Tanzania na Misri zaridhia ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuchakata nyama nchini

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Tanzania na Misri zimeweka historia nyingine ya ushirikiano baada ya kutia saini hati ya makubaliano ya ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuchakata nyama na mazao mengine ya mifugo kinachotarajiwa kutoa ajira kwa takribani watu 5,000.

Imeelezwa kuwa kiwanda hicho kitakajengwa kwa ubia baina ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (Narco) ya Tanzania na Kampuni ya Necai ya Misri na baada ya ujenzi wake kukamilika, kitazalisha nyama na bidhaa za ngozi kama viatu, mikanda, mabegi na chakula cha mifugo.

Kiwanda hicho kitakachoitwa Ruvu Integrated Industry kikiwa na uwezo wa kuchinja ng'ombe 1,500 na mbuzi 4,500 kwa siku, kitajengwa katika Ranchi ya Ruvu wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini wa hati ya makubaliano hayo baina ya nchi hizo jijini Dar es Salaam juzi, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, alisema ujio wa kiwanda hicho ni faraja kubwa kwa wafugaji hasa katika kipindi hiki ambacho hawana masoko ya uhakika ya mifugo yao.

Waziri Mpina alisema ujenzi wa kiwanda hicho pia kunapeleka salamu njema kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Jumuiya ya Maendeleo Mashariki mwa Afrika (IGAD) na mataifa mengine ambayo yanategemea mazao ya mifugo kutoka Tanzania.

Alisema asilimia 1.4 ya mifugo yote duniani iko Tanzania na asilimia 11 ya mifugo yote Afrika iko Tanzania, hivyo kuna uhakika wa viwanda hivyo vinavyoanzishwa sasa kupata malighafi ya kutosha muda wote.

Aliihakikishia Misri kuwa Serikali ya Tanzania inaendelea kufanya mageuzi makubwa katika uzalishaji wa mifugo pamoja na huduma za mifugo ili kuhakikisha malighafi hiyo ya viwanda inakuwa bora na inapatikana wakati wote.

Waziri Mpina aliagiza timu ya wataalamu kutoka Tanzania na Misri kukamilisha haraka upembuzi yakinifu wa mradi huo ili ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa, mkataba rasmi wa ubia wa ujenzi na uendeshaji wa kiwanda hicho uwe umesainiwa.

Pia aliwaagiza watendaji wote wa serikali wanaoshiriki katika majadiliano hayo kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha mkataba huo kutiwa saini.

Watendaji wanaohusika ni wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Viwanda na Biashara, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na taasisi nyingine zitakazohusika na mchakato wa upembuzi yakinifu.

Mbali na hilo, Waziri Mpina pia aliiomba Serikali ya Misri kuendelea kuwekeza katika maeneo mengine ya mifugo na uvuvi kwa kuwa fursa bado ni nyingi hasa katika uendeshaji wa Shirika la Uvuvi Tanzania (Tafico) ambalo serikali tayari imeshalifufua.

Waziri huyo alisema fursa za uvuvi wa ukanda wa uchumi wa Bahari Kuu (EEZ) ni kubwa kwa Tanzania kwa kuwa ina eneo la kilomita za mraba 223,000, ukanda huo ukiwa unafaa kwa uvuvi wa samaki aina ya jodari na wengine ambao ni wa daraja la kwanza duniani.

Aliiomba Misri kuwekeza katika viwanda vya kuchakata samaki wa bahari na maji baridi, ufugaji wa samaki pamoja na kununua meli kubwa za uvuvi zitazovua katika maji ya ukanda wa uchumi wa bahari kuu.

Balozi wa Misri, Mohamed Gaber Abulwafa, alisema hatua ya utiaji saini hati ya makubaliano hayo ni kielelezo cha ushirikiano uliodumu kwa zaidi ya miaka 50 baina ya Misri na Tanzania katika kuchochea uchumi wa mataifa hayo mawili.

Alisema Misri imevutika kuwekeza kwenye sekta hiyo ya mifugo baada ya kubaini Tanzania inayo mifugo mingi na bora na ujio wa mradi huo ni matokeo ya mazungumzo ya awali baina ya Rais John Magufuli na Rais wa Misri, Abdel Fattah El-Sisi, alipotembelea nchini mwaka 2017.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii habari ingekuwa 'serikali YAFUNGA kiwanda cha Wamisri kwa kukiuka mkataba, sasa hivi kungekuwa na kurasa 100. Ila kwasababu ni habari njema watu wanapita kimya.
ajira 5000 tu nacho ni kiwanda??????watu wanazungumzia viwanda vyenye ajira 50000 mpaka laki huko wewe unasema hicho kijimashine cha nyama??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari nyingine njema kwa raia wa Tanzania.Hongera serikali ya awamu ya tano.
 
Safi sana,sasa nitapanua mradi wangu
wa kufuga kiti moto. hili ni soko la uhakika.
 
hao wafanyakazi 5000 watakuwa wanafanya kazi gani umo kiwandani??? maana nnavojua mimi toka uchinjaji,uchunaji mpaka kukata kata hao Ngombe na Mbuzi siku hizi ni mashine tu ndo zinatumika,na pia je ni kweli tuna hao ngombe 1500 wa kulisha hicho kiwanda daily??? 1500x362=
 
1060110


SERIKALI ya Tanzania ina mpango wa kujenga kiwanda kikubwa cha kuchakata nyama na kuongeza thamani katika ngozi, chenye uwezo wa kuchinja ng’ombe 1,500 kwa siku sambamba na mbuzi na kondoo 4,500.

Kiwanda hicho kitajengwa mkoani Pwani ikiwa ni ushirikiano kati ya serikali za Tanzania na Misri, ambapo Kampuni ya Ranchi za Taifa (Narco) na Kampuni ya Uwekezaji ya Misri (Necai) ndio waratibu.

Tayari makubaliano ya awali ya ujenzi huo, ikiwemo upembuzi yakinifu yamesainiwa, lengo likiwa ni kuzikia fursa mbalimbali zilizopo katika bidhaa za mifugo ndani na nje ya nchi .

Mkurugenzi Mtendaji wa Narco, Profesa Philemon Wambura kwa pamoja na Osa wa Bodi ya Kampuni ya Necai, Jenerali Ahmed Hassan waliweka saini makubaliano hayo mwishoni mwa wiki Dar es Salaam, wakishuhudiwa na Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina na Balozi wa Misri nchini, Mohammed Gaber Aboul.

Awali akizungumza, Mpina alisema ujenzi wa kiwanda hicho unaweka rekodi kwa nchi hizo ikiwa ni jitihada zilizoanzishwa na Rais John Magufuli baada ya kukutana na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi, Agosti mwaka 2017, na kuweka mikakati ya ujenzi huo ambapo hatua za awali zimeanza.

Waziri Mpina alisema matumaini yake kuwa uwekezaji huo utakuwa wenye manufaa kwa kuwa asilimia 1.4 ya mifugo yote ifugwayo ipo nchini na asilimia 11 ya mifugo ya Afrika inapatikana Tanzania. “Tanzania ina mikataba mbalimbali ikiwemo ya uhifadhi na utunzaji wa mifugo, huku wizara ikiwa bega kwa bega na wafugaji ili kuzalisha mifugo bora na kuwa na nyama shindani pamoja na kuwa na mbari bora za mifugo,” alisema Mpina.

Kuhusu kiwanda alisema ni mradi wenye kuishangaza dunia ambapo nchi zote zipo tayari kwa ajilibya kutekeleza ujenzi huo,ambapo baada ya miezi mitatu tangu kusainiwa kwa upembuzi yakinifu hatua nyingine za ujenzi zitaendelea, na Tanzania imeahidi kugoa ushirikiano katika hilo.Alisema Tanzania inategemewa na nchi nyingi za Afrika kwa kuuziwa mifugo na hata nyama ikiwemo nchi za Nigeria na Ghana zikiwa zinategemea sana ngozi.

“Kupitia ujenzi huo, utasaidia kuendelea kukuza uchumi na kutakuwa na solo kubwa nchini Misri, Afrika na dunia kwa ujumla,” alisema Mpina huku akibainisha kuwepo pia fursa mbalimbali katika eneo la uvuvi wa samaki. Akizungumza, Balozi wa Misri nchini, Aboul alisema ushirikiano wa dhati baina ya nchi hizo umewezesha kukia hatua hiyo ya ujenzi wa kiwanda hicho na kutoa manufaa kwa nchi hizo.

Alisema makubaliano yaliyokiwa ni matokeo ya ujumbe wa Misri pamoja na Rais wa nchi hizo walipokutana na Rais Magufuli na wananchi wataanza kuvuna mazao ya mifugo, kukuza uchumi na hats kufanya biashara.

Naibu Waziri Abdallah Ulega alisema mradi pia utajikita kunenepesha wanyama walio hai, kuchakata nyama na kuiongeza thamani na kuongeza thamani kwa ngozi na bidhaa zake. “Ujenzi utaleta mapinduzi makubwa sekta ya mifugo, ambapo ng’ombe ataingia kiwandani akiwa hai, lakini akitolewa nyama ambayo nitaweza kuuzwa nchini na nje ya nchi na ngozi ikiwa imeongezewa thamani,” alisema. Alisema kwa kuwa mkoa wa Pwani una mifugo mingi iliyohamia, itakuwa fursa kwa kuinua uchumi wa eneo hilo.
 
Naomba niulize swali misri ina uchumi wa kati tunaoutaka sisi au inauchumi wa juu?
 
Sasa mkuu kwa akili yako kubwa unadhani hawa jamaa wanafanya hivyo ili watunufaishe tufikie uchumi kama wao tujiweze wao wakose pesa?

Kwa sababu tukishajiweza hawatapata tena hizo tenda wanazozipata kiholela
 
Back
Top Bottom