hapo ndugu yangu hakuna msaada wowoteNchi hii inautitiri wa kodi, na rais wetu mpendwa alilizungumzia sana kipindi cha kampeni. na ndio mifumo hii mibovu inayochangia wazawa kuwa masikini na kushindwa kufanya innovation au kufungua viwanda vidogovidogo vyenye kuzalisha bidhaa nafuu na kutoa ajira.. kuendelea na mifumo hii ni kuruhusu umasikini usio na kikomo kwa walala hoi wengi ambao ndio wanashabikia ccm na kuliwa kodi na kuchekelea.
mfano tazama hii
View attachment 327247
Ada ya ukaguzi wa vifaa vya zimamoto inaumuhimu gani hapo? je TRA wanagawa fire extinguisher?Je trafik anaekagua halipwi mshahara na hiyo pesa humlipa ruzuki ya kukagua trafik? ILi mradi tu ni visheria vinavyo waongezea mzigo wa kodi wananchi na hivi vilitungwa na ccm ktk mfumo ccm. Tunaomba rais wetu mpendwa JPM atimize wajibu kwa kutusaidia wananchi kupunguziwa kodi ili wazawa wajipambanue ktk kutumia raslimali tulizonazo kujikwamua kiuchumi na kuzipiku nchi zinazotuzunguka...lkn tukiendelea hivi tutabakia kushangilia majipu na hapa kaz# mwisho umaskini na hali ilele na mambo yaleyale.
Pia nimuombe rais wetu asimame imara kukemea ukandamizaji wa demokrasia unaofanywa na ccm ktk chaguzi za umeya na kule zanzbar. ni matumaini yangu rais wetu mpendwa wa JMT ataliona hili na kulifanyia kazi na mwisho automatic atasifika kuwa rais wa karne bila kujisifia mwenyewe.
CCM ni hatari kwa ustawi wa taifa siku za usoni kama watanzania hawatagutuka mapema!!!hapo ndugu yangu hakuna msaada wowote