Tanzania na Umoja wa Ulaya waazimia kuimarisha uhusiano

Cheko Lamhenga

Senior Member
Aug 1, 2018
165
93
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI

Tanzania na Umoja wa Ulaya (EU) waazimia kuimarisha
Uhusiano

logo.jpg

Tanzania na Umoja wa Ulaya (EU) wamekubaliana kuimarisha
uhusiano na ushirikiano kwa kufanya majadiliano ya mara kwa mara yatakayojengwa
katika misingi ya kuaminiana, usawa, uwazi na kuheshimiana ili kujenga uelewa
wa pamoja katika maeneo mbali mbali yenye changamoto kwa manufaa mapana ya watu wa pande zote mbili.​

Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa mazungumzo
kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt.
Augustine Mahiga (Mb) na Mkurugenzi wa Idara ya Pembe ya Afrika na Afrika
Mashariki, Huduma za Nje katika Umoja wa Ulaya, Bw. Patrick Simonnet wakati wa
ziara yake iliyofanyika nchini kuanzia tarehe 17 hadi 20 Februari 2019.​

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Waziri aliushukuru
Umoja wa Ulaya kwa misaada ambayo umekuwa ukiipatia Tanzania kwa ajili ya
utekelezji wa miradi mbalimbali ya maendelea katika sekta za kilimo, nishati na
ujenzi wa miundombinu ya barabara na viwanja vya ndege. “Umoja wa Ulaya ni mbia
muhimu wa Tanzania katika shuguli za maendeleo tokea mahusiano rasmi ya
kidiplomasia yalipoanzishwa mwaka 1975; baada ya kusainiwa kwa mkataba wa
kwanza wa Rome baina ya kundi la nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki (ACP) na
nchi wanachaama wa Umoja wa Ulaya”; alisema Mhe. Mahiga.​

Viongozi hao walihitimisha mazungumzo yao kwa kuazimia
kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya pande mbili hizi katika maeneo
mbalimbali ikiwa ni pamoja na biashara, uwekezaji, ushirikiano wa maendeleo na
usalama wa majini, hususan katika pwani ya Bahari ya Hindi.​

Aidha, walikubaliana kuimarisha ushirikiano katika
nyanja za kimataiafa ikiwa ni pamoja na kusaidia juhudi za kudumisha na
kuimarisha hali ya amani, usalama na utulivu katika eneo la Maziwa Makuu.​

Imetolewa
na:

Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki,

Dodoma.

21 Februari,2019
 
Hahahahaaaa, just hahahahaaaa! Mabeberu, Mashoga, blah blah blah blah! Haya, Buku 7fc mstari wa mbele, MATAGA fuatieni, Gweregwere mtakuwa mstari wa Mwisho. Maandamano ya kupongeza Serikali ya Dr. JPM kwa Kulamba Ice Cream (Matapishi)!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania na Umoja wa Ulaya (EU) wamekubaliana kuimarisha uhusiano na ushirikiano kwa kufanya majadiliano ya mara kwa mara yatakayojengwa katika misingi ya kuaminiana, usawa, uwazi na kuheshimiana ili kujenga uelewa wa pamoja katika maeneo mbali mbali yenye changamoto kwa manufaa mapana ya watu wa pande zote mbili.

Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) na Mkurugenzi wa Idara ya Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki, Huduma za Nje katika Umoja wa Ulaya, Bw. Patrick Simonnet wakati wa ziara yake iliyofanyika nchini kuanzia tarehe 17 hadi 20 Februari 2019.

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Waziri aliushukuru Umoja wa Ulaya kwa misaada ambayo umekuwa ukiipatia Tanzania kwa ajili ya utekelezji wa miradi mbalimbali ya maendelea katika sekta za kilimo, nishati na ujenzi wa miundombinu ya barabara na viwanja vya ndege.

“Umoja wa Ulaya ni mbia muhimu wa Tanzania katika shuguli za maendeleo tokea mahusiano rasmi ya kidiplomasia yalipoanzishwa mwaka 1975; baada ya kusainiwa kwa mkataba wa kwanza wa Rome baina ya kundi la nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki (ACP) na nchi wanachaama wa Umoja wa Ulaya”; alisema Mhe. Mahiga.

Viongozi hao walihitimisha mazungumzo yao kwa kuazimia kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya pande mbili hizi katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na biashara, uwekezaji, ushirikiano wa maendeleo na usalama wa majini, hususan katika pwani ya Bahari ya Hindi.

Aidha, walikubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja za kimataiafa ikiwa ni pamoja na kusaidia juhudi za kudumisha na kuimarisha hali ya amani, usalama na utulivu katika eneo la Maziwa Makuu.
 
Kajifunze kuandika vizuri uje upost tena
 
Hayo nimazingumzo ya kawaida kwani mahusiano yalikua yamekatwa? sasa hapo mkataba gani wamesaini.....just making headlines

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom