MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 295
- 679
Tanzania na Brazil zimeingia makubaliano ya kuinua kilimo cha Pamba ili kiwe na tija kwa wakulima nchini.
Makubaliano hayo yamejili wakati ambapo Brazil ipo katika hatua kubwa za kimageuzi ya kilimo huku ikiwa na mafanikio makubwa katika sekta hiyo ambapo unatekelezwa katika nchi tatu za Burundi, Kenya na Tanzania.
Mradi wa kuinua kilimo cha Pamba unaotekelezwa na Brazil nchini Tanzania utajikita Zaidi hasa katika kuhakikisha wakulima nchini wanapata Pamba mbegu bora na uzinduzi wa utafiti utamfikia mkulima ili aweze kuongeza tija.
Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa ameyasema hayo jana tarehe 11 Machi 2019 mara baada ya kutembelea na kukagua mashamba ya mfano wa kilimo cha Pamba katika kituo cha Utafiti TARI-Ukiriguru Mkoani Mwanza.
Bashungwa amesisitiza kuwa serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kwa kauli moja kuimarisha sekta ya kilimo huku katika zao la Pamba imejipanga kuhakikisha inazalisha mbegu vipara za Pamba zitakazotosheleza kwa wakulima wote
nchini na kuondokana na utumiaji wa pamba manyoya ambayo imezoeleka lakini tija yake ni ndogo katika uzalishaji kuliko Pamba Manyonya.