Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

A

Acha munyooshwe muache kuandika mambo ya kijinga jinga.
Hata hivyo mlikuea mnapata shushu saana kwenye hivyo vifurushi kama 3000vunapata gb1.2,
Hap mimi sijaona mabadiliko yoyote kwa sababu toza mwaka jana wote natumia kifurushi cha wiki 3000 kwa gb 1tu na 5000 gb 2 tu na bafo nakiona kupo vilevile.
Muda wa maongezi ni uleule haujabadilika kwa hiyo kumbe tuliumia kubishana na watu waliokuwa wanapata unafuu kwenye bando.
Una akili fupi sana
 
Hivi hakuna njia mbadala ya kupata internet tofauti na hii mitandao simu? mimi hapa bado limeisha toka jana na sina mpango wa kuangaika na hivyo virushi vyao ni mwendo wa freebasics tu.
 
View attachment 1740133
Royal bando

View attachment 1740134
Mega bando kwa wiki

View attachment 1740136
Internet kwa wiki

Kwa mabadiliko haya ya vifurushi kwa nini Waziri Ndugulile asijiudhuru kwa kuudanganya Umma wa Watanzania. Tuliaminishwa kwamba vifurushi vitapatikana kwa gharama nafuu, imekuwa kinyume chake.

Kwa heri Halotel, niliwapenda lkn ndo basi tena. Na jana nimetoka kuwapigia chapuo kuwa mko vizuri, kumbe sikujua masaa machache yajayo ingekuwaje.

Baada ya kutoa yangu moyoni, tujuzane wapi pa kukimbilia kwa sasa.

Akuna kwenye unafuu mkuu,hata huku upigaji umebalikiwa kwa kina la Ndugulile,naanza kutumia simu ya tochi soon.
 
Mambo!
Kutokana na tabia za uhuni na wizi wa mitandao ya simu nimejikuta nina laini za simu kwa kila mtandao (unaoshika maeneo niliyopo)

Sasa tangu juzi nimekuwa nikipokea ujumbe kutoka mitandao hiyo kwamba kutakuwa na mabadiliko ya maboresho ya vifurushi kuanzia tarehe 02-Aprili-2021

Jumbe hizo hazikuja kibahati mbaya kwani kabla yake au baada yake tayari vifurushi vilishavurugwa vurugwa kwa dakika kupunguzwa bei kupanda na ofa kuondolewa

Sasa tangu saa tisa nimekuwa nikiangalia menyu zao ila hakuna cha maana nilichoona kimeboreshwa kufanya nifurahie huduma kama zamani

Mfano Vodacom wameondoa supa uni na ofa ya ya kwako tu, Zantel ndo uozo kabisa maana kutoka dk160 hadi dk 35 sasa wameona haitoshi wamepunguza mpaka sasa ni dk30 tu, Tigo ndo nimeona kwa haraka haraka kuna dk 75 eti

Ninamiliki laini za Airtel, Vodacom, Tigo, Zantel, TTCL na Halotel; Je, ni mtandao gani una nafuu katika maboresho yake ili nihamishie majeshi huko?
Vodacom wameua brand hata freebasic hutumii
 
Ingekuwa mataifa yenye watu, CEO wa TCRA angekuwa ameshakabidhi ofisi, waziri angekuwa ameomba radhi na kung'atuka; kwa kuwa sisi ni 'NYANI ',.

Kote duniani sayansi halisi inapunguza ukali wa maisha, huku NYANI Land tuna sayansi yetu ya kichawichawi, yenye kutia nuksi kila jema wanalobuni 'WATU'.

Wanasiasa wa inji hii ya 'NYANI LAND' wamelaaniwa!

Kila juhudi wanayofanya inageuka kuwa mwiba kwa wananchi.

Nakumbuka kuanzia sukari, mafuta, n.k.
 
Leo tarehe 1/4/2021 makampuni ya simu yamefanya mabadiliko makubwa katika vifurushi vyao.

Wamepunguza vifurushi kwa kiasi kikubwa hasa vifurushi vya data, sitaweka hapa kifurushi kimoja baada ya kingine lkn kwenye mitandao yetu hilo lipo.

Nenda kwenye menu tu nadhani utakutana na upuuzi wote.

Nini nataka kusema?

Wakati dunia inakimbia kwa kasi kwenye technolojia sisi tunajirudisha nyuma tena kwa kasi kubwa na wala hapa siyalaumu haya makampuni ya simu kwani yenyewe yanapokea tu order toka Serikalini.

Kama wananchi wa kawaida kabisa tunaiomba Serikali iweze badilisha hiv vifurushi haraka sana maana wanachokifanya ni kurudisha juhudi za maendeleo ya kisayansi nyuma.

Na kwa vile tuna Serikali mpya nina hakika watashughulikia hili haraka sana na wala hawatasubiri hadi mwezi upite maana kilichofanyika ni zaidi ya upuuzi wa hali ya juu.

Kama Serikali itashindwa rekebisha hili basi tutajua hamna mpango na wananchi wa kawaida na mengi mnayoyaongea ni porojo tu

Naomba kuwasilisha.
Hili ni janga lililoadaliwa na Dr Mpango waziri wa fedha kupora kupora kudi badala ya kukusanya.
Lilichangiwa na yule aliyetamani kuifunga mitandao na badala yake aliazimu kuweka kodi kubwa kudhibiti watumiaji wa mitandao.
 
Wakuu,

Kama kweli tunaamini katika uhuru wa mawazo kama haki ya kikatiba, na kama kweli tunaamini katika uwajibikaji wa viongozi, basi naomba huyu waziri Ndugulile asome ninayoandika kama jinsi yalivyo.

Wewe waziri Ndugulile, waziri mwenye dhamana kwa niaba ya serikali; una akili timamu!?

Nauliza swali? Unazo zilizotimia?

Hivi, zile mbwembwe zote za kujigamba na kujitutumua kwamba mtahakikisha vifurushi vinakuwa vya bei nafuu, ndio matokeo yake haya tunayoyaona hapa?

Yaani wewe waziri, unaweza kuwafanya watanzania milioni zaidi ya sitini kuwa ni wapumbavu na mbumbumbu?

Ukakimbia kwenda kujitungia kanuni haramu na za kitapeli ili kuhalalisha wizi?

Ulisikia wapi dunia ya leo, data zinakuwa ghali namna hii?

Katika nyakati za utandawazi ambapo maisha yote yanategemea digital devices, kwanini ufanye uhuni wa namna hii?

Sifahamu lengo ni nini? ama ni mbinu za kubinya watu wasipate access ya mtandao?

Ndugulile, nikueleze tu kwamba, maisha ya watanzania wengi hayazunguki kwenye muhimili wa siasa pekee.

Kama lengo ni kuwabinya watu kisiasa, basi hilo ni lengo mfu lisilo na uhalisia.

Mitandao ndio maisha yetu, ndio chakula chetu na kipato chetu. Tusivurugane.

Tunahitaji vifurushi vishuke bei. TAFADHALI.

Kwa vision yake ya kumfurahisha boss ndio maana wakati fulani alidai wanafikiria namna waanze kutoza malipo kwa watumiaji wa whatsapp
 
Tupaze sauti zetu kwa nguvu kuwa nafasi aliyopewa ya uwaziri wa mawasiliano haimfai. Aondolewe apelekwe kwingine. Ameumiza Sana wananchi na Bei hizo za vifurushi. Wachache watamudu mawasiliano
Tupaze sauti zetu kwa nguvu kwa njia zote zinazowezekana, Nina Imani Rais atasikia kilio chetu Kama alivyomuhamisha Jafo.
 
App zisizo za msingi ni zipi?

Kati ya hizi
1.Twitter
2.whatssap
3.instagram
4.jamii forum
4.Telegram
Whatsapp mbadala telegram. Ondoa Whatsapp

Instagram binafsi siielewi kabisa, piga chini.

Twitter, JF na Telegram ndio apps nilizonazo na zinanitosha.
 
Subiri j4 mkuu Kama mama hatosikia kilio hiki bas ajiandae hyo wazir

Atambue tu nguvu ya mitandao na technolojia n kubwa kushinda nafas alyonayo

#NDUGULILE OUT
 
Hii ni tweet ya mtu anaejitiasa Baba Mwita:

Kitu ambacho Serikali mnatakiwa kufanya; punguzeni Kodi mnazotoza kwa Makampuni ya Simu, wao watashusha bei za Vifurushi, watumiaji na wanunuzi wa Vifurushi WATAONGEZEKA; in return, mtaingiza Kodi nyingi. Hizi sarakasi mnazotaka kufanya — ZITAWASHINDA. Tumieni AKILI sio NGUVU.

Maoni yangu:
Kama hawa ndio wanatuongoza mpaka leo hii, huwa nashangaa watu wanaohoji kama wapinzani wanaweza kuongoza hii nchi.
 
Back
Top Bottom