Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,777
- 41,071
karibu miaka miwili iliyopita katika kile ambacho kilijulikana kama "Sakata la Mapanki" kati ya vitu ambavyo Rais Kikwete alipinga ni kuhusika kwa Tanzania katika usambazaji wa silaha ndogondogo katika maeneo ya maziwa makuu na hivyo kuchochea vita. Katika hotuba yake ambayo iliungwa mkono baadaye na Bunge la Muungano Rais Kikwete alikataa kabisa kuwa Tanzania haihusiki na mambo hayo.
Ni wakati ule nilipoandika ripoti yangu ya kwanza kuhusu suala la silaha hizi ndogondogo (ripoti hii inapatikana kwenye makasha ya KLH News - Special Reports). Hata hivyo kuna habari mpya ambayo hatimaye inaweza kuwataja tena watu wale wale ambao tumekuwa tukiwasikia tena hasa baada ya mamluki na mfalme wa vita Victor Bout ambaye nilimtaja katika ripoti hiyo kutiwa mbaroni hivi karibuni na hivyo kuwafanya wauza silaha haramu wa eneo letu la maziwa makuu kuwa na matumbo joto.
Je Tanzania imeweza vipi kusimamisha baadhi ya viongozi wake na wananchi wake kujihusisha na udalali wa silaha za moto katika eneo letu la maziwa makuu? Je, hii ni kashfa nyingine ambayo inasubiri kutokea na hivyo kuthibitisha kile ambacho wengine tulikisema miaka miwili iliyopita?