Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Ewe Mwenyezi Mungu ni kwanini hukutupa Sisi Wanadamu Uwezo wa Kuusoma na Kuuona Moyo wa Wanadamu Wenzetu mapema ila kama tukijua ni Wanafiki basi tusitoe hata Ushirikiano wowote Kwao?

Kuna Mtu nilimwamini mno hadi nikapambana pamoja na Watu wengine ili asipokonywe Tonge lake huko Kigamboni nikiamini kuwa hatokuja kutusaidia tu Sisi tuliomsaidia lakini hasa atakuja kuwa Msaada kwa Watanzania wengi na alichokifanya ni tofauti na Mcha Mungu wa kweli ambaye ana Uchungu na Huruma na Watanzania wengi.

Sasa nimeshajifunza kutowaamini Watu.
 
Tatizo sio waziri pekee.
Tatizo ni TCRA na mamlaka zote husika.
Regulator wa haya makampuni ni TCRA, na kama walikaa kikao tulitegemea TCRA angesimama kwa manufaa yetu, sasa hapa hesabu ni hv

waziri + TCRA + makampuni ya simu = Bei mpya

Wachawi wetu hapa ni wizara husika na TCRA
Makampuni yanafuata miongozo na makubaliano na hizo mamlaka hapo juu.

Namna pekee ya kufikisha ujumbe kwa kasi ya mwanga ni kufanya boycott.
 
Hivi hakuna njia mbadala ya kupata internet tofauti na hii mitandao simu? mimi hapa bado limeisha toka jana na sina mpango wa kuangaika na hivyo virushi vyao ni mwendo wa freebasics tu.
nimejipooza na free 7gb kwa siku 14 yani 500 kila siku ndani ya siku 14 airtel, simu ya 4g kama hujawahi kutumia hizi gb7 zao za bure nazani ni wakati wake nimeanza nanzo leo wakati nasubiri waziri husika asikie kilio cha wanyonge
 
Kazi ndo inaanza
FB_IMG_16173553811028400.jpg
 
Aachie kiti watu wanaojitambua bana, we don't need poor thinking kind of Ministers! Ulimwengu wa leo ambao kila kitu ni mtandaoni, loss report, biashara, usajili mbali mbali halafu analeta hujuma za kijima namna hii!

#Ndugulile OFF
 
Hii ni tweet ya mtu anaejitiasa Baba Mwita;

Kitu ambacho Serikali mnatakiwa kufanya; punguzeni Kodi mnazotoza kwa Makampuni ya Simu, wao watashusha bei za Vifurushi, watumiaji na wanunuzi wa Vifurushi WATAONGEZEKA; in return, mtaingiza Kodi nyingi. Hizi sarakasi mnazotaka kufanya — ZITAWASHINDA. Tumieni AKILI sio NGUVU.
Ndio akili imetumika hapo, unapiga sehemu ambayo haikwepeki sio unapiga sehemu ambayo mtu ana option. Hapa watu watalalamika ila watanunua tu vifurushi.
 
Kweli kabisa, Kama nchi ni ya Wananchi basi bwana ndugulile must resign haraka iwezekanavyo. Amefeli.
 
Tupaze sauti zetu kwa nguvu kuwa nafasi aliyopewa ya uwaziri wa mawasiliano haimfai. Aondolewe apelekwe kwingine. Ameumiza Sana wananchi na Bei hizo za vifurushi. Wachache watamudu mawasiliano
Tupaze sauti zetu kwa nguvu kwa njia zote zinazowezekana, Nina Imani Rais atasikia kilio chetu Kama alivyomuhamisha Jafo.
Tunaita wengine mabeberu, kumbe mabeberu halisi yapo !!
 
Back
Top Bottom