Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Maisha magumu gb moja elfu tatu si Bora nile nyama, kwa mtindo huu serikali itazidi ku loose Kodi na makapuni ya simu, Mimi mwenyewe nitaacha kutumia mitandao ibaki jf
Mbona halotel gb 1 na mb 500 ni sh. 1500 tu?
 
Baada ya kupandishwa kwa vifurushi vya data kwa namna ya ajabu na ya kiharamia, ni wazi sasa lazima kuwe na namna ya kuyawajibisha haya makampuni.

Haiwezekani kabisa waziri ufanye uhuni wa aina hii bila kutizama hali halisi ya wananchi na mustakabali wa uharamia ulioufanya.

Halafu unatuhadaa kwamba unarekebisha? Kwa kutuona kwamba sisi ni wapuuzi tusio na ufahamu?

Bunge linapaswa kuingilia kati na kutoa mwongozo wa kisheria kuhusu kanuni zilizotungwa na huyu waziri muovu na waliomtuma.

Kwanza kabisa, ni Kanuni zilizo kinyume na Katiba na Kinyume na sheria za mawasiliano na habari.

Alijifungia tu chumbani na wahuni wenzie kupanga mkakati wa kidhalimu bila kutizama athari zake pana.

Kama hii ni conspiracy ya kuzima sauti za watu, basi inapaswa kutizamwa upya.

If you have issues with government critics, please deal with them on personal basis. There are cyber laws in place.

Maisha ni zaidi ya siasa. Hatuwezi kuwa watumwa wa siasa za kuziba midomo hata wasiohusika.

Tafadhali, BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linapaswa kuchukua immediate measures kurekebisha huu uharamia na uovu wa ndugulile na watu wake.

Na mahakamani tutaenda pia kama bunge litashindwa kufanya kazi yake haraka!
 
Na unlimited data, ni kiasi gani, haya mambo ya kupangikiwa pangiwa wakati mwingine yanakosesha watu fundamental freedoms za maongezi, kuwasiliana na kuishi bila pressure kupanda au kushuka.
 
Jero tu nilikuwa napata mb 500 na dakika 50 na sms juu. Kilichokuja sasa. unaweza sema unaota kumbe ndo unaishi hivyo..🤣🤣
 
Vimepandaa vyote dah hapo ndo siwezi kufatilia tutorials mbalimbali YouTube aisee imekula kwangu, acha niwe mtumiaji wa jf tu.
Halotel laini ya chuo
Screenshot_20210401-134437_Phone.jpg
 
Hawajui data ndio sehemu pekee mnyonge anapojipatia faraja. Ulevi wa bia tumehamishia katika Data na Internet na wengine ndio tunapata taarifa na michongo mbali mbali humu
Mimi hufatilia masomo na kujifunza huko YouTube Sasa kuongeza gharama Mara dufu ni zaidi ya ychawi, mama Samia aangalie hii Hali, Kama ile ya kwenye makodi Hadi watu wakafunga biashara ndio wakaja kugutuka.
 
Unaitumia katika mtandao upi? Maana nachojua ipo Tigo na Voda ambako huoni picha hata moja ila Voda wamelimit kuwa hutumii zaidi ya 50MB per day😁
Natumia Tigo naona Pich na Video kasoro ku-upload picha tu ndio siwezi.
 
Naanzisha rasmi kampeni ya kuhakikisha tunapata Waziri mpya wa Teknolojia baada ya huyu aliyepo kushindwa kwa makusudi kudhibiti bei ya vifurushi mitandaoni .

View attachment 1741015

Ewe mwananchi ni jukumu lako tena la haki kuhakikisha viongozi wabovu wanang'oka kwa namna yoyote ile ili nchi yetu isonge mbele , Madaraka ni kama mbio za kupokezana vijiti , Ndugulile ameshindwa kuwasaidia wananchi hivyo ni vema akang'oka ama akang'olewa .

Mungu ibariki Tanzania .
Sidhani kama Ndugulile ana kosa, yeye ni mtekelezaji tu kama wengine muhimu tupambane mitandao ya simu ipunguziwe kodi vifurushi vitashuka automatically. Mitandao ya simu inatozwa kodi kubwa sana ambayo inasababisha gharama kupanda na kuumiza watumiaji wake. Ndugu yangu unafikiri 2T aliyoitamka jana Dr Mpango itapatikana kwa miujiza, matunda ya hiyo 2T ndiyo haya...
 
Back
Top Bottom