Tanzania na Katiba Mpya au Katiba ya Zamani

mayaJr45

JF-Expert Member
May 12, 2016
560
205
Jaji Lubuva ametangaza majuzi wanamalizia maandalizi ili katiba mpya iweze kupigiwa kura .Na maswali kadhaa

(1)Watanzania tumejiandaa kwa hilo na tupo tayari ?

(2)Na kama hatupo tayari kwanini hatupo tayri?

(3)Tumeisoma vyema katiba hii mpya pendekezwa?

(4)Msukumo wa kisiasa na ushabiki utatufikisha mwisho wa jambo hili jema?

(5)Ni bora kuendelea kutumia katiba iliyopo au ni bora kuipigia kura katiba pendekezwa ili iwe katiba yetu?

(6)Katiba pendekezwa na katiba ya sasa ipi inajibu changamoto mbalimbali za kiuchumi kijamii kisiasa na changamoto nyingine?

Ukifuatilia jambo kwa undani utapata jawabu kuwa mchakato wa kupata katiba mpya umehodhiwa na wanasiasa kwa sehemu kubwa.ilikujua wanasisa wamehodhi jambo lililotawala ni serekali tatu au serekali mbili .Sio jambo geni maana infuence ya siasa mwisho wa siku ni kutaka madaraka tu.

Kuna mambo mengi yamezungumzwa ya msingi sana kwenye katiba pendekezwa na yanawagusa watu wengi kwenye sekta mbalimbali je tunaopinga tumeshawahi kukaa na makundi haya kama Wafugaji,Wakulimaa,Wavuvi, watu wenye ulemavu na kujua mapendekezo yao na kero zao yamewekwa ili yashughlikiwe kikatiba ndio tuje na dhana mbali mbali za kupinga ?

My take .

Huwezi kupata yote unayokusudia kwa wakati mmoja hata kwenye maisha ya kawaida, ukipata ambacho kinakupa unafuu wa kuendelea kutafuta kupata yote ni afadhali uchukue hicho kidogo kwanza .Tujiandae kwa kura hiyo kwa kusoma na kulingamisha kikatiba utatuzi wa changamoto mbalimbali za ardhi ,ufugaji , upatikanaji wa huduma za kijamii ,demokrasia kati Katiba iliyopo na katiba pendekezwa.
 
Back
Top Bottom