Tanzania na Uganda Kushirikiana Kuandaa Mashindano ya AFCON 2027. Rais wa CAF Aunga Mkono

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,586
14,138
Habari zenu wadau wa Michezo..

Inaelezwa kwamba Tanzania na Uganda wanatarajia kushirikiana kuomba kuandaa Mashindano ya AFCON mwaka 2027..

Haijaelezwa nani katoa hilo wazo ila ikumbukwe kwamba Rais Samia aliwahi kugusia kwamba Tanzania inakusudia kuomba kuandaa Mashindano hayo Kwa mwaka 2027.

Rais wa CAF Mutsepe anaonekana kuunga mkono wazo la kuandaa Mashindano hayo Kwa pamoja Kati ya Tanzania na Uganda jambo ambalo linatoa uhakika zaidi dhidi ya Washindani wengine wakiwemo Namibia na Botswana ambao nao wanataka kuomba Kwa kushirikiana..

Binafsi naona sio mbaya japo nilitamani tuandae peke yetu bila kushirikiana na Nchi yeyote.
Screenshot_20220717-182836.png
Screenshot_20220717-183030.png
Nahisi kutokana na mambo ya muda kuwa mfupi na gharama kubwa za miundombinu huenda Serikali imeona itakuwa vigumu kufanikisha kwa mda wa kiaka 5 iliyobaki kujenga viwanja vya kutosha na miundombinu mingine..

Wadau wa soka mnasemaje? 👇
 
Naona kama Wabongo hawana mzuka na haya Mashindano ila ingekuwa ni mambo ya Yanga na Simba pasingekalika.
 
Wabongo hatupendi mpira ila tunazipenda Simba na Yanga tu. Mtu yuko Kakonko halafu Kakonko fc ikicheza na yanga huyo mtu anashabikia yanga.
Uko sahihi mkuu maana Mashindano ambayo hayahusishi Simba na Yanga wanayapuza..

Unfortunately mimi napenda mpira na Sio mshabiki wa hizo timu japo huwa naziangalia zikiwa zinacheza wao Kwa wao na timu za Nje tuu..
 
Back
Top Bottom