Mtego wa Noti
JF-Expert Member
- Nov 27, 2010
- 2,591
- 1,599
Kwa sasa Kenya na dunia nzima wanaomboleza kifo cha mwanaharakati na mshindi wa zawadi ya Nobeli, Professa Wangari Maathai. Huyu mama alikuwa ni mwanaharakati na mwanamazingira mahiri sana. Hapa Tanzania nilishawahi kusikia kuwa tuna mtu aliyeshinda zawadi ya nobeli miaka mitatu iliyopita, naye ni Professa Pius Yanda wa chuo kikuu cha Dar es salaam, Idara ya utathmini raslimali(IRA). Je ni kwa nini sijasikia serikali hii ikijivunia uwepo wa mtu huyu? Au ndio ule usemi wa kuwa sifa na umaarufu wa mtu unaonekana akiwa hayuko hai tena?
Je, serikali imechukua hatua gani kumtangaza huyu mtu ambaye aliweza kuiweka nchi yetu katika ramani ya dunia na kuiongezea sifa nchi yetu?
Je, serikali imechukua hatua gani kumtangaza huyu mtu ambaye aliweza kuiweka nchi yetu katika ramani ya dunia na kuiongezea sifa nchi yetu?