Tanzania National Identities

Mpango wa kuwa na vitambulisho vya kitaifa:

  • Ni Nzuri

    Votes: 202 58.2%
  • Ni Mbaya

    Votes: 146 42.1%

  • Total voters
    347

Mwanagenzi

JF-Expert Member
Sep 11, 2006
697
212
Hii ni habari nzito iliyokuwa inasubiriwa...

Kwa kuwa tumekuwa na matatizo sana kwenye mikataba, sijui na mradi huu utasalimika!

Ni kampuni ile ile walioshinda tenda zamani wakanyimwa ikawa kesi? Au ni zabuni mpya?


Vitambulisho vya taifa Tanzania kugharimu Sh192bilioni

Na Simon Berege, Dodoma, MWANANCHI

SERIKALI imetangaza rasmi kuanza kutekelezwa kwa mradi wa taifa wa kutengeneza vitambulisho vya raia wa Tanzania walimo ndani na nje ya nchi pamoja na wakazi wasio raia waishio nchini utakaogharimu jumla ya Dola za kimarekani 152 milioni sawa na Sh192bilioni.

Waziri wa Mambo ya ndani, Joseph Mungai alisema mjini hapa jana kwamba mradi huo unaoanza mara moja ulipitishwa na kikao cha Bazara za Mawaziri kilichoketi Februari 2 mwaka huu mjini hapa chini ya Rais Jakaya Kikwete. Mchakato wa maandalizi yake ulianza mwaka 1995 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2009.

Akizungumza na Wanahabari kwenye ofisi za Bunge, Mungai alieleza kwamba vitambulisho hivyo vipya vitatumia teknolojia ya Smart Card ambayo ina uwezo wa kuingiza taarifa nyingi za muhusika zinazoweza kutumika kurahisisha huduma mbalimbali kwa mwenye kitambulisho.

Teknolojia ya Samart Card ni ya kisasa zaidi kwani inaweza kubeba picha ya mwenye kitambulisho, alama za dole gumba, alama za kiganja, taarifa za DNA (chembechembe za urithi) , vipimo vya ndani ya macho, taarifa za elimu na nyingine, alieleza Waziri Mungai na kuongeza kwamba teknolojia hiyo imeonekana kufanikiwa sana katika nchi ya Malaysia ambako walikwenda kujifunza.

Akifafanua zaidi Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Lawrence Masha, alisema kwamba uzuri wa teknolojia hiyo mtu anaweza kuamua ni taarifa zipi zisomwe na nani kama zile zinazohusu DNA, Afya, Uhalifu, Elimu, Benki na nyinginezo.

Kwa mfano alisema si lazima mtu wa benki ajue kwamba una-typhoid, au ukienda polisi si lazima wajue mambo yako mengine alieleza Masha na kuongeza kwamba teknolojia hiyo pamoja na kuwa nzuri kuliko ile ya Barcode ambayo ilitumika katika kutengeneza vitambulisho vya kupigia kura ni ya gharama nafuu.

Kama tungekuwa tumetumia smart card kuandikisha kadi za kura ingekuwa rahisi sana kutekeleza mpango huu kwa sasa...kwa kutumia Smart card unaweza kuongeza taarifa wakati wowote tofauti na barcode alifafanua Waziri Mungai na kubainisha kwamba Benki ya dunia imeshakubali kusaidia Dola 20 milioni kufanikisha mpango huo.

Mungai alieleza kwamba katika mradi huo raia waishio nchini na wale wanaoishi nje ya nchi watapewa vitambulisho na wasio raiai ambao wanafanya shughuli mbalimbali hapa nchini watapewa vitambulisho vitakavyowatambulisha wao na utaifa wao.

Alisema mradi huo utakuwa wa kitaifa kama ulivyo wa uchaguzi mkuu na wa sensa ambao utapewa vyenzo za kuukamilisha kwa kuzingatia ratiba maalum ya utekelezaji inayoanza mwezi huu na kukamilika mwaka 2009.

Katika kuhakikisha kwamba utekelezaji wake unakwenda vyema Waziri huyo alisema kwamba utaundwa Wakala wa Usimamizi wa Vitambulisho (National ID Management Agency) unaojitegemea kwa ajili ya kuendesha mradi huo chini ya Wizara ya Mambo ya ndani kwa kushirikiana na wadau wengine.

Alisema Mradi huo utaongozwa na Kamati ya Usimamizi ya Makatibu Wakuu na Wakuu wa Idara na vitengo vinavyohusiana na mambo muhimu kwa vitambulisho vya taifa ambayo pamoja na mambo mengine itatoa mwongozo na mwelekeo wa programu za mradi.

Kazi nyingine ya kamati hiyo itahusu ufuatiliaji wa mchakato wa mabadiliko ya menejimenti, kuidhinisha bajeti ya mipango ya utekelezaji, kuhakikisha kwamba fedha zilizotengwa kwa ajili ya programu husika na kufanya mapitio ya utekelezaji wa mipango kamambe wa shughuli mradi.

Waziri Mungai alieleza kwamba kutokana na makisio yaliyomo kwenye bajeti ya mwaka 2006/07 jengo maalum limetengwa kwa ajili ya mradi huo na watendaji wakuu wa Wakala wa usimamizi wa vitambulisho watateuliwa bila kuchelewa.

Wizara ya mambo ya ndani inachukua fursa hii kutoa wito kwa wananchi waliopo ndani na nje ya nchi na wageni waliopo nchini kutoa ushirikiano ili kufanikisha utekelezaji wa mradi huu muhimu kwa taifa alitoa rai Mungai na kubainisha kwamba vitambulisho hivyo vitatolewa bure.

Mradi huo utatekelezwa katika hatua mbili ambazo ni ya maandalizi na nyingine ni ya utekelezaji. Ratiba ya awamu ya kwanza inaonesha kwamba shughuli ya uanzishaji Wakala wa Usimamizi wa Vitambulisho na uteuzi wa watendaji wakuu na uimarishaji wa kiutendaji wa kuazimwa watumishi wengine kutoka idara za serikali vinapaswa kukamilika katika kipindi cha Februari na Aprili mwaka huu.

Kwa upande wa ukamilishaji wa makusanyo ya fedha zinazohitajika kutoka bajeti ya Serikali, wahisani na vyanzo binafsi utatekelezwa kati ya Marchi na Mei mwaka huu wakati Kampeni ya kufahamisha umma kupitia vyombo vya habari, mikutano ya hadhara, semina na mikutano ya ndani itafanyika kuanzia Aprili mwaka huu hadi Juni 2008.

Ratiba hiyo inaonesha kwamba mapitio (review) ya sheria husika na kufanya marekebisho inapobidi yatafanyika katika kipindi cha Februari hadi Mei 2007 wakati jukumu la kujenga uwezo katika ngazi mbalimbali litafanywa na ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma kati ya Julai na Desemba 2007.

Hatu ya pili ambayo ni ya utekelezaji wa mradi itahusisha utambuzi na uandikishwaji itafanyika kati ya Julai na Desemba mwaka huu ikihusisha ukusanyaji wa taarifa mbalimbali, uundaji wa kamati za utambuzi, Uchapishaji wa kadi za vitambulisho, usambazaji na utoaji wa kadi za vitambulisho na uanzishaji wa rejista za utambuzi.
 
Nina wasi wasi na akina Tibaizarwa , Otieno, nk. Hapa sasa swala nani i raia na nani si ndipo linakuja lakini kwa rushwa na kujuana yote hata yanawezekana Tanzania yetu ya ajabu . Wacha tuone .

Je kwa nini baraza la Mawaziri likalie hili jambo na si Bunge ? Pesa hizi zinatolewa hazina ama ni mambo ya akina Richmonduli kuchangisha kama sherehe za Uhuru ? Naomba msaada tafadhali .
 
ooh ! here we go again ! Yaani hili suala wameliongelea tu hapo hapo "Mzee wa kuropoka" akadandia treni kwa mbele na kusema kuwa kutakuwa na mabasi ya kasi, treni za kasi na kadhalika ! Ok, tumekuelewa, vitambulisho vya uraia je ?????

Na ndio maana huwa sishangai sana, maana najua wanaongea weee halafu huku wananchi wanafurahia wakiona wadanganyika wanasahau wanaanza kuzusha nyingine ! ama kweli wao ni wao.
 
The whole Idea sounds really juicy and convincing lakini kama kawaida ya Tanzania, inaweza kuwa ni longo longo... lakini kama waliweza kuboresha passport then hii kitu inawezekana.
 
KUboresha Passport lilikuwa ni swala la kimataifa, kwani ifikapo mwaka 2010 Passport zote au Travel Document lazima zisomeke kwa Machine.

Vitambulisho vimepigwa longo longo ni sawa na vyeti vya kuzaliwa.
 
Ila hii kitu itatugharimu pesa nyingi sana, maana inabidi system zote zinazoweka kumbukumbu zifanyiwe overhauling, kuanzia Hospitali /polisi /shule /benki /ardhi/tra nk.

Na ugumu wa hili swala unakuja kuwa Tanzania hatuna mfumo wa Social Security Number kwa wananchi wote, ila nadhani watumishi wote ambao wana mifuko ya pensheni wanazo number.

Only time will be the judge.
 
Gharama ni ndogo kulinganisha na faida. Itagharimu kwa makisio karibu USD 70million. Idadi ya watanzania wote kwa ajili ya ID ni kama USD 2.00 Gharama ya passport sasa hivi ni approx. USD let say 30.00, kwa hiyo utaona bado gharama ni ndogo. Inabidi tuilipie na ifanyike kiusahihi.
 
Nadhani kuna umuhimu wa kuwa na Personal Identification Number (PIN) kama wenzetu wa Kenya walivyo nazo.

Hizi namba zitolewa mara moja mtoto anapozaliwa na ziwe zinafanyiwa update.

Hizi PIN zinaweza kutumika kutengeneza kitu kama TIN (Tax Identification Number) na Voter Registration Number (VRN)
Pia hizi namba zinaweza kutumika kwenye nyanda mbalimbali kama Hopsitalini, kwenye bima na hata kwenye mafao. pia itarahisisha mfumo wa utoaji huduma kwa jamii.

Kama zitatolewa mara mtoto anapozaliwa na kuchukuliwa finger print hapo hapo basi itakuwa ni vigumu sana mtu kugushi kwani lazima uwe na information zote za mahali alipozaliwa mtoto, hospitali, majina ya wazizi na registrar.

Hii kazi ikifanyika vizuri basi tutakuwa tumepiga hatua sana kwani hizi namba zinaweza pia kutumika wakati mtu unakwenda benki kuchukua mkopo nk.

Wanatakiwa pia waingize kitu kingine kama Personal Education Number (PEN) nk.
 
Jamani hivi vitambulisho ni kama credit card (smart card), inakuwa na details more ambazo zinaweza kuonekana na idara zinazohusika tu. Hata UK wanaanza kuwa nazo kuanzia hivi karibuni.

Aljazeera

Mimi sipo huko jikoni lakini jinsi walivyoeleza vilumbwengo vyote hivyo vinaweza kuwekwa humo kwenye hiyo card. JK alipokuwa UK aliongelea hili kwa ufasaha na halina longolongo kwani hata kampuni ya kufanya hiyo kazi ilitangazwa.
 
Mimi nazungumzia gharama ya kubadilisha system nzima mfano mzuri ni polisi, ukifungua kesi sidhani kama huwa wanatunza kumbu kumbukwenye computer bali ni kwenye majarada.

Sasa pindi hivi vitambulisho vitakapoanza kutumika inamaana kuwa polisi itabidi wa upgrade system yao means new computers/kutrain watu kwenye every single police post(kumbuka baadhi ya vituo havina umeme).
 
Sijui kama ilishapostiwa...

Tanzania Chooses Digimarc for Voter ID Program Digimarc supplying secure ID materials for Tanzania voter identification program

Beaverton, Ore. May 1, 2007
Digimarc Corporation (NASDAQ: DMRC) today announced it was recently selected by the Tanzanian National Electoral Commission to provide secure ID materials for the photo registration of eligible voters around the country. The Digimarc solution is helping Tanzania with ongoing registration of new voters for national and local elections at thousands of locations nationwide.

"Digimarc is playing a growing role in helping countries across the African continent to improve the identity management and credentialing systems that support a range of critical government functions, including elections, national ID systems, and driver licensing," said Bob Eckel, president, government programs, Digimarc Corporation. "We are pleased to be working with Tanzania to bring secure voter credentials to its citizens as a means to take part in future elections."

Digimarc secure citizen identification and credentialing solutions are well-suited to the needs of African nations. Digimarc secure ID solutions are used currently in several key driver license programs in Africa, including Botswana, Ghana, Lesotho, and Mozambique.
About Digimarc

Digimarc Corporation (NASDAQ: DMRC), based in Beaverton, Oregon, is a leading supplier of secure identity and media management solutions. Digimarc provides products and services that enable the annual production of more than 60 million personal identification documents, including two-thirds of U.S. driver licenses and IDs for more than 25 countries. Digimarc's digital watermarking technology provides a persistent digital identity for various media content and is used to enhance the security of financial documents, identity documents and digital images, and support other media rights management applications.

Digimarc has an extensive intellectual property portfolio, with more than 300 issued U.S. patents with more than 6,000 claims, and more than 500 pending U.S. and foreign patent applications in digital watermarking, personal identification and related technologies. The Company is headquartered in Beaverton, Oregon, with other U.S. offices in Burlington, Massachusetts; Fort Wayne, Indiana; and the Washington DC area; and international offices in London and Mexico.

Please go to www.digimarc.com for more company information.
Press Contacts
Leslie Constans
 
If this tender has been won freely and fairly it could well be the first that has been awarded freely and fairly, in the history of TZ ie. NO 10% .What is happening regards the National Identy Cards that is also long overdue.Can they not agree to combine the two in one exercise?
 
Mzee Mwanakijiji,

Samahani mkuu lakini hao Digimarc Corporation mara nyingi vitambulisho vyao ni Bomu, yaani rahisi sana kutoa fake copy inayofanana na ikatumika. Kwa wale wanaoujua mipango ya Pass na vitambulisho watakubaliana nami kwamba hakuna nchi ngumu kutengeneza fake copy ya vitambulisho na pass za Canada. Sina mapenzi ila ndio ukweli maanake wajanja wengi nawajua na husema wenyewe!
Nimeyasema leo hii mtakuja nambia kama hamtakuta Wazaire, Wakenya na Rwandese wamevibeba mikobani!
 
Mkandara,MJJ,Kichuguu,Mugongo,defunkadelic,Mswahili,Nungwi,Dua....

....FINALLY!!.....hii dili nameanza kuisikia tangu enzi za Lyatonga Mrema. Nasikia mtoto wa kiraracha alitaka kukata mshiko wake wajanja "wakamsinya."

Kuna anayemjua DALALI wa hao Digimarc, Tanzania? Hakuna kampuni ya kigeni inayofanya biashara Tanzania bila kuwa mwenyeji behind them.

Nasikia hata dili la kuchapisha noti Tanzania ukitaka kuliingia hilo utaivaa chupi kichani.

Mkandara,
kama wasomali,wazaire,warundi,... watavipata hivyo ni kwasababu maofisa wetu wamewapa mkononi. Unakumbuka wale wabunge wa CUF? Hivi kesi yao imeishia wapi?
 
Mkandara.... kuna data zozote ambapo vitambulisho vya Digimarc vimewahi kulalamikiwa. Sijui waliwezaje kushinda tenda, na walipammbanishwa na makampuni gani? Sijui pia hii tenda ni ya kiasi gani!!
 
Kama Pass Mpya zinagushika ni hivi vitambulisho.

Tanzania tuna tatizo moja nalo ni kufanya kila kitu bila kufikiria miaka ijayo.

Mfano si mwaka 2005, walitoka na Permanent Voter Registration (PVR) na watu tayari wana vitambulisho vya kupigia kura?

Nadhani kitu cha kwanza cha kufanya ni kutoa Vyeti vya Kuzaliwa visivyogushika.
 
Mzee Mwakijiji,

Wewe opo jikoni umeona jinsi DC, Shy town na kwingineko wanavyochapisha vitambulisho. Mimi mwenyewe nimewahi kuwa nacho miaka hiyooo nilipokuwepo huko.

Insurance card na Driver's licence zenu nyingi toka states tofauti zinatengenezwa na hawa jamaa. Ushahidi gani tena hali unajua fika kuliko mimi hapa, na kama Unakumbuka vikao kibao vimefanyika kuhusu kuimarisha vitambulisho vyenu na bado watu wanavifyatua kama nguo za China.
 
Mkandara..hivi vya wamarekani vinaghushika bwana... ina maana hivyo vya Canada havigushiki kabisa au inategemea na kampuni inayotengeneza?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom