Tanzania nakupenda, sipendi majigambo

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Natafakari maelezo yangu haya, Naomba Mods au mwenye Clip ya ule wimbo wa Tanzania nakupenda aueke hapa.

Tumetoka mbali wote pamoja, safari ya matumaini ilianza vyema leo tumegeukana, hakuna majibu kuna kulaumiana tu. Hajulikani mzazi ni yupi ama mlezi au nani mwenye jukumu la kuondowa matatizo yetu. Hapo ndipo naukumbuka wimbo Tanzania nakupenda.

Maisha maisha maisha yetu, sisi ni wa kujuta tu ,ama kweli tuna bahati mbaya watanzania. Sidhani kama ni kweli,siamini macho yangu, aaah basi tu, si wewe Tanzania yetu au nimesahau?
Mbona giza tele narudi nyuma hivi badala ya kusonga mbele inakuwaje sisi? Hapana Tumerithi ugonjwa ule ule ,natamani ingekuwa vyengine .Nakupenda Tanzania

Majingambo yanaendelea kila siku, majiko hayafuki moshi unaona upepo , watu wamejinamia kwa makundi mitaani wengine wamebeba mafurushi barabarani yamewapita kimo, ukiwauliza hawajui wanakwenda wapi wanakwambia wanaitafuta nyimbo yetu ya nakupenda Tanzania.

Mara sauti la ngurumo linakuja "fanyeni kazi" aah kwa upole wanyonge hawa wanauliza ziko wapi hizo kazi jamani? masikini Tanzania lakini nakupenda. Basi watu wananyamaza ,huku wakisindikizwa kwa mziki wa kupotea wa nakupenda Tanzania.. machozi yanakaribia kutoka,


Vijana wadogo, wazee na watoto wamebeba bendera ya Tanzania, wanaimba na kuipunga bendera kuashiria matumaini. "Sitakusahau wewe, kwa ulivyo barikiwa..... nakupenda, nakupenda...." jamani.


"Hapana si bure , tujiulizeni maana mwenye kujiuliza hajuti" hii ni sauti ya wanyonge. Lakini huo ndio msamiati wetu kila baada ya muda na watanzania ndivyo tulivyo. Tuendelee tu kuipenda Tanzania

Mwisho.

Leo nimekuja hivi(mnisamehe)

Kishada
 
Back
Top Bottom