Tanzania Mpya: Ndoto ya Radio Producer. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Mpya: Ndoto ya Radio Producer.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Radio Producer, Jul 26, 2012.

 1. Radio Producer

  Radio Producer JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Poleni na kazi Wadau.
  Nimeona niweke wazi leo ndoto yangu juu ya fikra yangu dhidi ya Tanzania Mpya. Katika mifano yote nitakayoitoa siiombei Tanzania kuingia kwenye shida wala jambo lolote baya ila kama hakuna mabadiliko hayo yote yanaweza kutokea.

  Mara zote ndoto ndiyo njia kuu ambayo Mungu alitumia kuongea nawatumishi wake enzi hizo vile vile hata leo kwa watumishi wa sasa. Naamini kuwa haya ni MAONO toka Mungu mwenye macho na Asikie maneno haya:-

  1. Haki
  Kwa wale tusioweza kutambua vizuri zaidi haki Tanzania imetoweka kabisa hasa pale mahakama ilipoonyesha daliliza kutumika kisiasa kama vyombo vya habari vinavyosema. Ukweli uko hivi kama Tanzania itaendelea hivi inaziba milango ya kupatikana kwa UKOMBOZI maana hakuna mtu atakayekubali kuondoka madarakani na kumwachia mwingine.

  2015 ni mwaka wa hatari sana kwani kuna mawili tu eidha Vita au CCM kubaki madarakani, nakuhakikishieni kuwa kama haki itaendelea kwa mtindo huu basi ujue hakuna njia ya ukombozi Tanzania. Ni mambo mengi sana yanatokea lakini hakuna haki inayotendeka.

  2. Ndoto ya Radio Producer.
  Hii Tanzania imekuwa kama Nigeria kuna vituko vingi hujapata kuona na hakuna msaada wowote. Sasa basi katika maono yangu nimefundishwa kuwa Tanzania inaweza kukombolewa kwa MAOMBI tu. Natamani nipate nguvu makanisa yote Tanzania tuunganishwe tupate kuwa na maombi tu ya siku 7 ya kufunga na kuomba juu ya utawala mbovu uliopo ili uweze kuangamizwa hata mwezi ni mkubwa mno Tanzania ingekuwa mpya.

  Najua UMOJA ndiyo unatenda maajabu, ndiyo maana hata siku ya Pentecoste wale watu walikuwa pamoja. Hata sasa tukiwa pamoja tukaungana nchi nzima kumlilia Mungu auangamize utawala mbovu uliopo, hakuna risasi, wala damu ya mtu itakayomwagika na Tanzania itakuwa nchi mpya.

  Ndoto yangu radio producer ni Kuunganisha Timu ya Kitaifa ya Maombi kwa ajili ya kuomba ukombozi kutoka kwa Muumba Mbingu na Nchi. Najua ipo siku itatimia.
   
Loading...