Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Jana Rais wangu mpendwa, Amiri jeshi mku mtukufu John Pombe Magufuli amezungumzia hali ya kiasia visiwani Zanzibar na kuweka bayana kwamba kamwe hataingilia mgogoro huo kwa kuwa Tume ya Uchaguzi ZEC ina uhuru wa kujiamulia mambo yake kama ambavyo inaona inafaa, bila kuingiliwa . Wazee wa Dar es salaam walishangilia sana ijapokuwa hawakuonekana kukijua wanachoshangilia.
Lazima nikiri kuwa mimi nimeshindwa kumuelewa kama kweli anayaamini anayoyasema kuwa Tume iko huru na haiingiliwi na yeyote.
Lakini bado tunakumbuka vikosi vyake vilipoizingira Nyumba lakutolea matangazo ya uchaguzi,Bwawani na vipi Naibu mwenyekiti wa Tume alvyo dhalilishwa na kuchukuliwa kijeshi na polsi na kuzuiwa asiendelee na kutangaza matokeo, kabla Jecha hajafuta uchaguzi; je hii ndio tafsiri ya UHURU WA TUME? au ina maana kuwa serikali ya Zanzibar ina mamlaka kamili ya kujiamulia mambo yake hata ikiwa ndivyo sivyo na mambo yaliobakia kwenye Mamlaka ya muungano ni ulinzi tu ! ina maana Muungano wa mkataba unakaribia?
Rais wangu pia anasema “Mtu yeyote (isipokuwa Mazombie) ambaye atathubutu kuleta chokochoko iwe Pemba, Unguja,........ watajua kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vipo na vitawashughulikia kikamilifu.”
Lakini hapa na hoja ikiwa kweli tunathamini uhuru wa Tume na sio maslahi ya kisiasa, kwa nini tunaingilia maamuzi ya Tume ya Burundi waliomtangaza Nkuruzinza na tunashiriki kufuata mwafaka na kuwa na kigugumizi kwa Zanzibar? Msema kweli ni mpenzi wa mungu, lakini ni mungu gani huyu anamuabudu Rais wangu na anaowachukia na kutowajali wazanzibari na kuwathamini waburundi?
Naomba mnieleweshe!