Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,254
Sijui basis ya maamuzi yetu inatoka wapi, maana sijakutana na taarifa yeyote ya utafiti inayohalalisha umuhimu wa huu mradi wa vitambulisho vya taifa. Lakini nimeona dada Meghji ametumia sehemu ya kutosha katika bajeti yake kuelezea hili jambo. Kilichonichosha zaidi ni sababu za huu mradi zilizotolewa na dada Zakia. Yeye anasema sababu mojawapo ni kuimarisha demokrasia. Sasa nimekuwa najaribu kufikiria link kati ya viambulisho na demokrasia, kwa kweli sijaona. Sana sana nimeona katika nchi zingine sababu moja ya kukataa kuwa na IDs ilikuwa ni kwamba IDs zinaingilia uhuru wa watu (freedom/liberty). Sasa sisi hii kwamba IDs vinasaidia kuleta demokrasia tumeitoa wapi?
Kwa maoni yangu, hii project haina maana, ni ghali pasipo na sababu za msingi na yafaa kabisa ipigwe chini!
Nyie mnasemaje?
Ni project ya muhimu lakini ilitakiwa isubiri mipango mingine ya kimaendeleo yenye umuhimu wa haraka imalizike kwanza. Na siyo tu imalizike kwanza, bali imalizike kwa ubora na viwango vya juu, maana hela ambazo zingeelekezwa kwenye vitambulizo zingeliweza kuelekezwa kwenye ubora wa mipango ambayo tunahitaji sasa hivi.
Zoezi kama hili la vitambulisho lingeweza kuletwa hata mwaka 2030, ambapo lingekuwa rahisi zaidi kufanyika, kuanzia gharama na hata teknolojia inakuwa imebadilika na kuoana na mazingira yetu ya kimaendeleo ya wakati huo.