Tanzania na Umoja wa Ulaya waazimia kuimarisha uhusiano

Jambo mhimu zaidi katika haya ni kama huyo anayesababisha mavurugano ya mahusiano na jamii hizi na wananchi wake anajifunza chochote kutokana na matukio haya na kujirekebisha kwenda mbele.

Vinginevyo, mipasho kama hii haina maana yoyote.
 
Aisee. Kwahiyo tunataka kuambiwa kuwa tulikuwa tumetengana nao ndio maana tumekubaliana upya kushirikiana? Ni nani aliyetibua huo ushirikiano uliokuwepo mpaka tunaanza kuingia makubaliano mapya ya kuendelea kuwaomba misaada?

Si Mwanasheria wenu Msomi aliyeko makao makuu ya EU aliwaaminisha kuwa mahusiano ya TZ na EU yameharibika kwenye utawala huu wa JPM
 
Hii wizara wawe wanawekwa wazee tu wenye hekima na uelewa mpana wa kimataifa

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Mahusiano ni ya nchi kwa nchi sio mtu mmoja na nchi.

Ni jambo gumu sana kuacha kushirikiana na nchi na kuamua kushirikiana na mtu.
 
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI

Tanzania na Umoja wa Ulaya (EU) waazimia kuimarisha
Uhusiano

View attachment 1028679
Tanzania na Umoja wa Ulaya (EU) wamekubaliana kuimarisha
uhusiano na ushirikiano kwa kufanya majadiliano ya mara kwa mara yatakayojengwa
katika misingi ya kuaminiana, usawa, uwazi na kuheshimiana ili kujenga uelewa
wa pamoja katika maeneo mbali mbali yenye changamoto kwa manufaa mapana ya watu wa pande zote mbili.​

Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa mazungumzo
kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt.
Augustine Mahiga (Mb) na Mkurugenzi wa Idara ya Pembe ya Afrika na Afrika
Mashariki, Huduma za Nje katika Umoja wa Ulaya, Bw. Patrick Simonnet wakati wa
ziara yake iliyofanyika nchini kuanzia tarehe 17 hadi 20 Februari 2019.​

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Waziri aliushukuru
Umoja wa Ulaya kwa misaada ambayo umekuwa ukiipatia Tanzania kwa ajili ya
utekelezji wa miradi mbalimbali ya maendelea katika sekta za kilimo, nishati na
ujenzi wa miundombinu ya barabara na viwanja vya ndege. “Umoja wa Ulaya ni mbia
muhimu wa Tanzania katika shuguli za maendeleo tokea mahusiano rasmi ya
kidiplomasia yalipoanzishwa mwaka 1975; baada ya kusainiwa kwa mkataba wa
kwanza wa Rome baina ya kundi la nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki (ACP) na
nchi wanachaama wa Umoja wa Ulaya”; alisema Mhe. Mahiga.​

Viongozi hao walihitimisha mazungumzo yao kwa kuazimia
kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya pande mbili hizi katika maeneo
mbalimbali ikiwa ni pamoja na biashara, uwekezaji, ushirikiano wa maendeleo na
usalama wa majini, hususan katika pwani ya Bahari ya Hindi.​

Aidha, walikubaliana kuimarisha ushirikiano katika
nyanja za kimataiafa ikiwa ni pamoja na kusaidia juhudi za kudumisha na
kuimarisha hali ya amani, usalama na utulivu katika eneo la Maziwa Makuu.​

Imetolewa
na:

Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki,

Dodoma.

21 Februari,2019
No any deal!
 
Umoja wa Ulaya ufanye majadiliano na serikali waache kugusia Demokrasia na Haki za Binadamu? Mahiga aache uzuzu wake
 
Back
Top Bottom