Tanzania na mipango miji yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania na mipango miji yetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The hammer, Feb 10, 2012.

 1. The hammer

  The hammer JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 1,236
  Trophy Points: 280
  Tanzania ni moja ya nchi maskini sana duniani japo umaskini wetu ni wa kipato tu na si RASILIMALI.Moja ya vitu ambavyo ni viashiria vya umaskini wetu ni mipango miji yetu ilivyo kwa mjini na hata vijijini. KWA MIJI ILIYOPANGWA VYEMA,KUNA MAMBO MENGI YENYE FAIDA NIKITAJA FAIDA CHACHE MOJAWAOPO NI KUEPUKANA NA MSONGAMANO WA MAGARI,HUSUSANI KWA MIJI INAYOKUWA KWA KASI HAPA TZ. PIA KUEPUKANA NA MAGONJWA MBALIMBALI KAMA MALARIA NA MENGINE YA MLIPUKO................Na faida nyingine nyingi ambazo zingetuondolea adha nyingi.... But sijajua nini kwanini serikali haijaweka kipaumbele katika makazi yaliyopimwa,na kuhakikisha nyumba hazijengwi iwe mjini au vijijini bila maeneo husika kupimwa kama kilivyopimwa Masaki na kwingineko na MTU ANAYEJARIBU KTK ENEO LISILOPIMWA HUCHUKULIWA HATUA HATA KABLA UJENZI HAUJAFIKA MBALI HII INGEONDOA TATIZO KABISA WAKATI HUOHUO VIWANJA VILIVYOPIMWA VINAKUWA VINGI HATA KULIKO MAHITAJI KULIKO HIVI SASA VIWANJA VILIVYOPIMWA HUSIKIKA USIKU WA MANANE KUKISHAKUCHA WENYE FEDHA WAMESHAVIMILKI. WANA JF NINI TATIZO KWA SERIKALI YETU KUFANYA HIVI,KWANI FAIDA NI NYINGI SANA....Nawasilisha
   
 2. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Tanzania ilipotea jumla pale ambapo utawala na mfumo wa sheria ulipigwa teke. Hali hii naamini ilitokana na ufukara uliosababishwa na siasa za Nyerere za ujamaa na kujitegemea, siasa ambazo in the long run hazileti nguvu ya kiuchumi ndiyo maana hata Wachina waligundua hilo.
  Baada ya watu kuzinduka usingizini na kujikuta hawana kitu, hapo ndipo kila mmoja, serikali ikiwemo, akaanza kutafuta mbinu ya ku-survive na ndipo sheria zilipoanza kupindishwa na rushwa ikawa mtawala wetu.
   
 3. morenja

  morenja JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,534
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  miji holela ni mfano halisi jinsi uongozi wa nchi usivyo kuwa na mipango,na sawa na baba na mama walionzia kwenye chumba kimoja cha kupanga .wakazaa watoto sita .wamekua wakubwa .na bado wako chumba kimoja,uongozi tanzania hii .hakuna future plans si kwenye upangaji miji tuu .ni sekta zote za maendeleo ,mfano mipango ya umeme ,bomba la kusafirishia gesi,na sidhani kama kutatokea mabadiliko kama ccm .wataendelea kuwepo madarakani ..sijui
   
 4. The hammer

  The hammer JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2013
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 1,236
  Trophy Points: 280
  Mh Anna Tibaijuka, ni lini utasimamia na kuhakikisha viwanja vya ujenzi wa nyumba unakuwa umepimwa tayari na kusubiri wateja na si wateja kusubiri viwanja vilivyopimwa bila mafanikio...

  Na nini hatma ya nyumba zilizojengwa bila mpangilio??

  Lini serikali itakomesha ulanguzi wa viwanja vya ujenzi wa nyumba?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. K

  Kikwajuni One JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2016
  Joined: Mar 18, 2013
  Messages: 8,175
  Likes Received: 1,555
  Trophy Points: 280
  Viwanja ni Tatizo sana katika majiji makubwa na miji mbali mbali.Majiji kama Dar,Tanga,Mbeya,Arusha nk.Kupata viwanja vilivyopimwa kwa kusubiri wanunuzi,ni bahati sana.Ndio maana wengi wanaishiwa kuuziwa viwanja vya watu,vyenye migogoro,na kuingia hasara kubwa.
  Twashukuru serekali yetu sana,tena sana kwa kutuelimisha wananchi kuhusu kununua Viwanja,visivyo na migogoro.Wengi wananchi,sasa tumeanza kuelewa njia sahihi za kupata viwanja.
   
 6. The hammer

  The hammer JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2016
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 1,236
  Trophy Points: 280
  Ila kiuhalisia ongebidi kuwepo na makampuni ya kupima viwanja na watu waende huko kinunua kwa hayo makampuni.Maana ni lini nchi itakuwa na mipango miji mizuri kama haya yataachwa kuendelea.Lazima kuwepo na uthubutu wa mipango miji na si kila mtu ajenge kila mahali tu.
   
Loading...