Tanzania National Football Team (Taifa Stars) | Special Thread

Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania almaarufu kama Taifa Stars, muda mfupi ujao itajitupa uwanjani kupambana ugenini dhidi ya Zimbabwe. Huu ni mchezo wa marudiano katika hatua za awali za Kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika. Katika mchezo wa kwanza uliorindima Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam, Taifa Stars iliizaba Zimbabwe bao 1-0-bao la John Raphael Bocco.

Leo hii,Taifa Stars itahitaji sare au ushindi wa aina yoyote ili kuweza kuendelea na hatua inayofuata. Mechi husika itaanza saa kumi kamili jioni kwa saa za hapa nyumbani. Watanzania tuiombee na kuipa nguvu Taifa Stars ili iweze kusonga mbele.

cc Jamal Malinzi
 
Last edited by a moderator:
hizo ndo jezi ambazo watu wanazilalamikia? Mbona sioni ubaya wake.. Wanaozilalamikia walitaka ziwe za aina gani? Ingawaje hazina rangi zote 4 za bendera ya taifa, zipo poa sio mbaya sana wala sio nzuri. Kitu kingine wachezaji wanaonekana wamepanda au ni ufundi wa kamera? Kidogo niseme naangalia timu moja toka afrika magharibi. Miaka yote nimezowea kuona wachezaji wetu wana maumbile ya lishe la unga-robo usicheze mbali hapa wanaonekana kila mtu at least kala na kushiba. Hii nzuri sana.
tunataka jezi ambazo ambazo zitakuwa na mchanganyiko mzuri wa rangi za bendela ya taifa cc jamali malinzi
 
Back
Top Bottom