Tanzania na TRA wametufikisha hapa. Aibu

Kuna email inasambaa mtandaoni ya kuogopesha. Tunavuliwa nguo uchi.

Hebu soma huu waraka. Wawekezaji wanavyotuchukulia. Kwa mtindo huu, Tanzania inazama
Mimi ni mTanzania naipenda Tanzania Ila umefika mahali sina furaha Kwa haya yanayo endelea kiukweli fuwatilieni Uzi nilisema kama Sera ya awamu ya tano haitobadilika term hii hali itakuwa mbaya zaidi.
 
Huyu Kiwavi ambaye amekuwa copied kama ni M'bong lazima atahangaishwa na Serikali ya Uchumi wa Kati
 
Hamna kitu hapo hizo ni fake emails za kuichafua Tanzania yetu.We need to be tough in collecting revenues.Otherwise we won't make it.
Kwa uongozi usiofuata taratibu ulizojiwekea wenyewe. Tanzania ni chafu kuliko hata uchafu wenyewe.
 
wapiga dili hao..chinesse are not genuine investors at all..ukiona wanalalamika ujue hakuna kupiga dili, whic is good!!
btw...nadhani this is cheap propaganda!!
Si huwa mnasema wazungu Ni mabeberu so mnapendelea wa Asia meaning wachina, wajapan, wakorea, nk.. Kumbe wachina nao wakisema kweli wanakuwa mabeberu?!!!

Alichosema hapo ni kweli tupu, hata wazawa wengi wamefunga biashara awamu hii kwa sabb hizo
 
Ni kweli Mamlaka zinazovizia biashara za Tanzania ni nyingi mno alafu nyingi ya hizo zimejifunza u-TRA, yaan vinatoza fines and penalties kubwa kubwa utadhani vinajua hiyo biashara itatoa hizo pesa kwenye fungu lipi!
TRA Kuweni rafiki, jifunzeni kutotisha watu
kwa fines and penalties. Kumbuka ni kila mwaka na madai yake.


1. Halmashauri- Service Levies
- Lesseni
-Mazingira wenu na fain
-Michango changia
2. TRA -Corporate Tax
- PAYE
-SDL
-VAT
-Property tax
3. Wizara ya na Kodi ya ardhi
4. WCF
5. NSSF

6.OSHA -Hawa Wana list ndefu ya vya kulipia, mafunzo, kupima afya wafanyakazi

7. NEMC, wana list pia, annual fees, na permit fees

8. FIRE Wana list pia ya vitu tofauti vya kulipia, eg, fire extinguishers, certificate, mafunzo!

9. Kama una gari, ongeza fine za barabarani, na issue zote za gari.

10. Wakala wa vipimo, mizani reg fees
and fines.
11. Visima refu, vina zake.
12.BRELA

na bado list inaendelea,
Kama lengo ni kuongeza ukubwa wa tax base, tunakosea, tujaribu kuongeza efficiency kwenye tozo chache,
Yaani kwa Hali ilivyo mamlaka ni nyingi kiasi kwamba kampuni zinalazimika kuongeza gharama za ndani kwa kuajiri mtu atakayekuwa kazi yake ni kuzungukia hizo mamlaka, maana in real business life ni shughuli kubwa hiyo.
 
Basing on our current regime I wont ignore the contents in that letter. TRA, Traffic and all others that is there natural habit, complaints everyday from everywhere.

Sijui ni wawekezaji gani tunaosema kila siku tunawavutia, huyo mchina anadai kapoteza more than 1 mil. US dollar; na sio kwasababu biashara yake ilikuwa ngumu, tatizo ni hao TRA na wenzao na rushwa juu kila siku wanagonga hodi mlangoni kwake.
Tatizo wakati mwingine siyo wao kama TRA ni sheria,Kanuni na mifumo isiyo rafiki inabidi ipitiwe upya kweli kweli kuondoa ukiritimba, kodi za kujirudia, faini na riba kubwa zisizozingatia faida au kulipika, kodi na tozo nyingi mno kwa kila uwekezaji na biashara kwa ujumla, mtizamo hasi ya serikali kwa wafanya biashara na vice versa. Serikali iwachukulie kama washirika wao maendeleo na ustawi wa jamii na vivyo hivyo wafanyabiashara wasiwe na mawazo hasi kwa TRA, ziwepo taratibu rahisi za kupata vibali,mafunzo kwa watumishi wa TRA na wadau/wafanya biashara ya kila mara kwa ujumla badala ya kuviziana,elimu na uhamasishaji wa kila mara na matumizi ya teknolojia katika ukusanyaji wa kodi na tozo, upanuzi wa wigo wa kodi watu wote walipe.wapunguze ukubwa wa sekta isiyo rasmi ilipe kodi badala ya kungangania makampuni na biashara rasmi kuongeza ukusanyaji wa pato. Ongeza idadi ya wafanyakazi TRA na weledi wa kazi na mifumo ya kiutawala ibadilike ikibidi kutoka mamlaka kuwa wakala/ agency. Haya yakifanyika itapunguza pia rushwa.
 
Niandike kiswahili. Huu sio uongo. Kama hatutakua makini then hata hizo kodi tutazikosa. Mtu ameamua kujiajiri anasafirisha Mzigo. Analipa TRA yeye, halmashauri Na bado anailipia Mzigo Ushuru. Wao wamekaa barabarani wanamkamata Dereva Wa Gari atoe risiti ya mzigo alioubeba kupata sh mbili Na kumsaidia mjasiriamali. Dereva hawezi kuitoa maana bosi atagundua. Hapo ujue Dereva akienda tupu hasara tunayo sisi sio dereva wala bosi. Tunaenda kuua biashara. Tutumie hekima. Narudua tena wafanyakazi Wa TRA mnaokaa maofisini hamjui shida za wafanyabiashara kazi kukinga mikono jitafakarini. Mpango ndugu tafakari ni ajira ngapi unaenda kuua kwa hiyo kete. Unaweza ukawa right by the letter of the law lakini ukajikuta unafungisha biashara elfu kumi. We need help not you dragging us down. We have tried at least acknowledge that!!
 
Kodi ya vitanda utalii ongeza hapo. Mwenyekiti wa Taasisi ya wafanya biashara asaidie kwa kuishauri serikali kwa maslahi ya taifa. Uchumi utaanguka.
 
wapiga dili hao..chinesse are not genuine investors at all..ukiona wanalalamika ujue hakuna kupiga dili, whic is good!!
btw...nadhani this is cheap propaganda!!
Inaweza ikawa kweli... laki je..!!
1. Hatuna kodi kabla ya kuanza biashara?
2. Hatuna watu wa OSHA, FIRE etc kwenye registration?
3. Hakuna TRA na makorokocho mengine?

Kuna wakati, tuangalie kilichosemwa..
 
Ni kweli Mamlaka zinazovizia biashara za Tanzania ni nyingi mno alafu nyingi ya hizo zimejifunza u-TRA, yaan vinatoza fines and penalties kubwa kubwa utadhani vinajua hiyo biashara itatoa hizo pesa kwenye fungu lipi!
TRA Kuweni rafiki, jifunzeni kutotisha watu
kwa fines and penalties. Kumbuka ni kila mwaka na madai yake.


1. Halmashauri- Service Levies
- Lesseni
-Mazingira wenu na fain
-Michango changia
2. TRA -Corporate Tax
- PAYE
-SDL
-VAT
-Property tax
3. Wizara ya na Kodi ya ardhi
4. WCF
5. NSSF

6.OSHA -Hawa Wana list ndefu ya vya kulipia, mafunzo, kupima afya wafanyakazi

7. NEMC, wana list pia, annual fees, na permit fees

8. FIRE Wana list pia ya vitu tofauti vya kulipia, eg, fire extinguishers, certificate, mafunzo!

9. Kama una gari, ongeza fine za barabarani, na issue zote za gari.

10. Wakala wa vipimo, mizani reg fees
and fines.
11. Visima refu, vina zake.
12.BRELA

na bado list inaendelea,
Kama lengo ni kuongeza ukubwa wa tax base, tunakosea, tujaribu kuongeza efficiency kwenye tozo chache,
Yaani kwa Hali ilivyo mamlaka ni nyingi kiasi kwamba kampuni zinalazimika kuongeza gharama za ndani kwa kuajiri mtu atakayekuwa kazi yake ni kuzungukia hizo mamlaka, maana in real business life ni shughuli kubwa hiyo.
VAT ungeiondoa kwenye list, kwa sababu inamuhusu mtumiaji wa mwisho. Mfanya biashara ni kama wakala tu wa kukusanya VAT. Ila hayo mengine yaani umegonga penyewe.. Msululu wa malipo hadi inakuwa ngumu sana kuanzanzisha biashara
 
Ndugu zangu hali ni mbaya. Tusichukulie mzaha
Si huwa mnasema wazungu Ni mabeberu so mnapendelea wa Asia meaning wachina, wajapan, wakorea, nk.. Kumbe wachina nao wakisema kweli wanakuwa mabeberu?!!!

Alichosema hapo ni kweli tupu, hata wazawa wengi wamefunga biashara awamu hii kwa sabb hizo
. H
 
Kwa watu ambao tumewahi kufanya shughuli za uwekezaji kwenye mataifa mbalimbali, nikilinganisha baina ya mataifa ambayo nimewahi kuwepo, Tanzania ndiyo eneo la hovyo na gumu kuliko nchi zote.

Nimewahi kushughulika na uwekezaji Australia, Canada, Chile, Argentina, Ghana, South Africa, Mozambique, Mali, Burkina Faso, Liberia na Burundi.

Katika mataifa hayo yote, nikifanya ulinganifu, mahali pabaya kabisa kuwekeza ni Tanzania. Kama ni mfanyabiashara, au mwekezaji, ni aheri uende Burundi kuliko Tanzania.

Tanzania hapafai kwa uwekezaji kwa mazingira yaliyopo. Karibia kila eneo ni tatizo:

1) Kodi ni nyingi na kubwa

2) TRA ni tatizo kubwa. TRA inafanya kazi kama genge la wahuni. Wanaweza kukukadiria kodi ambayo siyo stahili, hata ukilipa hiyo isiyo halali, bado kila wakati watakuwa ofisini kwako kutaka zaidi na zaidi. Wanaweza kukudai risiti hata za miaka 15 iliyopita, kama zinechakaa au zimepotea kwa sababu uliona hazina kazi tena, ujue una shida.

3) Wakuu wa Wilaya, wakuu wa mikoa na mawaziri, wakati wowote wanaweza kuja kwenye kitega uchumi chako na kutoa tamko lolote lile, hata kufunga shughuli zako bila ya kufuata sheria wala masharti ya leseni

4) Rais naye anaweza kutoa tamko lolote kwa kutegemea siku hiyo alivyoamka. Na kwa tamko lake tu ambalo halipo hata kisheria, biashara yako inaweza kuwa imeishia hapo

5) Polisi nayo haieleweki. Matarafiki wa Tanzania ndiyo ovyo kuliko nchi zote nilizowahi kutembelea. Hata uwe mwangalifu namna gani, huwezi kufanya safari ndefu Tanzania, ukafika na kurudi bila kutengenezewa kosa la kulipa. Kuna wakati niliwahi kusafiri toka Lusaka mpaka Ndola mpaka Mbeya. Zambia sikulipishwa kwa kosa lolote. Toka Mbeya mpaka Namanga, Arusha nililipishwa mara 4. Toka Namanga mpaka Nairobi, mpaka Nakuru mpaka Sirari upande wa Kenya, sikulipishwa hata mara moja. Toka Sirari mpaka Mwanza nililipishwa mara 2. Nilienda Burundi nilikaa wiki 2 sikulipishwa kwa kosa la barabarani hata siku 1. Tanzania, ni nchi ya kuviziana, ni nchi ambayo Serikali inafanya kazi ya kuwakomoa wananchi wake, au kuwasomesha namba kwa lazima, wapende wasipende

6) Taasisi msururu ambazo zipo kwaajili ya kukwamisha badala ya kuwezesha. Mara OSHA, TFDA, TBS, WCF, NEMC, FIRE, etc, hao wote wanapokuja kwako lengo kuu ni kuchukua hela

7) TANROADS - hawa wana penalties za ajabu kabisa. Adhabu zinaanzia dola 4,000 kwenda juu. Unapima mzani wa kwanza, wa pili, wa 3, mzigo upo sawa. Mzani wa 4, unaambiwa mzigo umezidi, penalty dola 4,000. Njiani hujaongeza wala kupunguza mzigo lakini mwanzoni mzigo unaambiwa ulikiwa sawa, mwishoni unaambiwa mzigo umezidi.

Kwa ujumla, Tanzania hapafai kwa uwekezaji. Katika Africa, Ghana is the best, na ndiyo maana uchumi wake unakua kwa kasi kitakwimu na jwa macho. Siyo huu wa Tanzania unakua kwenyr makaratasi ya watawala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom