Tanzania National Football Team (Taifa Stars) | Special Thread

Kumbe hii ni mechi ya kukamilisha ratiba. Nigeria na Tanzania hawana nafasi ya kukwalifai kwenda Gabon. Hovyo!!!!!
 
Bongo tupo nyuma kila kitu isipokuwa Kuchonga. Kuchonga kwenyewe labad tutashindwa tukiingia katika mashindano ya kuchonga.
 
Naona msaada umebaki kwa kipa tu wengine hawa wakitishiwa chenga wanapeleka makalio!
 
Naona anatangaza kupitia Beinsports sijui ni channel gani. Naangalizia online jamaa ana accent ya kibritish. Namsifu kwa kuyatamka majina yetu yanayoanza na "M" vyema eg "Msuva" maana huwa inakuwa vigumu hasa kwa mtu asiye mwafrika kumfundisha jinsi ya kuyatamka bila kuvunja mfupa wa ulimi.
Safi sana!
Vijana wamekaza, safi mno!
 
Kibongo zaidi.....Makipa wangekuwa na soko kama wachezaji wengine kipa wetu angepata soko..
 
Back
Top Bottom