Tanzania na ushoga/food of thought

Oct 5, 2015
88
476
Mh. UMMY MWAIMU NA MARUFUKU YA VILAINISHI
Mh waziri wa afya Bi. Ummy Mwaimu amepiga marufuku ugawaji wa vilainishi kwa mashoga. Ni kwa sababu mradi huo haukuishia tu kwenye kugawa vilainishi lakini pia una viashiria vya kuhamasisha ushoga. Kwahiyo kuendelea kugawa vilainishi kunaweza kupelekea kuongezeka kwa vitendo hivyo visivyoakisi utamaduni, mila na desturi zetu kama watanzania.
Kuna mambo ya kutafakari vilevile; maamuzi ya Mh. Waziri ni ya kuheshimiwa na kuna nia nnjema kabisa ya kuliokoa taifa hili.
Pia ifahamike kuwa vilainishi vinasaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa kwa hao mashoga. Na ieleweke tu kuwa wapo mashoga kwenye ndoa, na wapo wanaoshiriki mapenzi na wanawake pia. Kwa hiyo naona haja ya kufanya kitu cha ziada ili kuepuka majanga ya magonjwa ya zinaa.

Mh. MAKONDA NA MARUFUKU YA MASHOGA
Mkoa wa Dar Es Salaam, ambao Paul Makonda ni mkuu wake, unaongoza kwa idadi ya mashoga zaidi ya 3000 wengi wao wakiwa ni vijana wadogo chini ya miaka 24. Hii ni ishara kwamba utamaduni huu unakuwa kwa kasi na zaidi kwa kizazi kipya. Mh. Makonda alitoa kauli za kupinga vitendo hivi. Ni sawa, katika jamii yetu vushoga haukubaliki na wengi. Lakini kuna haja ya kuangalia namna ya kupinga ushoga, kama ni jambo la kupinga, au kama tunaweza. Kwa sababu kuna unaweza kuyapinga lakini style unayotumia ikawa ya kuhamasisha. Hata hivyo, jambo la kustua ni kuwa, kwa taarifa ‘zisizo rasmi’ mashoga wapo serikalini. Na pengine miongoni mwao wapo waliomfikisha Mh Makonda mahali alipo sasa hivi. Wapo wanaotajwa kushika au kuwahi kushika nafasi kubwa za uongozi; mawaziri, wabunge, viongozi wa taasisi kubwa nk. Ni jambo la kustua, la kufikirisha na pengine la kuacha lijiendee lenyewe.

MATOKEO YA TAFITI (Dr. Mmbaga EJ, Prof. Leshabari MT, et al ); MUHIMBILI UNIVERSITY
Utafiti ulifanyika Dar es Salaam wa watu 150 wanaoshiriki mapenzi ya jinis moja. Matokeao yake kama ifuatavyo; katika jumla ya wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja (men having sex with men/MSN) walihojiwa, zaidi ya nusu (54%) walikuwa wazaliwa wa Dar es Salaam, wakati asilimia 42 walikuwa wakazi wa Dsm waliozaliwa mikoani na asilimia 4.0 walitoka Mombasa.
Umri wa wahojiwa ulianzia miaka 15-40, wakati wengi wao (78%walikuwa na umri wa miaka 24 au pungufu). Asilimia 46 walikuwa wamemaliza elimu ya sekondari au zaidi, huku asilimia 28hawakuwa na elimu rasmi (formal education).

Theluthi mbili (68%) walikuwa peke yao kimahusiano/single wakati asilimia 12 walikuwa katika ndoa (wana wake zao) na asilimia 12.7 walikuwa na mahusiano na wanahume wengi. Asilimia 72 hawakuwa na watoto huku asilimia 15.3 walikuwa na motto mmoja na asilimia 12.7 walikuwa na watoto wawili au zaidi.

Asilimia 54.7 walikuwa na biashara zao ndogondogo, huku 16% walikuwa na ajira rasmi (serikalini au sekta binafsi) na asilimia 8.7 walikuwa wanafunzi lakini asilimia 22.6 walidai kutokuwa na ajira.

Zaidi ya asilimia 16 walikuwa wakatoliki, asilimia 41.3 walikuwa wakristo wa madhehebu mengine huku asilimia 42.7 walikuwa waislamu.

Katika hao, asilimia 60.7 walidai kuwa mapnzi ya jinsia moja kwa baina ya wanaume ndio walionza nayo (anal sex) huku asilimia 32 walidai kuanza kushiriki mapenzi na jinsia tofauti, na asilimia 3.3 walianza mapnezi kwa njia ya mdomo au punyeto (oral sex/ masturbation).

Kuhusu wasiwasi wa maambukuzi ya VVU na magonjwa mengine ya zinaa, asiliimia 20.7 ndio waliodai kuwa na wasiwasi wa kuambikizwa. Matumizi way a kondom wakatia wa kushiriki matendo ya ngono kwa mara ya kwaza yameripotiwa kwa asilimia 14.7 tu.

Mahali palipotumika sana kwa tendo la ngono la kwanza ni numbani, kwa kiwango cha silimia 23.3 au kwenye nyumba ya mwenza (22%). Wengine walitaja kuwa shule za bweni, (19.3)
Kuhusu vichocheo vya kufanya mapenzi ya jinsia moja, asilimia 59.3 walidai kuwa ni starehe, asilimia 20 walidai ni walilazimishwa na asilimia 1.3 walidai waliahidiwa zawadi na watu walioshirikiana nao kwa mara ya kwanza.

Kuhusu kufanywa na kufanyiwa; Asilimia 65.3 hupendelea zaidi kufanyiwa na wenzao, wakati asilimia 18 hupendelea zaidi kuwafanyia wengine na ailimia 16.6 wanapendelea vyote (kufanya na kufanyiwa) kwa kiwango sawa.

Wastani wa wapenzi wa jinsia moja ambao washiriki wa tafiti waliwahi kuwa nao ni kati ya 10-60 katika muda wote wa maisha yao. Huku asilimia 94 walikuwa na wapenzi wawili au zaidi wakati wa kuhojiwa. Hata hivyo asilimia 32.6 waliripoti kuwa na mpenzi wa kike angalau mmoja wakati asilimia 44.8 walidai kuwa na wapenzi wa kike zaidi ya mmoja.

Zaidi ya asilimia 90 ya wahojiwa wanatumia pombe na asilimia 72 kati yao walihusisha pombe na tendo la mapenzi ya jinisa moja walipofanya mara ya mwisho.
Matumizi ya Cocaine na bangi yalikuwa kwa asilimia 37.3.

KWA RAFIKI ALIYENIANDIKIA INBOX
Kuhusu Asili/Nature
Rafiki mmoja ameniandikia kwa lugha ya kiingereza (natafasiri sehemu ndogo ya maandiko yake) kuwa; ‘’mambo ya asili yanaweza kuwa na madhara makubwa na tata kiasi kwamba akili zetu za kawaida zikashindwa kutafsiri na/au kuelewa; tunaweza kuita madhara haya kuwa ni maajabu. Na matokeo yake hasi tunaweza kuyahusisha na laana kwa watenda dhambi......’’
Anaendelea...’’Jambo la msingi ni kuwa mambo ya asili yanajitokea yenyewe kwa namna ya pekee; vimbunga, mafuriko, ukame, njaa, Tsunami, milipuko ya volcano, maradhi ya akili, upumbavu, kukosa nguvu za kiume na ushoga...’’. ‘’Sisi binadamu tunajipa ukuu na kutafsiri asili(nature) kwa kiwango na faida yetu ya maisha ya duniani, lakini mara nyingi elimu ya sayansi na dini zimeshindwa kutafsiri mambo ya asili yanayoshangaza’’. Kwa hiyo usilete utakatifu hapa, kwa kujikita kwenye maelezo kiduchu yasiyotosha kuhusu maumbile na kazi zake, halafu unahitimisha bila kufikiri zaidi’’.

MTAZAMO WANGU. Ni kweli kwamba mambo ya asili yanaweza kuwa na madhara makubwa na kwa hiyo yanahuzunisha. Tsunami na milipuko ya volcano haviepukiki vinapotokea, lakini havipendezi. Lakini yapo yanayoepukika. Binadamu tutashindwa kuibadili asili (nature) lakini hatushindwi kuirekebisha kwa manufaa na ustawi wa sisi binadamu wenyewe.
Ushoga hauwapendezi wasio mashoga, lakini mashoga wenyewe wanafurahia. Hii ni tofauti na majanga ya asili ambayo hayafurahiwi na mtu yeyote mwenye akili timamu (kuondoa wenye maradhi ya akili wanaofurahia kuua watu wengine/ mfano serial killers).

Je! Hatuwezi kuepuka Ushoga? Kama hatuwezi, je hatuwezi pia kuepuka madhara yake? Mbona tunaweza kuepuka madhara ya ukame kwa kutengeneza chakula maabara! Mbona mafuriko yanaweza kuepukika kwa kujenga miundombinu stahiki! Je! Tumetafuta namna ya kuepukana na ushoga kabla ya kuutetea? Bahati mbaya bado kuna mdahalo wa kwamba ushoga ni jambo la asili au la! Lakini angalau tunajua kuwa wapo watoto wadogo waliodanganywa kupewa zawadi ili waingiliwe kinyume na maumbile na baadae kuwa mashoga moja kwa moja, wapo wengine ambao mazingira kama ya shule za bweni yaliwapelekea kufanya mapenzi ya jinsia moja. Je hayo ni mambo ya asili yasiyoepukika?
Nakataa kwamba ushoga ni jambo la asili kwa sababu hakuna ushahidi kutoka kwenye asili yenyewe kwamba wapo binadamu wanazaliwa wakiwa mashoga. Lakini tuna ushahidi kwamba ni matokeo ya matendo ya binadamu baada ya kuzaliwa.

Nakubali kuwa sio sawa kuwatenga, na ni sawa kuwatetea wanapokosewa haki zao kama binadamu lakini sio sawa kuushabikia ushoga. Sio sawa kuushabikia ushoga hasa katika mazingira yetu ya Africa ambapo umasikini ujinga na maradhi vimetamalaki.
Nimewahi kuandika namna mchakato wa kuukubali ushoga ulivyokuwa, awali ushoga ulitambulika kama maradhi ya akili na hivyo kuwa watu wanaohitaji tiba. Baadae ulitolewa kwenye maradhi ya akili na kuwa sehemu ya maisha, hii ilitokea bila tafiti za kisayansi bali kwa mashinikizo ya makundi ya mashoga. Baadae ukatungiwa sheria za kuwalinda. Lakini cha kushangaza unahamasishwa!!! Kwanini kuuhamasisha???. Hapo kuna kitu kimejificha. Ni kitu gani?

KWANINI HATUPASWI KABISA KUUSHABIKIA USHOGA KATIKA JAMII ZETU
1. Familia ndio msingi wa ujenzi wa Taifa lolote (Family is the basic unity of the nation; Civics Form One). Taifa lenye muono wa kujijenga litawekeza kwenye kuboresha familia, ndio maana katika baadhi ya nchi zilizoendelea kiongozi anapimwa kwa namna anavyoongoza familia yake. Kumbe Daktari bora anatoka kwenye familia bora iliyomuandaa, kiongozi bora, mwalimu bora, askari, injinia, mwandishi, mchungaji nk; wataandaliwa vema katika familia na jamii. Tunaweza kuwa na watu wenye taaluma hizo lakini wasiwe katika ubora wao kwa sababu tu jamii nzima imeparanganyika. Sasa ushoga, kwa sababu za kiafya, kimila, kitamaduni unakwenda kuharibu mifumo ya familia zetu, endapo utapigiwa chapuo. Afrika haijawa tayari kuupokea.

2. AFYA; katika mazingira ya maginjwa ya zinaa, hasa UKIMWI vitendo vya ushoga havipaswi kupigiwa chapuo. Ni rahisi maranying zaidi kuambukizwa/kuambukiza maradhi kwa kufanya ngono kwa njia ya haja kubwa.

3. FATHERHOOD/ Rafiki mmoja aliandika ‘Ooh! We have got a royal baby with wrong genitals’. Ni Edner Whatney wa uingereza alipoonesha kusikitishwa na kuzaliwa kwa prince George, mtoto wa kifalme mnamo tar 22/7/2013. Edner anaona kuwa katika nchi yake iliyoruhusu ushoga, kuzaliwa mwanaume ni kuzaliwa na viungo visivyo sahihi. Kwa mtazamo wangu, nikifikiria zaidi kauli ya Edner, naona ushoga unadhalilisha heshima ya baba katika jamii (fatherhood);
 
Kwanini mambo ya ajabu (ushoga) kama haya yanasambaa duniani sasa hv, mwisho wa dunia unakaribia?
 
ⓟⓘⓒⓗⓐ ⓛⓘⓝⓐⓘⓢⓗⓐ ⓜⓔ ⓢⓘ ⓜⓠⓘⓝⓖⓘ
 
Siupendi Ushoga,Ila Kama Mungu wa Biblia Alishindwa Kuumaliza Enzi za Sodoma,Je Sisi Leo Hii Tutaweza?
Mungu hajashindwa na chochote na hatokaa aje kushindwa na chochote.Hawezi shindana na mwanadamu maana siku zake ni 120 tu
 
Back
Top Bottom