Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Na sisi kama watumiaji lazima tufanye Counter attack.

Tuhamasishane Mei Mosi kususie huduma zao zote za internet mpaka watakaposhusha bei.
 
Mimi hili nilianza kuliona huku voda tangu waliposhusha kifurushi cha jimwage cha wiki kutoka kupewa 4gb kwa 5,000 mpaka 2gb. Namimi katika kujibu mapigo nilichofanya ni ku uninstall instagram with immediate effect! Sasa hiyo 2gb naitumia jf na whatsapp tu na inabaki..! Sasa nasikia hata hiyo ya 2gb kwa 5,000 nayo wanaiona nyingi, wanaifuta sijajua wataleta nini ila niwahakikishie tu na mimi sitakubali, lazima nile nao sahani moja. Kama vipi tunarudi kwenye sms tuu kwani nini bana..?
Kuanzia Mei mosi tususie huduma zao zote za internet.

Wasituone sisi wajinga kutuibia pesa zetu za ngama tukawaacha hivi hivi....we must respond!

Mark the date, Mei Mosi
 
Hii mitandao ya Simu inatufanya watumiaji Mazuzu sana, wanajipangia wanavyotaka tu

Ushirikishwaji au uchukuaji wa maoni kuhusu bei za vifurushi hawana

Utaratibu wa wapi sijui huu
 
Mmmh kitaisha but nataka nipunguze machungu kwanza
kwa kweli....
Screenshot_20210401-131825~2.jpg
Screenshot_20210401-131825~2.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
View attachment 1740411
 
Back
Top Bottom