Tanzania na Urusi kuongeza ushirikiano katika sekta ya utamaduni na michezo

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
728
473
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Andrey Levonovich Avetisyan ambapo katika mazungumzo hayo viongozi hao wamekubaliana kuongeza ushirikiano katika Sekta ya Utamaduni na Michezo.

Aidha, viongozi hao wamekubaliana pia kuongeza ushirikiano katika masuala ya Utamaduni wa nchi hizo pamoja na wadau wa Utamaduni na Sanaa kupata mafunzo nchini Urusi katika maeneo ya kutumia vifaa vya Muziki na kutumbuiza jukwaani.

Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekaribisha Mhe. Balozi Avetisyan kushiriki katika Tamasha la Utamaduni la Tanzania litakalofanyika Mwezi Mei, 2023 mkoani Njombe na Tamasha la Utamaduni na Sanaa Bagamoyo litakalofanyika baadae mwaka huu ambapo Mhe. Balozi amekubali mwaliko huu.

Kwa upande wake Balozi Mhe. Avetisyan ameikaribisha Tanzania kushiriki katika Matamasha yanayofanyika nchini humo ambapo ameukaribisha Muziki wa Taarabu ambao ameeleza kuwa umekua ukipendwa na Warusi wanaoishi nchini Tanzania pia nchini Urusi.

IMG-20230329-WA0040.jpg
IMG-20230329-WA0039.jpg
 
Urusi iliwahi kufanya nini duniani zaidi ya vi sera vya kupambana na USHOGA

USSR
 
Sema Urusi kama hawako serious. Ukipita ubalozi wao mandhari ni mbovu. Bendera yao tu ubalozini imepauka na kuchanika chanika. Hebu wawe serious kidogo
 
Back
Top Bottom