Tanzania nchi pekee ambayo UKISEMA UKWELI TU UNAKUWA SHUJAA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania nchi pekee ambayo UKISEMA UKWELI TU UNAKUWA SHUJAA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fikirikwanza, May 18, 2012.

 1. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Naomba wanaJF kwa niaba ya watanzania wote tujaribu kulimlika hili; Tanzania imedhihirika wazi kuwa katika hali ya kawaida katika maisha yetu ya kila siku hasa ya kisiasa hakuna kitu kama kusema ukweli, wanasiasa hawasemii ukweli kabisaaaa; Yaani imefikia wakati hata wananchi wakisikia mwanasiasa amesema ukweli inakuwa sababu tosha ya kumwagia sifa kemkem.

  Mifano ipo; Mrema alipokamata dhahabu uwanja wa ndege ikiwa ni sehemu ya kazi ya wizara yake enzi hizo alipata sifa kama kwamba kilikuwa kitu cha ziada mno na watz hawakutegemea kabisa.

  Mara kadhaa Mrema amekuwa na sifa kemkem kwa vile tu alithubutu kusema ukweli kinyume na siasa za TZ; Kwanini kusema ukweli tu linakuwa dili kubwa kuliko kawaida??? TZ haisemi ukweli ktk hali ya kawaida????? nauliza!!


  Ukiachana na Mrema lakini pia utakutana na Vyama vya Upinzani ambavyo vimeamua kusema ukweli; Vyama hivi hata zilipokuwa vidogo vilikua ghafla na kila mtu akashangaa; Kusema ukweli bado ndo nguzo ya nguvu TZ, kwani wengi hawasemi ukweli, Je taifa la uongo mwingi ukweli kidogo litafika???

  Siku hizi hata ndani ya CCM kuna watu walijaribu kusema ukweli kidogo tu, wakawa maarufu. Hii ni judgement yangu kuwa sitta alisema ukweli kidogo sana kupitia Mwakyembe lakini ghafla hawa jamaa wakawa maarufu; Ni mwakyembe mwenyewe aliyesema hakusema ukweli wote ili kuilinda serikali; sasa pamoja na kuficha uovu wa serikali hata kama ni kidogo mwakyembe hakuwatendea watz haki, umaarufu unatoka wapi kwa sitta na mwakyembe wanaweza kuficha sehemu ya ukweli?? lakini kwa vile ni nchi ya uongo ukweli kidogo ni dili!!!!!!

  Hebu shangaa ya mussa uone ya firauni; Filikunjombe ktk kutekeleza maajukumu yake tena aliyoyaomba mwenyewe kwa gharama kubwa ikiwemo kukesha anafanya kampeni apewe huo ubunge; eti kusema ukweli tu kawa shujaa, apokelewa na kila mtu, swali ni kwamba kwani hao wapokeji wake walijua siku zote huwa anasema uongo sasa amebadilika wana mpongeza???? ni kweli walijua hilo ndo maana ya kumpongeza; ni kama kumpongeza rais kwa kuwaapisha mawaziri, ni kama mkupongeza spika kwa kuhudhiria vikao vya bunge, ni kama kumpongeza polisi kwa kukamata wezi, ambavyo kwa kweli siku hizi hapa TZ ndio mwendo mdundo. Tunampongeza baba kwa kulea mwanae kama kwamba alikuwa na hiari ya kuea au kutosa.

  Ninavyoelewa mimi pongezi ni kwa kufanya zaidi ya unavyotakiwa kisheria; Kinyume na isivyorajiwa, Je kuwatongeza watu kwa kusema ukweli tu, kuusema tu ni zaidi tunavyotarajia kwa mujibu wa sheria iliyowaweka madarakani??? Nashawishika kusema hizi pongezi za baba kulipa ada ya mtoto, hizi pongezi za rais kuhutbia bunge, hizo pongezi za kiongozi kuwa na msimamo wakati ndo uongozi wenyewe, hizi pongezi za nesi kmchoma sindano mgonjwa, au kumpa dawa ameze, hizi pongezi za rais kutembelea kijiji chetu, hizi pongezi za golikipa kupangua mkwaju, hizi pongezi za kutimiza wajibu ni kansa inayoua taifa. Tz ni kama taifa la wapenda sifa, utasikia mara kadhaa mtu anafanya jambo zuri kwa mujibu wa sheria anadai apigiwe makofi, apewe sifa kwa kufanya hizo, kwani alikusudiwa kufanya vingine??? utapataje sifa kwa kutimiza wajibu wako tuuu, lazma tuangalie wapi tunakosea, mtoto anajibu swali darasa anapigiwa makofi kwani mwalimu anadhani kijana kaenda kufanya nini darasani??? labda kama class 2 anajibu la class 4; class 4 anajibu maswali ya class 7 hapo sawa.

  Huu Ugonjwa wa Sifa na Pongezi, ni kansa kubwa kwa taifa; Ipo siku kiungo atamlamba mtu chenga harafu anasubiri apigiwe makofi ndo aendelee kuucheza mpira.

  Nawasilisha
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ukisema hivi kuhusu Filikunjombe, je utasemaje kuhusu mapokezi ya Ngeleja kule usukumani? Ngeleja kaondolewa kwa ufisadi na wasukuma wanapongeza kwa maandamano! Lol
   
Loading...