!

Tumeona juzi kuwa baadhi ya wagombea wa upinzani walikatwa kwa kukiuka sheria au taratibu za uchaguzi.

Nilidhani tungeona wapinzani, kama anavyofanya Rais Magufuli kwa watendaji wake wazembe, nao wakienzi misingi ya utawala bora kwa kukemea watendaji wao waliozembea hadi makosa ya kijinga yakajitokeza kwa wagombea wao lutojua namna ya kujaza fomu, lakini hali ni tofauti.

Cha ajabu, wapinzani wetu wa Tanzania wanakimbilia kuona wameonewa. Wanasusia uchaguzi na kutaka waonewe huruma. Kama kawaida yao.

Sanjari na hilo kituko cha pili kinachoendana na hicho ni wapinzani wetu hawa, wanaofahamu fika kuwa zoezi la uchaguzi lina kanuni za kukata rufaa, bila kusubiri rufaa zilizokatwa na wagombea wao, wakabaka tena demokrasia na utawala wa sheria kwa kutangaza kujitoa katika uchaguzi!!

Haya leo rufaa nyingi zimepita na wagombea wao wameshinda, wapinzani hao hao wasiotaka kuona sheria zinafuata mkondo wake wameibuka na kuwatisha wagombea wao walioko tayari kuendelea na uchaguzi. Hii ndio demokrasia wanayoipigania miaka yote?

Nimeshangaa sana, mara wanasema nembo za vyama vyao zisitumike katika karatasi ya kura. Kituko kingine hiki. Kiongozi wa kitaifa unataka kubinya haki za kiongozi wako wa chini? Tena kibabe??Ndio demokrasia mliyoipigania tangu 1992.

Hivi vyama vinasimamia nini hasa katika siasa za nchi hii? Vikishika dola hivi si tumeangamiza hili Taifa?

Yani chama hakina itikadi, hakina falsafa, hakijui sheria zikoje, hakifuati sheria bali kila siku ni kuona kimeonewa tu, unatarajia nini!

Nchi hii imefika hapa kwa sababu ya mifumo inayoenzi demokrasia, utawala wa sheria na hizi ndizo tunu za utawala bora.
 
Ona akili za miccm
IMG-20191110-WA0068.jpeg
Screenshot_20191110-191355.jpeg
Screenshot_20191110-180753.jpeg
IMG_20191110_180930.jpeg
IMG-20191110-WA0007.jpeg
 
Kwani tatzo liko wapi?! Uongozi si hiari mbona kuforce sasa.. Shindeni nyie kwa kishindo kwan tatzo liko wapi!
 
Back
Top Bottom