Tanzania National Identities

Mpango wa kuwa na vitambulisho vya kitaifa:

  • Ni Nzuri

    Votes: 204 58.5%
  • Ni Mbaya

    Votes: 146 41.8%

  • Total voters
    349
Sijui basis ya maamuzi yetu inatoka wapi, maana sijakutana na taarifa yeyote ya utafiti inayohalalisha umuhimu wa huu mradi wa vitambulisho vya taifa. Lakini nimeona dada Meghji ametumia sehemu ya kutosha katika bajeti yake kuelezea hili jambo. Kilichonichosha zaidi ni sababu za huu mradi zilizotolewa na dada Zakia. Yeye anasema sababu mojawapo ni kuimarisha demokrasia. Sasa nimekuwa najaribu kufikiria link kati ya viambulisho na demokrasia, kwa kweli sijaona. Sana sana nimeona katika nchi zingine sababu moja ya kukataa kuwa na IDs ilikuwa ni kwamba IDs zinaingilia uhuru wa watu (freedom/liberty). Sasa sisi hii kwamba IDs vinasaidia kuleta demokrasia tumeitoa wapi?

Kwa maoni yangu, hii project haina maana, ni ghali pasipo na sababu za msingi na yafaa kabisa ipigwe chini!

Nyie mnasemaje?

Ni project ya muhimu lakini ilitakiwa isubiri mipango mingine ya kimaendeleo yenye umuhimu wa haraka imalizike kwanza. Na siyo tu imalizike kwanza, bali imalizike kwa ubora na viwango vya juu, maana hela ambazo zingeelekezwa kwenye vitambulizo zingeliweza kuelekezwa kwenye ubora wa mipango ambayo tunahitaji sasa hivi.

Zoezi kama hili la vitambulisho lingeweza kuletwa hata mwaka 2030, ambapo lingekuwa rahisi zaidi kufanyika, kuanzia gharama na hata teknolojia inakuwa imebadilika na kuoana na mazingira yetu ya kimaendeleo ya wakati huo.
 
Kwa wanaofahamu, wilaya ya Temeke ndiyo ilikuwa ya kwanza kuanza kuandikisha vitambulisho vya uraia.

Swali:
Inakuwaje kama mtu alijiandikisha na wakati anapewa taarifa ya kwenda kuchukua kitambulisho, anakuwa mbali na eneo lake kwa muda uliopangwa kwenda kukichukua?

Msaada tafadhali.
Vipi kuhusu usalama wa kitambulisho kama hakikuchukuliwa kwa muda uliopangwa?
 
Mpango mzuri, na mikakati inasomeka, ila tu, mimi naona issue mpya itakayofanana na ile ya escrow. Ndugu zangu mtakaopata hizo nafasi punguzeni tamaa tujenge nchi yetu...
 
Nitapataje kitambulisho cha taifa au cha mpiga kura? Nipo hapa dar es salaam
 
Huu mpango ulikuwa zimamoto ..au ndo watu wamesha fanya Yao ? Maana sijaskia siku nyingi sana hili suala likizungumziwa
 
Ni kuhusu kutoonekana wazi saini katika vitambulisho (ID):
Kwangu mimi ili mradi saini ziko ndani ya ID sioni ni katika hali ipi tutakwama kwa sababu ya kukosa saini ya kuonekana wakati picha ipo, namba ya ID ipo (yenye taarifa nyingi umri, unapoishi, ..) na zaidi tunajua penye matumizi mabaya ya ID saini ikionekana inaweza ikaigwa isigundulike kirahisi mpaka Police Identification Bureau. Naamini Rais wetu hakuwa na taarifa zote kamili alipozungumzia suala hili. Kwa sasa mtu hawezi kuiga saini kwa sababu haioni. Hakuna wasiwasi 100% pale ambapo kuna mashine ya kusoma ID na itasaidia zaidi kama saini ikifichwa ndani ya ID. Yafuatayo hapa ni kwa pale ambapo hakuna mashine ya kusoma ID. Katika matumizi ya ID, mara nyingi itategemea mahitaji ya ID:-
  1. Kawaida mtu ataonyesha ID yake, namba ya ID itanukuliwa na atasaini mahala na ataacha hivi viwili kama kumbukumbu halafu mtu atarudishiwa ID yake, atapata huduma, ataondoka na ID yake. Kama saini inayoonekana kwenye ID, mhalifu ataigushi na kujulikana ni baada ya muda na utaratibu mrefu hadi agundulike (ikibidi hadi Police Identification Bureau). Kama saini iko ndani ya ID, saini yake haitagushiwa na hivyo akisaini ni rahisi kujulikana haraka baadaye ikibidi kwa kupeleka/kutuma namaba ya ID palipo na mashine ya kusoma ID.
  2. Kama ni kuhusu kesi, mfano Polisi, mtu ataonyesha ID yake, namba ya ID itanukuliwa na atasaini mahala, anapata huduma halafu ataweza kuondoka na ID yake au ID yake itabaki hadi shauri liishe. Kama saini inaonekana kwenye ID, mhalifu ataigushi na kujulikana ni baada ya muda na utaratibu mrefu hadi agundulike. Kama saini iko ndani ya ID, saini yake haitagushiwa na hivyo akisaini ni rahisi kujulikana haraka sana baadaye ikibidi kwa kutumia mashine. Tukumbushane kuwa mara nyingi sehemu za matukio haya zitakuwa na mashine ya kusoma ID.
Kwahiyo, utaratibu wa sasa uendelee. Kwangu mimi ni itasaidia zaidi kuwa na ID yenye picha na namba ya ID (ambayo ina taarifa nyingi; umri, unapoishi, nk.) huku mtu akidanganya saini itajulikana haraka na mara moja uki-peleka/tuma namba ya ID palipo na mashine ya kusoma ID.
 
Jamani hivi vitambulisho ni kama credit card (smart card), inakuwa na details more ambazo zinaweza kuonekana na idara zinazohusika tu. Hata UK wanaanza kuwa nazo kuanzia hivi karibuni.

Aljazeera

Mimi sipo huko jikoni lakini jinsi walivyoeleza vilumbwengo vyote hivyo vinaweza kuwekwa humo kwenye hiyo card. JK alipokuwa UK aliongelea hili kwa ufasaha na halina longolongo kwani hata kampuni ya kufanya hiyo kazi ilitangazwa.
Haya!
 
Hivi hakuna utaratibu wa kuangalia taarifa zako za kwenye kitambulisho cha uraia kama ilivyokuwa cha mpiga kura kwa njia ya simu ?
 
Hizo ID zilizozungumziwa na huu uzi mkongwe ndio hizi walizotoa NIDA kuanzia 2015?
 
Back
Top Bottom