Tanzania na Afrika Kusini zaja na tamasha la msimu wa utamaduni

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,623
01..-1024x683.jpg

Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bwana Haji Janabi (kushoto) akiongea na wajumbe wa Kamati ya Maandalizi kutoka Tanzania na Afrika Kusini katika kikao awali kufikia kwa maandalizi ya Tamasha la Msimu wa Utamaduni wa Afrika Kusini nchini Tanzania ambalo linatarajiwa kufanyika kuanzia mwishoni mwa mwaka 2022 hapa nchini. Katikati ni Bwana Ruphus Matibe Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kimataifa Idara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni kutoka Afrika Kusini na Corry Masilela Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Matukio (wa kwanza kulia)

02..-1024x683.jpg

Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bwana Haji Janabi (wa pili kulia) akiwa na ujumbe wa Afrika Kusini wakati wa maandalizi ya Tamasha la Msimu wa Utamaduni wa Afrika Kusini nchini Tanzania ambalo linatarajiwa kufanyika kuanzia mwishoni mwa mwaka 2022 hapa nchini. Wa pili kulia ni ni Bwana Ruphus Matibe Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kimataifa Idara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni kutoka Afrika Kusini
03..-1024x683.jpg

Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi kutoka Tanzania na Afrika Kusini wakitembelea eneo la Makaburi ya wapigania Uhuru yaliyopo Mazimbu mkoani Morogoro ikiwa ni maandalizi ya Tamasha la Msimu wa Utamaduni wa Afrika Kusini nchini Tanzania ambalo linatarajiwa kufanyika kuanzia mwishoni mwa mwaka 2022 hapa nchini.
04..-683x1024.jpg

Bwana Ruphus Matibe Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kimataifa Idara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni kutoka Afrika Kusini akitembea mti wa Khaya Antotheca (Mkangazi) ambao ulipandwa Julai 09, 2012 Mazimbu mkoani Morogoro na aliyekuwa Makamu wa Rais wa ANC na Serikali ya Afrika Kusini Mhe. Kgalema Montlanthe.
05..-683x1024.jpg

Bwana Ruphus Matibe (kulia) Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kimataifa Idara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni kutoka Afrika Kusini akipokea vitabu vya Kiswahili ikiwemo Kamusi Kuu ya Kiswahili Toleo la Tatu jijini Dar es Salaam
06..-1024x683.jpg
07..-1024x683.jpg

Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Msimu wa Utamaduni wa Afrika Kusini nchini Tanzania kutoka Tanzania na Afrika Kusini wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kikao cha maandalizi ya Tamasha la Msimu wa Utamaduni wa Afrika Kusini nchini Tanzania ambalo linatarajiwa kufanyika kuanzia kuanzia mwishoni mwa mwaka 2022 hapa nchini.
08..-1024x683.jpg

Wajumbe wa Kamati ya Maandalizi kutoka Afrika Kusini waliovaa shuka la Kimaasai wakiongozwa na Bwana Ruphus Matibe Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kimataifa Idara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni kutoka Afrika Kusini (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kikao cha maandalizi ya Tamasha la Msimu wa Utamaduni wa Afrika Kusini nchini Tanzania ambalo linatarajiwa kufanyika kuanzia kuanzia mwishoni mwa mwaka 2022 hapa nchini.
……………………………………….
Na Eleuteri Mangi, WUSM-Dar es Salaam

Tanzania na Afrika Kusini zimedhamiria kukuza ushirikiano katika Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo amabyo ni sehemu ya utekelezaji wa Mkataba wa Ushirikiano uliosainiwa mwaka 2011.

Utekelezaji wa Mkataba huo baina ya nchi hizo mbili unakuja na utaratibu wa kuwa na Tamasha la Msimu wa Utamaduni wa Afrika Kusini nchini Tanzania ambalo lengo lake ni kuunga mkono juhudi za kupanua wigo wa utalii, biashara za bidhaa na huduma za kiutamaduni.

Akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na wajumbe wa kamati ya Maandalizi kutoka Tanzania na Afrika Kusini, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bwana Haji Janabi amesema kikao hicho cha siku nne kuanzia Agosti 1- 4, 2022 ni hatua za awali kufikia azma hiyo ya kufanyika kwa Tamasha la Msimu wa Utamaduni wa Afrika Kusini hapa nchini.
Tamasha la Msimu wa Utamaduni wa Afrika Kusini linatarajiwa kufanyika katika maeneo manne hapa nchini ambayo yamebeba Historia ya Afrika Kusini katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro na Zanzibar.

Dhima kuu ya tamasha hilo ni kuwa na jukwaa la kuonesha vipaji vya Sanaa na Utamaduni, kukuza ushirikiaano wa kikanda, kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Afrika Kusini, maonesho ya mavazi, mihadhara ya umma pamoja na midahalo yenye lengo la kutoa elimu kwa jamii baina ya nchi hizi mbili.

Kwa upande wake Bwana Ruphus Matibe Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kimataifa kutoka Idara ya Michezo Sanaa na Utamaduni kutoka Afrika Kusini amesema msimu huo wa Utamaduni wa Afrika Kusini nchini Tanzania unataraiwa kuanza na tamasha hilo Tanzania ambalo linatarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 17 hadi Desemba 04, 2022 hapa nchini kwa lengo la kuwakumbusha watu wa nchi hizo mbili historia yao njema tangu enzi za Harakati za Ukombozi chini ya Waasisi wa mataifa hayo mawili chini ya waasisi Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Nelson Mandela wa Afrika Kusini.

“Tupo hapa kuunganisha watu wa Afrika Kusini na wazee wao, Tanzania hatukupewa tu ardhi wakati wa harakati za Ukombozi, tulipewa mahali pa kuishi kulingana na ukarimu wa watanzania wakiongozwa na Hayati Mwl. Julius Nyerere” amesema Bwana Matibe.

Bwana Matibe ameongeza kuwa wazee wa mataifa hayo waasisi na wananchi wa mataifa hayo wakati huo walitekeleza wajibu wao wa kuhakikisha wamejenga umoja katika nchi zao hatua iliyosaidia kupatikana uhuru na kusisitiza kuwa Tamasha la Msimu wa Utamaduni wa Afrika Kusini nchini Tanzania ni moja ya fursa kwa kizazi cha sasa kutatua changamoto za kiuchumi zinazokabili nchi za Afrika.

Akizungumzia mafanikio ya harakati za Ukombozi wa nchi hiyo wakiwa Tanzania ambayo wanaitambua kuwa ni nyumbani kwao, Bwana Matibe amesema kiunganishi kikubwa kati yao na Watanzania ilikuwa ni lugha ya Kiswahili ambayo asili yake ni ya Afrika tofauti na lugha nyingine zilizotumiwa na wakaoloni.
Ili kuenzi tunu hiyo ya Kiswahili ambayo ni lugha ya kazi sasa katika Umoja wa Afrika (AU), Bwana Matibe amesema Afrika Kusini wapo mstari wa mbele kufundisha lugha ya Kiswahili kwa shule za msingi nchini humo ambapo tayari nchi hizo mbili zimesaini mkataba wa makubaliano ya kufundisha somo hilo Julai 07, 2022 wakati wa Maadhimisho ya Kwanza ya Siku ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam.

Source: Fullshangwe blog
 
Imekaa vizuri
 
Kwenye vitu vya hovyo wana A ila wambie Bando, Sabuni na Mafuta juu. Utaskia Vita Ukraine utadhani Russia imepandisha mafuta bei.
 
Back
Top Bottom