Tanzania na Brazil kuinua kilimo cha Pamba nchini

MIMI BABA YENU

Senior Member
Mar 1, 2019
196
500
Tanzania na Brazil zimeingia makubaliano ya kuinua kilimo cha Pamba ili kiwe na tija kwa wakulima nchini.
Makubaliano hayo yamejili wakati ambapo Brazil ipo katika hatua kubwa za kimageuzi ya kilimo huku ikiwa na mafanikio makubwa katika sekta hiyo ambapo unatekelezwa katika nchi tatu za Burundi, Kenya na Tanzania.

Mradi wa kuinua kilimo cha Pamba unaotekelezwa na Brazil nchini Tanzania utajikita Zaidi hasa katika kuhakikisha wakulima nchini wanapata Pamba mbegu bora na uzinduzi wa utafiti utamfikia mkulima ili aweze kuongeza tija.

Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa ameyasema hayo jana tarehe 11 Machi 2019 mara baada ya kutembelea na kukagua mashamba ya mfano wa kilimo cha Pamba katika kituo cha Utafiti TARI-Ukiriguru Mkoani Mwanza.

Bashungwa amesisitiza kuwa serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kwa kauli moja kuimarisha sekta ya kilimo huku katika zao la Pamba imejipanga kuhakikisha inazalisha mbegu vipara za Pamba zitakazotosheleza kwa wakulima wote
nchini na kuondokana na utumiaji wa pamba manyoya ambayo imezoeleka lakini tija yake ni ndogo katika uzalishaji kuliko Pamba Manyonya.
1552399410599.png
 
bababikko

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
2,393
2,000

View attachment 1043966
Kuna waturuki nao walisema ivyo ngoja tusubiri tuone
 
muchetz

JF-Expert Member
Aug 16, 2010
921
1,000
Bashungwa amesisitiza kuwa serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kwa kauli moja

Huwa napata tabu sana.... hivi unaposema Serikali ya Tanzania inyoongozwa na JPM, una maanisha kuwa serikali ya Tanzania itakayoongozwa na mtu mwingine haitakuwa na hiyo dhamira. Kwani kusema tu serikali ya Tanzania(bila kuhusisha jina la mtu kuna ubaya gani?) Uandishi wa kishabiki kunapoteza mantiki na uzito wa habari yako kama upo.
 
kirikou1

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
4,075
2,000
Huwa napata tabu sana.... hivi unaposema Serikali ya Tanzania inyoongozwa na JPM, una maanisha kuwa serikali ya Tanzania itakayoongozwa na mtu mwingine haitakuwa na hiyo dhamira. Kwani kusema tu serikali ya Tanzania(bila kuhusisha jina la mtu kuna ubaya gani?) Uandishi wa kishabiki kunapoteza mantiki na uzito wa habari yako kama upo.
Maana yake kwa maandishi hayo teuzi zatafutwa kwa udi na uvumba
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom