Tanzania na Vifurushi vipya vya Data na Sauti (Aprili 2021) - Mwitikio wa wananchi

Sina mengi ya kuongea ila kupitia vifurushi vya mitandao vya kila mtumiaji simu hapa nchini, ipo sababu ya kumuwajibisha kwa kile kinachoonekana dhahiri kuwa ni maumivu tuliosababishiwa kwa makusudi. Dhamira ya mtu kupewa dhamana sio kuumiza watu bali ni kuhakikisha usimamizi mzuri wa maslahi ya raia kwa ujumla. Naamini raisi wangu u msikivu na utalifanyia kazi hili.
Tuzidi kufanya maombi ili naye asivimbishe kichwa
 
Naanzisha rasmi kampeni mitandaoni ya kuhimiza na kumshauri Mh. Rais Samia kututafutia Waziri mwingine mwenye kujua matatizo ya Watanzania aongoze Wizara ya Mawasiliano. #Ngugulile#Out#.
Mjomba alishaondoka
 
Leo tarehe 1/4/2021 makampuni ya simu yamefanya mabadiliko makubwa katika vifurushi vyao.

Wamepunguza vifurushi kwa kiasi kikubwa hasa vifurushi vya data, sitaweka hapa kifurushi kimoja baada ya kingine lkn kwenye mitandao yetu hilo lipo.

Nenda kwenye menu tu nadhani utakutana na upuuzi wote.

Nini nataka kusema?

Wakati dunia inakimbia kwa kasi kwenye technolojia sisi tunajirudisha nyuma tena kwa kasi kubwa na wala hapa siyalaumu haya makampuni ya simu kwani yenyewe yanapokea tu order toka Serikalini.

Kama wananchi wa kawaida kabisa tunaiomba Serikali iweze badilisha hiv vifurushi haraka sana maana wanachokifanya ni kurudisha juhudi za maendeleo ya kisayansi nyuma.

Na kwa vile tuna Serikali mpya nina hakika watashughulikia hili haraka sana na wala hawatasubiri hadi mwezi upite maana kilichofanyika ni zaidi ya upuuzi wa hali ya juu.

Kama Serikali itashindwa rekebisha hili basi tutajua hamna mpango na wananchi wa kawaida na mengi mnayoyaongea ni porojo tu

Naomba kuwasilisha.

Hii ndio ilikuwa sera ya Magufuli katika akuhakikisha mitandao ya kijamii watu washindwe kuitumia, maana alishasema anatamani malaika washuke wafungie mitandao.
Acha ufala bi dada kwani Magufuli yupo kwasasa mbona unakichwa kama panzi, we lia na Wakina suluhu na waziri husika.
 
Yaani kuwaonjesha tu bei ndio mnalalamika hivi? Bei elekezi kwa mujibu wa Dr. Ndungulile ni Mb 1 @3-5 shs....ndio kwanza tupo kwenye 1Mb @3.3shs tukifika sh 5 mtaweuka kabisa!
Kwahiyo wewe haikuhusu?
 
N
Tunazo taarifa za uhakika kwamba mnanunuliwa bando ili mtukane watu , sasa huo uongo kwamba uliwahi kununua umeutoa wapi ?
Naweza kukuajili hata wewe, mfanyakazi wangu wa kiwango cha juu namlipa milioni moja kwa mwezi na wa chini kabisa laki tatu, sasa wewe najua hata kiwango hicho huna bado upo sebuleni kwa shemeji yako unasubili vitumbua na wapwa zako.
 
Wakuu,

Kama kweli tunaamini katika uhuru wa mawazo kama haki ya kikatiba, na kama kweli tunaamini katika uwajibikaji wa viongozi, basi naomba huyu waziri Ndugulile asome ninayoandika kama jinsi yalivyo.

Wewe waziri Ndugulile, waziri mwenye dhamana kwa niaba ya serikali; una akili timamu!?

Nauliza swali? Unazo zilizotimia?

Hivi, zile mbwembwe zote za kujigamba na kujitutumua kwamba mtahakikisha vifurushi vinakuwa vya bei nafuu, ndio matokeo yake haya tunayoyaona hapa?

Yaani wewe waziri, unaweza kuwafanya watanzania milioni zaidi ya sitini kuwa ni wapumbavu na mbumbumbu?

Ukakimbia kwenda kujitungia kanuni haramu na za kitapeli ili kuhalalisha wizi?

Ulisikia wapi dunia ya leo, data zinakuwa ghali namna hii?

Katika nyakati za utandawazi ambapo maisha yote yanategemea digital devices, kwanini ufanye uhuni wa namna hii?

Sifahamu lengo ni nini? ama ni mbinu za kubinya watu wasipate access ya mtandao?

Ndugulile, nikueleze tu kwamba, maisha ya watanzania wengi hayazunguki kwenye muhimili wa siasa pekee.

Kama lengo ni kuwabinya watu kisiasa, basi hilo ni lengo mfu lisilo na uhalisia.

Mitandao ndio maisha yetu, ndio chakula chetu na kipato chetu. Tusivurugane.

Tunahitaji vifurushi vishuke bei. TAFADHALI.
Mkuu, imetoa ujumbe mfupi, wa wazi bila unafiki, Hawa watu wazidi Sana tupanda vichwani wananchi,huwezi kufanyia wananchi unyama wa namna hii,huu ni unyama ,kukomoana Kama vile hii nchi waliachiwa na baba zao,wao Kama mawaziri hulipiwa kila kitu na mishahara minono itokanayo na jasho zetu kwenye vipato vyetu vya kawaida alafu ndo sie wanatutorture kiasi hiki,
Nawambia hasa mawaziri Kama huyu mnaoendekeza matumbo ,kulamba mfalme viatu ili kulinda vyeo vyenu huku mkiwafanyia unyama watanzania, siku zenu zaja mungu atawaacheni salama mtapata mapigo yasio pungua 47 KWA maisha mafupi hapa duniani na imekua
 
Mkuu admin alitoweka ktk mazingira tatanishi haonekani ko me ndo sonko ila natafuta mtu nimuweke admin then nileft!
hahahaaah kwa vifurushi hivi magroup ya ajabu ajabu ni ya kuachana nayo. Na pia apps zisizo na msingi...
 
Back
Top Bottom