Tanzania na Noble prize winners, tunamjua Prof Yanda?

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
2,591
1,599
Kwa sasa Kenya na dunia nzima wanaomboleza kifo cha mwanaharakati na mshindi wa zawadi ya Nobeli, Professa Wangari Maathai. Huyu mama alikuwa ni mwanaharakati na mwanamazingira mahiri sana. Hapa Tanzania nilishawahi kusikia kuwa tuna mtu aliyeshinda zawadi ya nobeli miaka mitatu iliyopita, naye ni Professa Pius Yanda wa chuo kikuu cha Dar es salaam, Idara ya utathmini raslimali(IRA). Je ni kwa nini sijasikia serikali hii ikijivunia uwepo wa mtu huyu? Au ndio ule usemi wa kuwa sifa na umaarufu wa mtu unaonekana akiwa hayuko hai tena?
Je, serikali imechukua hatua gani kumtangaza huyu mtu ambaye aliweza kuiweka nchi yetu katika ramani ya dunia na kuiongezea sifa nchi yetu?
 
  • Thanks
Reactions: ffn
Au sisi tunajivunia hizo awards anazopata JK akienda huko nje kwa wanaonunua nchi yetu?
 
Kwa sasa Kenya na dunia nzima wanaomboleza kifo cha mwanaharakati na mshindi wa zawadi ya Nobeli, Professa Wangari Maathai. Huyu mama alikuwa ni mwanaharakati na mwanamazingira mahiri sana. Hapa Tanzania nilishawahi kusikia kuwa tuna mtu aliyeshinda zawadi ya nobeli miaka mitatu iliyopita, naye ni Proffesa Pius Yanda wa chuo kikuu cha Dar es salaam, Idara ya utathmini raslimali(IRA). Je ni kwa nini sijasikia serikali hii ikijivunia uwepo wa mtu huyu? Au ndio ule usemi wa kuwa sifa na umaarufu wa mtu unaonekana akiwa hayuko hai tena?
Je, serikali imechukua hatua gani kumtangaza huyu mtu ambaye aliweza kuiweka nchi yetu katika ramani ya dunia na kuiongezea sifa nchi yetu?

Mimi ndiyo kwanza naona leo kama kuna mtanzania amewahi kupata tuzo/nishani ya Nobel.
 
Kama Prof Yanda yuko smart inabidi ajipromoti mwenyewe badala ya kuwangojea hao "jamaa"!
 
Mimi ndiyo kwanza naona leo kama kuna mtanzania amewahi kupata tuzo/nishani ya Nobel.
Huyo ndio mimi namfahamu, inaweza kuwa kuna wengine walishapata lakini kwa utamaduni wetu hasa wa serikali yetu kujai zaidi wanasiasa badala ya wataalamu ndio maana huwezi kuwafahamu watu wa namna hii.
Ingelikuwa labda JK ndiye alipewa hiyo zawadi ya nobeli, ungelazimishwa ufahamu....ndio maana kila akipata ka-zawadi hata kama ni kwa wanaotaka kununua nchi waandishi wanampamba mno.
Tujivunie kuwa na watu kama Prof Yanda............
 
hivi inatakiwa mwenyewe ndio ajitangaze? hii is not a politician by the way...
 
Kwa sasa Kenya na dunia nzima wanaomboleza kifo cha mwanaharakati na mshindi wa zawadi ya Nobeli, Professa Wangari Maathai. Huyu mama alikuwa ni mwanaharakati na mwanamazingira mahiri sana. Hapa Tanzania nilishawahi kusikia kuwa tuna mtu aliyeshinda zawadi ya nobeli miaka mitatu iliyopita, naye ni Proffesa Pius Yanda wa chuo kikuu cha Dar es salaam, Idara ya utathmini raslimali(IRA). Je ni kwa nini sijasikia serikali hii ikijivunia uwepo wa mtu huyu? Au ndio ule usemi wa kuwa sifa na umaarufu wa mtu unaonekana akiwa hayuko hai tena?
Je, serikali imechukua hatua gani kumtangaza huyu mtu ambaye aliweza kuiweka nchi yetu katika ramani ya dunia na kuiongezea sifa nchi yetu?

Kwanza andika neno Nobel Prize kwa usahihi
Pili sijui kama unaelewa vizuri maana ya Nobel Prize
Tatu ni kwamba hakuna mtanzania aliyewahi kupata Nobel Prize walau hata ya amani ambayo ndiyo waafrika wachache wamewahi kupata kama Prof. Wangari Mathai, Nelson Mandela na Desmond Tutu
Nchi inayoongoza kwa watu wake kupata Nobel Prize ni United States of America (zaidi ya 300) ikifuatiwa na Uingereza na Ujerumani.
Katika nchi hizi kuna Nobel Prizes nyingi za sayansi kuonyesha wapo mbali katika utafiti na ugunduzi.
Nne uwe unasoma vitu kwanza kabla hujaanzisha mjadala. Kuna knowledge nyingi iliyoufunguliwa kwenye internet lakini watu wetu bado ni vihiyo sana na hawajui namna ya kuona hiyo knowledge.
 
asante kwa kunisahihisha....
la fuata hiyo link uone kama TZhatujawahi kuwa na winner kweli!
Swahili Time: Prof. Pius Yanda wa UDSM apata Nobel Prize

Halafu picha ya mtu mwenyewe ni hii hapa....
Prof.+Pius+Yanda.jpg
 
  • Thanks
Reactions: ffn
Ni kweli mkuu huyu jamaa alistahili kupongezwa kwa kutuwakilisha vema. nadhani pengine hakupata uzito sana kutokana na kuwa Tuzo hiyo ilishindwa na group ya watu, na aliyewaongoza katika kuipata, ni Al Gore.
 
Mdawa sijakuelewa...kwa hiyo una maana hiyo aliyopata haikuwa nobel prize? ofauti ni kuwa ilikuwa ni pamoja na wengine ambao ni kama Al gore! au unataka kutuaminisha kuwa hajapata nobel prize? nina wasiwasi na wewe....
Sasa wewe unazidi kupotosha watu kwa sababu hujasoma hata comments kwenye hiyo article uliyofanya reference.
Nimesoma comments na zinaonyesha habari hiyo ni uzushi tu wa kiswahili.
 
sasa which is which huyu Prof. Yanda si alipata? hata kama alipata ndani ya group lenye watu wengine bottom line ni alipata and it should be recognized ila tu ndo hivo tanzania hatuna utamaduni wa kiujivunia vya kwetu labda akishatuacha (Mungu pitisha mbali) ndo tutajivunia.............shame
 
Nimepeda comment yako. tatizo la tanzania ni kuwa hatupendi kuwatambua na kuwasifu wataalamu tulionao. tunapenda na tumezoea kusifia wanasiasa ambao hakuna wanalolifanya zaidi ya kufuja rasilimali zetu tu.
Huyu mtu alistahili publicity ya nguvu ili watu wafahamu hadhina waliyo nayo.
sasa which is which huyu Prof. Yanda si alipata? hata kama alipata ndani ya group lenye watu wengine bottom line ni alipata and it should be recognized ila tu ndo hivo tanzania hatuna utamaduni wa kiujivunia vya kwetu labda akishatuacha (Mungu pitisha mbali) ndo tutajivunia.............shame
 
Jmn watanzania tuache ubishi wa kipumbavu na tabia ya kupenda kujifanya tunajua wkt hatujui.

Nimeona humu ndani watu wengi wanabisha kwamba huyu jamaa hajapata nobel,well hii nobel alipata ila tuseme alipata kma tume ya mazingira nazan,ilikua group ya watu wakapata iyo tuzo.

Me nilikua mwanafunzi udsm wkt anapewa hii tuzo na pia chuo kilimpongeza kwa kutoa taarifa pale utawala notice board.

Ttz letu hatupendani mtu ukisikia mtanzania kashinda kitu flan nje badala ya kusikia faraja na kufurahi we ndo unakandia! Kwa tabia hii hata tupate katiba mpya na chadema iingie madarakan hatutaendelea kwa maana cc wenyewe hatupendani
 
Back
Top Bottom