Tanzania na Serikali ya China kusaini MoU hivi karibuni kudhibiti bidhaa feki toka China

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
bidhaa-china.jpg


Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji iko kwenye mazungumzo na serikali ya China ili kupata njia bora ya kuzuia bidhaa bandia na hafifu kutoka huko kuingizwa soko la Tanzania.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Adelhelm Meru, aliyasema hayo wiki hii katika mahojiano maalum kuhusu utekelezaji wa sera, mipango na usimamizi wa sheria unaofanywa na Serikali ya Tanzania kuelekea kuwa nchi ya viwanda.

"Tanzania tunafanya mazungumzo na China ili kufanikisha makubaliano kati ya TBS (Shirika la Viwango Tanzania) na Shirika la Ukaguzi la China ili wasaidie kwenye ukaguzi wa bidhaa za China kabla hazijapakiwa kwenye meli kusafirishwa kuja Tanzania.

Kwa sasa tunashirikiana na kampuni mbili za ukaguzi za SGS na Bureau Veritas ambazo zipo duniani kote," alisema Dk. Meru.

Dk. Meru alisema mazungumzo yamefikia hatua nzuri na kwa sasa mkataba wa makubaliano (MoU) unafanyiwa kazi, ukikamilika utasainiwa na lengo ni utekelezaji wake kuanza kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Alisema kuwa katika makubaliano hayo Tanzania itatoa viwango vya ubora (specification) inayotaka kwa kila bidhaa, na kuhakikisha bidhaa zinazoingia ni ambazo ubora wake umeshakubalika, utaratibu ambao unatumiwa pia na nchi za Ulaya na Marekani.

"Kwa kuwa bidhaa nyingi zinazoingia nchini mwetu kwa sasa zinatoka China, chini ya makubaliano hayo ni lazima zikaguliwe kulekule kabla ya kupakiwa kwenye meli kuja nchini," alisema.

Dk. Meru aliendelea kueleza kuwa kampuni hizo ni kubwa, lakini kuna baadhi ya nchi ukaguzi unachukua muda mrefu kwa kushindwa kuwafikia wadau wote kwa haraka kutokana na kampuni kuwa kwenye mji mmoja.

"Tunalenga kupanua zaidi ili TBS waweze kushirikiana na taasisi nyingine za udhibiti wa ubora, bidhaa zote zikaguliwe kabla hazijaingia nchini," alisema Dk. Meru.

Aliongeza kuwa kinachofanywa kwa sasa ni ukaguzi kwenye masoko na kukamata bidhaa bandia na hafifu. Alisema TBS inaongezewa nguvu ili kuyafikia maeneo mengi nchini na kutumia vifaa vya kisasa.

Alisema anatambua uwapo wa bidhaa hizo katika soko la Tanzania na mipango inaandaliwa kukamata na kuchukua hatua madhubuti kwa waingizaji ikiwamo kuziba mianya ya uingizaji bidhaa hizo.

"Unapokuwa na uwezo wa kukagua bidhaa za nje kwa mfumo wa kompyuta, inarahisisha kazi kwa kuwa tangu mzigo unapakiwa inajulikana na unapofika inakuwa suala la ukaguzi wa kujiridhisha zaidi," alisema.

Dk. Meru aliendelea kueleza kuwa ukaguzi unapofanyika kwa ushirikiano kuanzia mzigo unapotokea, unasaidia kupunguza uzito wa kazi na kuchelewesha mizigo bandarini.

Source: Nipashe
 
itakuwa vizuri hilo likifanikishwa maana tumekuwa jalala la bidhaa mbovu,hafifu na zisizokuwa na viwango.China inatengeneza vitu vingi vyenye ubora na hata Marekani wanavinununa,ila kwa hapa kwetu wa kulaumiwa ni wafanyabiashara wanaotuletea hizo bidhaa kwa kujali zaidi faida bila kuzingatia ubora wala kuwajali watumiaji.
pia inatakiwa ufuatiliaji wa viwanda bubu vya wachina humu nchini vinavyotengeneza vitu feki ili kufanikisha lengo hilo.
 
"Tanzania tunafanya mazungumzo na China ili kufanikisha makubaliano kati ya TBS (Shirika la Viwango Tanzania) na Shirika la Ukaguzi la China ili wasaidie kwenye ukaguzi wa bidhaa za China kabla hazijapakiwa kwenye meli kusafirishwa kuja Tanzania.
Watu watapakia mzigo kuelekea Dubai na kisha watapakia kwenye majahazi kutoka Dubai kuja Afrika Mashariki! Kwahiyo, wasidhani wakifanya hivyo tu watakuwa wametatua tatizo... wanatakiwa kwenda maili moja zaidi!
 
Kama China ni waungwana walipe fidia waliyosababisha kwa watanzania, wengi wameunguliwa nyumba na mali zao kwa sababu ya appliances fake
 
Back
Top Bottom