Tanzania na China zasaini mkataba wa uendelezaji wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR kutoka Mwanza - Isaka

huko ndiko hakuna biashara? ukiacha mengine idadi kubwa ya watanzania ipo mikoa ya Shinyanga,Simiyu,Mara,Mwanza,Kagera,Geitana Tabora umbari kutokamikoa hii hadi bandari ya salama ni kati km 700 hadi 1300,tofauti yabei za bidhaa kati ya Dar na mikoa hii ni kubwa mno kutokana na gharama za usafirishaji kwa kuwaona watanzania hawa na kuwahudumia ni sahihi zaidi kuliko kuangalia biashara na Kongo kwanza lakini korido hiyo iko kimkakati vizuri sana sio kidogo kwani kuna Rwanda,Burundi na Uganda. ukifikisha reli Mwanza tayari umefika uganda kwani tayari pale pana meri za kubeba mabehewa kwenda Uganda,lakini pia mzigo ukifika Isaka huo tayari umefika Rwanda,Burundi maana toka isaka hadi kwenye mpaka ni safari ya masaa tu.
Mkuu, kwani unadhani makamanda hawayajui hayo? Wanaujua huo ukweli, ila bongo zao walikabidhi kwa tundu na akaondoka nazo kwenda kwa shoga yake Amsterdam huko ubeberuni!
 
Dar-Moro=300Km

Moro-Makutupora=426Km

Makutupora-Isaka=435Km

Isaka-Mwanza=220Km

Isaka-Rusumo=371Km

Kwa nini kazi zisiende kwa mfuatano ili hata ngoma ikikwama njiani ruti iwepo ya kuishia hata Isaka.

Wachina watamaliza na kukabidhi Isaka-Mza huku kipande cha Makutu-Isaka kikiwa bado hata tenda haijatangazwa halafu anaingia Rais mwingine na kusema reli siyo kipaumbele chake,mradi unaachwa kwenye mataa kama katiba mpya tunakuwa tumepoteza pesa bure.
Nashukuru umeliona hili na wewe...unajua nimejiuliza sana nini hiki? Anyways akili ya mwafrika utategemea nini? Na mchina atamaliza ndio wakati hata hatujaunganisha dodoma-isaka.
 
Kama nilimsikia vizuri msemaji wa kampuni ya kichina iliyopewa ujenzi wa reli ya kutoka Mwanza kwenda Isaka, alizingumzia kuhusu vipande ulivyo taja hapo juu, kwamba wanaweza kusaidia katika ujenzi wa sections hizo wakitakiwa kufanya hivyo, vile vile nilimsikia Waziri wa miundo mbinu na ujenzi akigusia kwa mbali sections hizo tajwa na kutoa impression as if watapewa Wachina kuzimalizia itakapo bidi - I might be wrong lakini reading between the lines naona huko ndiko tutakapo elekea eventually ni suala la muda tu, Wachina hawakwepeki - binafsi hilo naona ni sawa tu tunacho taka ujenzi wa reli ukamilike kama ilivyo pangwa tangu mwanzo.
Swali; kwanini waanzie Mwanza na sio Dodoma kuja Isaka? Hauoni kuna shida sehemu? Ningeelewa kama tender zingekuwa zimetangazwa za dodoma isaka.
 
TANZANIA NA CHINA YASAINI MKATABA WA KUJENGA RELI YA KISASA (MWANZA-ISAKA)

Serikali ya Tanzania na China vimeingia makubaliano ya kujenga reli ya kisasa ya Kilometa 341 kutoka Mwanza hadi Isaka

Hicho ni kipande cha tano, ambapo kipande cha Kwanza ni kutoka Dar mpaka Morogoro, Cha pili ni kutoka Morogoro hadi Makutupora

Kipande hiko cha tano kitajengwa na kampuni ya ujenzi ya China. Mkataba wake umetiwa saini mbele ya Rais Magufuli.

---
HOTUBA YA RAIS MAGUFULI (KWA UFUPI)
Naipongeza Kampuni ya Kichina kwa kushinda zabuni ya ujenzi wa reli ya kisasa Kilometres 341 kutoka Mwanza hadi Isaka( mradi una gharama ya Tril 3.0677), nina matumaini watafanya kazi kubwa.

Ujumbe kutoka kwa Rais wa China Xi Jinping, tumeupokea lakini na mimi nimetuma ujumbe mwingine umfikishie Rais wa China na mimi mambo niliyomueleza ni masuala ya kushirikiana kwa hizi nchi mbili katika masuala ya kiuchumi.

Kwa ujumla mazungumzo tuliyoyafanya yalikuwa mazuri na nimemhakikishia Tanzania itaendelea kushirikiana na China kwa sababu ni ndugu zetu, sasa ni wakati wa Tanzania na China kujenga uchumi kwa nguvu zote na kuonesha ushirikiano mkubwa.

Rais Xi Jinping nimemuomba watusaidie katika miradi mikubwa mitatu kule Njombe, nimemuomba watujengee KM 48 kule Zanzibar.

Nimewaeleza hali halisi kwamba China ni Nchi Tajiri Duniani, na sisi Tanzania tuna mazao mengi, ndio maana kwenye zawadi zangu nimetoa korosho, chai na kahawa, nataka wakaanze kula korosho za Tanzania badala ya Nchi nyingine, huu ndio wakati wa kulishika soko la China. Endapo kila raia wa China atakula korosho nusu kilo, maana yake watakuwa wanakula Tani Mil 750, korosho zote zinazolimwa Tanzania zitaisha.

Nimemuomba Waziri wa Mambo ya Nje China Wang Yi, akafikishe salamu zangu kwa Rais Xi Jinping kwamba watusamehe madeni ikiwemo deni lile tulilolibeba wakati tunajenga reli ya TAZARA, deni la nyumba za Askari USD 137 M, na deni la kiwanda cha urafiki USD 15 M, nimeomba watufutie kwasababu China ni Rafiki zetu, pia wao ni Matajiri.

Nampongeza sana Waziri Wang Yi kwasababu hajavaa barakoa maana anajua Tanzania hakuna Corona na kwa kumuhakikishia nakwenda kumshika mkono tukale chakula.
Wachina ni binadamu kama sisi ila wanatoka sayari nyingine. Wamepambana kushinda zabuni ya ujenzi kwa eneo lenye madini mengi, naona hata wakitujengea bure watakuwa wamejilipa maradufu
 
Ni vizuri lakini kutumia neno wameshinda zabuni wakati zabuni haijatangazwa ukweli ni kwamba wametoa mkopo tukawapa wajenge lakini sio kweli kwamba wameshinda zabuni!
Zabuni zilitangazwa mkuu. Watendee haki. Si vema kusema uongo. Kama hujui uliza kwanza ujulishwe.
 
DED wa Geita alinunua gari la milioni 400.

Waziri wa Mambo ya nje wa China katoa msaada wa milioni 380.
Nipo nje ya maada
Hilo la DED halikubaliki, ni wendawazimu. Ila pia ujue kua akija rafiki yako tajiri nyumbani kwako akakupatia chunvi ya sh 500 utakuwa mwendawazimu pia kukataa.
 
Waturuki waliokuwa wanaimbwa kama Wimbo wa Taifa wameshidwa kazi? Wakati Waturuki wakipewa Dar-Moro kwa pesa zetu, viongozi wetu hawakuwaona Wachina? Miradi mingi ya Awamu hii ni substandard kwa sababu ya makandarasi dhaifu, je kugawa Mradi mmoja vipandevipande kila kipande na mkandarasi wake, haiwezi kuwa ndo sababu? TAZARA imejengwa na Wachina na ina umri karibu miaka 50, je imeleta faida gani kwa Taifa? Kipande cha Dar-Moro mbona hata hakiimbwi wala hakitajwi kimefika wapi na lini Walugulu wataanza kufaidi matunda ya Awamu ya Tano? Dar-Moro ni km 300 na ilikuwa ikamilike Novemba, 2019, Mwanza-Isaka ni km 340, ni lini Wasukuma wapiga kura wataachana na Musukuma Bus Service? Maswali mengi!
Mkuu, lengo la kugawa mradi kwenye vipande vingi ilikuwa pamoja na mambo mengine kuweka kandarasi tofauti kila kipande. Nielewe vema, kandarasi tofauti na si mkandarasi tofauti. Hivyo kwa mfano, lots one na two zina kandarasi tofauti hata kama mkandarasi ni kampuni moja.

Kuwapa Wachina lot 5 haizuii kuwapa wengine lots 3 na 4. Usishangae Mturuki akapewa tena lot mojawapo. Kila tenda hutangazwa kivyake.

Pia walichoombwa Wachina kwenye lots 3 na 4 ni kutusaidia financing. Hakuna aliyewahakikishia kuwa tenda watapewa wao.
 
Mbona maswali yako ni totally incoherent! Kama kuna walio kuelewa wanisaidie.

Labda nizungumzie kuhusu TAZARA, ni kweli inaendeshwa ki hasara hasara bahati mbaya Serikali zetu mbili hazijawahi kulivalia njunga suala hili - TAZARA inaendeshwa kisiasa zaidi kuliko kibihashara - binafsi nilisha guduwa kwamba Serikali ya Zambia na Tanzania zinaoneana aibu, hakuna anae kubali kumfunga paka kengere!

Kuna mambo mengi ya kipuuzi yanatendeka bila ya Serikali zetu hasa ya Tanzania kuchukuwa hatuwa yoyote, mfano: kuna mantiki gani kwamba Managing Director wa Tazara lazima awe Mzambia hata kama hana sifa, kipengele hicho kimekuwa grossly misused, wanatumika kuuza mali zote za Tazara upande wa Tanzania siyo upande wa Zambia - waliuza Kurasini material base ikiwemo aridhi kubwa na majengo/Godowns yenye thamani kubwa waliwauzia Wahindi kwa hela zakutupwa, wakamega sehemu ya aridhi ya Tazara iliyojengwa nyumba za wafanyakazi huko Temeke Maganga karibu na Vetenary wakuwauzia Kampuni ya Oil Com, wakaenda TAZARA DSM Railway station sehemu ya Cargo base wakamkodisha Mhindi sijui kwa terms zipi, kinacho sikitisha zaidi ni uuzaji/ukodishaji wa chunk kubwa ya aridhi karibu na karakana ya TAZARA mnunuzi/mkodishaji kajenga depot kubwa ya kuhifadhi containers, kibaya zaidi alipora jengo lililo kuwa linatumika kitengeneza/service fuel injector pumps za locomotives na ku-calibrate injector nozzles - machines/equipment za gharama kubwa na umuhimu wa pekee zikang'olewa na kutupwa wapi sijui, hizi ni hujuma za wazi wazi - hivi sasa jengo hilo linatumiwa na Mhidi huyo kama ofisi ya kuratibu ma-containers yake, yaani yeye na-washirika wake wanaona Ofisi ni ya muhimu zaidi kuliko jengo na mali za TAZARA, ujasiri huu anaupata wapi??

Juzi juzi hapa nilipita sehemu hiyo tajwa nilishangaa kukuta sio kwamba Mhindi anahifadhi ma-containers tu bali amekwenda mbali zaidi na kujenga kituo kikubwa cha uuzaji mafuta, awezi kujenga kituo cha kuuza mafuta bila ya kumilikishwa aridhi kwanza! Swali ni,je, nani anampatia kibali cha kupora aridhi ya Tazara, jengo la Taraza, kujenga kituoa cha mafuta na kufanya apendalo as if Serikaki yetu imekwenda likizo?

Binafsi nashauri Dk. Magufuli,Wizara ya uchukuzi, PCCB, na vyombo vingine vya dola fatilieni suala hili kwa karibu zaidi ili kubaini undani wake na kuchukuwa hatua stahiki, hujuma za mali za TAZARA upande wa Tanzania ni kubwa mno - upande wa Zambia hawauzi chochote, kila kitu kipo intact kabisa.

Hapa nimezungumza mambo machache tu yanayo kwamisha utendaji mzuri wa Shirika, tatizo ni hujuma na kutojari ustawi wa TAZARA - Shirika likitaka kuendeshwa kiufanisi liondokane na kasumba ya kuendesha shirika kisiasa, hakuna mantiki yoyote ya kusema Mkurugenzi mkuu lazima atoke Zambia, kaimu wake Mtanzania, Mkurugenzi wa fedha Mzambia, Mkurugenzi wa Traffic Mzambia yaani mission critical posts zote wanapewa Wazambia hapo unategemea nini - tutavuna tunacho panda, lakini cha ajabu Board members wa Tazara upande wa Tanzania sio kwamba hilo hawalioni hawasemi chochote wapo kimya kabisa.

Kwa kumakizia risala yangu ndefu nataka kukufahamisha kwamba utendaji mbovu wa TAZARA wasilahumiwe Wachina, wachawi wa reli ya Tazara ni sisi wenyewe - maswali mengine kuhusu ujenzi wa SGR nimeshindwa kukujibu kwa sababu sijui unataka kujua nini!!
Safi sana kwa maelezo marefu yasiyochosha. Nadhani bro Magu anajua kinachoitesa TAZARA ndiyo maana aliagiza upelekwe bungeni muswada wa kuruhusu kila nchi mshirika iwajibike kuendeleza upande wake wa reli.
 
Swali; kwanini waanzie Mwanza na sio Dodoma kuja Isaka? Hauoni kuna shida sehemu? Ningeelewa kama tender zingekuwa zimetangazwa za dodoma isaka.
Mkuu, hapo lengo ni kuwahakikishia Waganda na potential financiers kuwa mradi utatekelezwa ili isitutokee kama inayowatokea Wakenya. Uganda wana maamuzi yao ya kufanya juu ya wapi wanaelekeza reli yao kwanza; Tz au Kenya.

Sijui ni kwa vipi watu wanaoonekana wazi wana zero understanding na masuala haya wanakesha hapo kuponda hiki au kile. Kuna mwingine eti anauliza tenda ilitangazwa lini! Sasa huyo si zero brain anapaswa kusoma tu kimya kimya kama library!
 
Back
Top Bottom