Tanzania na mfumo wa digitali tunaoutarajia utakidhi haja? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania na mfumo wa digitali tunaoutarajia utakidhi haja?

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by KIBURUDISHO, Sep 1, 2011.

 1. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 953
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  WanaJF wenzangu pia watanzania wenzangu nimekaa nimefikiria sana hadi nikaona nililete hili mbele yenu ili tulijadili kwa pamoja maana naami palipo wengi hapaharibiki jambo.

  Hivi mfumo huu wa digitali tunaoutarajia utakidhi haja ya kila mtanzania kwa atakayekuwa tayari kumiliki tv bila kujali wapi anakoishi pia umbali gani toka ilipo transimita ya kurushia matangazo?

  Naingiwa na wasiwasi juu ya mfumo huu kutokana na hii ya sasa yenyewe baadhi ya maeneo fulani hapa mjini matangazo hayo kwa njia ya (vingamuzi) yanasumbua.

  Nikauliza kwa nini tusitumie mfumo wa satelite wenye uhakika zaidi na wenye uwezo wa kumfikia yeyote popote pale bila kujali yuko mabonde kuinama au mlimani. Nilijibiwa kuwa kurusha matangazo kwa njia ya satelite ni gharama sana tofauti na kurusha matangazo kwa njia ya minara (transimita).

  Sasa tutaogopa gharama ya kurusha matangazo kwa njia ya satelite tukimbilie huko kwa bei nafuu abako hatutakuwa na uhakika wakuwafikia wananchi wote popote pale walipo ndani ya Tanzania.

  Ombi langu kwa serikali hebu liangalieni hili kwa makini na kwa undani.
   
 2. yangoma

  yangoma Member

  #2
  Sep 2, 2011
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimelipata nitalifanyia kazi subiri nipumzike maana.
   
 3. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Hizo ni ahadi tu kama za wanasiasa, uwezo wa kuingia digital hatuna inahitaji garama kubwa ikiwemo kutumia fibres, i mean kila mtu awekewe cable na humo humo iunganishwe na simu,internet na tv,kama nchi za wenzetu cable provider ndio huyo anatoa kila kitu Tanzania tutaweza?

  Kwa ulaya ipo kampuni ya CANAL DIGITAL inayotoa huduma kama hizo, dstv wenyewe bado wanatumia sattelite kurusha matangazo yake,not easy kwa sasa bado tutaendelea kutumia analogue terrestial broadcasting.

  Wataalamu wa mambo haya watatueleza zaidi huo ndio ufahamu wangu.
   
 4. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 953
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Mara ya kwanza nilivyokwenda likizo nyumbani huko mkoani nilikuta pale halmashauri ya wilaya wanatumia internet ya fibre optic haikuwa na nguvu kabisa.Juzi nilikuwa huko nilikuta pale halmashauri wametupa mbali vile viantena vya internet vya fiber wamefunga mtambo wa ukweli wa VSAT DISH wa internet unapiga kazi bila shida yoyote.Sasa hawa wataalamu wetu ni wapi wanapotupeleka.
  NIONAVYO MIMI:Kwanini serikali isingetuhamisha kutoka band ya C-BAND ya kutumia zile ungo kubwa na kutupeleka kwenye band ya KU-BAND yenye vile vinyungo vidogo.Tena tukawa kwenye degree 36 ilipo Dstv,Uwe DSTV,au TING au STARTIMES wote wawe wanatumia satelite moja ili mtumiaji uwe na ungo mmoja tu kama utahitaji zote kati ya hizo utakuwa unabadilisha tu LNB kulingana na idadi ya vingamuzi ulivyonavyo.Hivi ndivyo nionavyo mimi
   
 5. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu kwanza naona kuna vitu vinachunganya s nakushauri soma na tazama videoclip wenye kiuganishi hiki. DIGITAL TELEVISION . NINI TUTARAJIE? - teknohama-Bongo

  Itakusaidia kuelewa na kuondoa manganyiko fulani ulionao. ingwa binafsi sio telecommunication engineer but nina interest na kufuatlia haya mambo kwa karibu
   
 6. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 953
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Tusilinganishe jiografia ya nchi yetu na ya wenzetu haya mambo bado, miundo mbinu ya nchi yetu haijakidhi haja ya kuwa na mfumo wa kidigitali tusikurupukie jambo kama tunavyokurupukia hii mikataba baadae tunalizwa naamini hiyo 2012 wanayosema itafika lakini bado si nusu ya nchi itakuwa bado haijafikiwa na mfumo huu.!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...