Tanzania Mpya tunayoitaka

DOFFA

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
425
233
MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YANAWEZEKANA KAMA YAFUATAYO YATAPEWA KIPAO MBELE NA NCHI TUKIONGOZWA NA SERIKALI:
1. Kusimamia sera ya kijamaa na kujitegemea ili kutumia ardhi yetu inavyopasa pamoja na rasilimali zingine.

2. Serikali na Taasisi zingine kutoa elimu kama huduma kwa jamii siyo biashara na serikali isimamie miongozo na sera kikamilifu ili kutoa elimu sawa kwa wote.

3. Serikali isimamie vizuri rasilimali za nchi kama utalii,madini,gesi,anga,bandari,uvuvi,mifugo na kilimo ili yote haya yawe na mchango mkubwa kwenye maeneo muhimu kwa nchi mf.maeneo ya huduma na biashara.Ili kila mtu ajenge nyumba bora lazima bei ya vifaa ya ujenzi ishuke na kuwa rafiki kwa watu wote.{supply=/> demand}.

4. Uwekezaji kwenye utafiti wa ukweli ufanyike ili kuwa na njia bora ya utekelezaji wa vipao mbele vya nchi kwa maslahi ya taifa na miradi isimamiwe kwelikweli,tuache utani wa kuchekeleana ila tuheshimiane.

5. Katiba ya nchi iwe ni msingi wa kusimamia rasilimali zake kwa faida ya watu wake wote kuzingata usemi usemao-''People who living in glass houses should not throw stones''.

Tafsiri isiyo rasmi ni kwamba ''SIYO VIZURI KURUSHIANA MAWE KWA WATU WAISHIO NYUMBA ZA VIOO''.

6.Viongozi wa kisiasa kuacha kutumia lugha za kiuchochezi,lugha ya kuudhi,kukatisha tamaa,lugha za kibabe-TUWE NA LUGHA YENYE STAHA ISIYO NA UKAKASI.

KIONGOZI WA NCHI APEWE NAFASI YA KUTIMIZA VIPAOMBELE VYAKE KWA WAKATI ILI ASIWE NA VISINGIZIO VINGINE.
 
Atawale kwa kufuata misingi ya sheria na katiba, ni hilo tu ndiyo tunamuomba, asitawale kwa kutumia akili yake
 
Atawale kwa kufuata misingi ya sheria na katiba, ni hilo tu ndiyo tunamuomba, asitawale kwa kutumia akili yake

Tatizo kubwa lipo kwenye katiba ambayo inampa mkuu wa nchi mamlaka mkubwa kupita kiasi hivyo kuifanya katiba iwe kama kivuli na kuupa nguvu mfumo wa chama kimoja.
 
Tatizo kubwa lipo kwenye katiba ambayo inampa mkuu wa nchi mamlaka mkubwa kupita kiasi hivyo kuifanya katiba iwe kama kivuli na kuupa nguvu mfumo wa chama kimoja.
Sasa nini kifanyike?
 
Namba 4. Mashirika na makampuni ya simu yadhamini watu wetu wa ndani kufanya tafiti za maana. Tuachane na kusubiri wazungu watupe kwani wakitupa wao tafiti zitakuwa kwa masrahi yao. Tufanye wenyewe tunaweza
 
Ndungu yangu DOFFA umeongea vizuri!!Ila kwa nchi yetu hii!!bado sana tena kwa hali inavyoenda!!sijui
 
Ndungu yangu DOFFA umeongea vizuri!!Ila kwa nchi yetu hii!!bado sana tena kwa hali inavyoenda!!sijui
Ni kweli DAFFI aisee umeona safari ni ndefuueeeh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom