Tanzania na siasa za "hatukukutana barabarani"

mharakati

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,271
391
Ndugu zangu katika kipindi hiki kibovu kiuchumi, kisiasa na kiutawala katika taifa letu napenda tena kumshukuru Mh. Edward Lowassa kwa kurudia ile kauli ya "hatukukutana barabarani" ambayo imetuhakikishia kwa namna moja au nyingine jinsi ya serikali zetu zilivyoendeshwa "kiushikaji" zaidi ya kikanuni na kimaadili.

Serikali ya sasa inashindwa kuchukua hatua zozote za kiutawala kwa viongozi wake, au kufanya maamuzi mazito ya kiuongozi yanayoweza kuleta afueni kwa wananchi katika hali hii ngumu kwa sababu wengi wao "hawakukutana barabarani". Angalia Mkullo , Ghasia, Kawambwa hawa wana mahusiano ya karibu yasiyo ya kazi na Rais na familia yake na wengineo wengi katika baraza hili la mawaziri na wakuu wa mashirika na taasisi za umma ambao hata kama hawana uhusiano wa karibu na Rais bado wanachuma faida ya sera hii isiyo rasmi ya serikali hii na kuendelea kulea uozo katika utawala na hivyo kudhoofisha uongozi wa umma na hatimaye kuliangusha taifa.

Rais anakosa nguvu hadi kwenye chama chake ambapo yeye ni mwenyekiti kwa kuendeleza ushikaji usiokua na maslahi kwa kuogopa kuchukua hatu kwa wale ambao hakukutana nao barabari hadi chama tawala kama mhimili wa utawala wa nchi kimekua dhaifu na kuiambukizia serikali siasa chafu na udhaifu huu huku ukiathiri utendaji kazi na maisha ya wananchi kwa ujumla.

serikali zote zilizopita zilikua zinalindana lakini kidogo kero zilikua chache, sasa kero ziko nje nje na bado "ushikaji" umetawala kwa nguvu zote. Kweli huu ni utawala wa watu waliokutana kando ya barabara
 
Back
Top Bottom