SoC04 Tanzania Mpya: Mambo ambayo tunapaswa kuyafanyia mageuzi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Anordynho

Member
Apr 24, 2024
5
2
ELIMU: Tunajua kuwa elimu ni kitendo kinachohusishaa masuala mazima ya mabadilishano au urithishwaji wa maarifa, mawazo na ujuzi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwinginee ay jamii moja kwenda kwenye jamii nyingine.

Katika TANZANIA tuitakayo tunatakiwa kubadlishaa mfumo wa elimu kuwa wa vitendo zaidi ili kupunguza utegemezi wa wanafunzi kwa serikali kuajiriwa baada ya kumaliza masomo yao pia kuanzisha na kusimamia masomo kama kilimo, sanaa ya ufundi na biashara kutoka ngazi ya sekondari pia kuboresha na kuimarishaa vyuo vya ufundi na pia katika elimu tuwe na mfumo ujulikano kama uibuaji wa vipaji kama mchezo wa mpira, uimbaji, ubunifu sidhani kama mwalimu aliyekaa na mwanafunzi kwa miaka sita ashindwe kutambua kipaji cha mtoto (tuwatumiee walimu) baadae vipaji viendelezwe kama n mchezo wa mpira basi kijana apelekwe sehemu sahihi (academy) kama ni mbunifu basi aende sehemu sahihi hii itatusaidia kupunguza utegemezi na tatizo la ajira pia itaongeza utambuzi na maendeleoo kwa taifa.

Pia katika suala zima la ujifuzanji serikalia iandaee vifaa kuendana na wakati mfano katika uhandisi vifaa haviendani na usasa ndo maana unaona tenda nyingi za ujenzi wa madaraja au barabara wahandisi wanatoka nje ya nchi haf wa kwetu wanakuwa kama vibarua au basi hiyo ikishindikana tuwe na hatua ya kupeleka baadhi ya vijana wetu nje ya nchi kwenda kujifunza ambapo serikali itagharamia.

Pia shule nyingi bado zina changamoto ya miundombinu kama madarasa, nyumba za walimu, maabara na vifaa vya kufundishiaa na ujifuzanji kwa hiyo serikali iajiri walimu angalau kuwe na uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi hamsini pia nashauri angalau kila shule ya kata iwe na chumba kimoja cha kompyuta ili kujifunza tehama kuendana na wakati pia nashauri kutolewa kwa kikokotoo maana kinavunja moyo ufanisi kwa walimu na kuwepo kwa utolewaji wa elimu hafifu, kutafuta mbadala wa adhabu ya viboko na ningependaa adhabu itolewe ya kitaaluma zaidi pia suala zima la mtoto kupata mimba hafu akijifungua anarudi shule wakati aliyemupa mimba kama nae alikuwa ni mwanafunzi yupo jela anatumikia kifungo cha miaka thelathini hapana siioni hamsini kwa hamsini(50/50) kama atarudi shule basi na mtoto wa kiume arudi yaani wasubiliane kama hatarudi shule basi kijana wa kiume aendelee kukitumikia kifungo cha miaka thelathini.

SIASA: Pia katika TANZANIA tuitakayo kwenye siasa tunahitaji tume huru ya uchaguzi sio tu kwa jina bali kwa vitendo mfano RAIS wa nchi asishiriki kuteua kamati ya tume huru ya uchaguzi tuhitaji kiwe chombo kinachojiendesha chenyewe pia baadhi ya nyazifa kama mkurugenzi wa wilaya, halmashauri watu waombe kama ajira na sio kuteuliwa na RAIS pia ukuu wa wilaya, ukuu wa mkoa watu wagombee kama wanavyofanya wabunge ili apatikani kiongozi anaejua eneo vizuri pia kupunguza rushwa,undugu na kuongeza ufanisi wa kazi na hii inapunguza makosa mfano mtu anaweza kuwa mkuu kitengo fulani akakosea huko kwa kuharibu mali za wananchi kwa sababu yupo karibu na RAIS anahamishwa kitengo pia kupunguza hela wanazopokea mke wa RAIS hizo 60% hadi 20% ili hela ziende kwingine kwa wananchi masikini na pia sio sahihi kiongozi mkuu wa nchi kuendelea kulipwa baada ya kutoka madarakani wakati alikuwa analipwa wakati anafanyaa kazi pia anamafao URAIS ni kazi kama kazi zingine atumie mafao yake.

NISHATI NA TEKNOLOJIA: Pia katika suala zima la nishati bado ni changamoto nashauri kuwepo na shirika mbadala kulisaidia shirika la tanesco katika kusambaza umeme mfano kwa sasa wanasema umeme ni mwingi kuliko mahitaji lakin bado umeme unakatika sasa sijui shida nini pia serikali ifanye subside kwenye shirika ili kupunguza gharama ya upatikanaji wa umeme ili hata mwananchi wa hali ya chini apate umeme pia nashauri serikali kufanya utafiti kabla haijaanzisha miradi ya umeme mfano bwawa la mwl nyerere maji yamezidi ikabidi milango minne kati ya tisa ya bwawa hilo kufunguliwa ambapo matokeo yake ni mafuriko huko rufiji na athari nyingi pia nashauri serikali kugharamikia vijana baadhi wakajifunze kuhusu teknolojia nje ya nchi kama china, urusi na marekani ili uchimbaji madini tufanye wenyeji hii itasaidia kuongeza utoaji kuliko uingizaji wa bidhaa maana kwa sasa 98% ya migodi ipo chini ya wawekezaji kutoka nje ya nchi hafu sisi vibarua wa kawaida.

HABARI NA MAWASILIANO: Pia kwa sasa vyombo vingi vya habari vimekuwa chawa kwa serikali havitaki kuibua matatizo yanayowakumbuka wananchi masikini kila kukicha ni kusifia serikali hata kama hakuna cha maana kilichofanyika sidhani kama waandishi wa habari wanahitaji elimu ya kazi zao lakin wanahitaji elimu ya kizalendo wajue kulitumikia taifa mfano wakati wa uchaguzi tuhitaji vyombo vya habari visimame imara kuujulisha na kuielimisha jamii na sio kuwa machawa cha chama fulani pia kwa sasa kuna uingizaji wa simu fake duuuu idara ya mawasilianoo waipambaniee.

KILIMO NA UFUGAJI: Najua asilimia kubwa ya viongozi wa serikali si wakulima na kama ni wakulima basi wanaweka wafanyakazi hawaijui adha wanayopitia wakulima, mfano mwaka jana mkoani njombe watu wanauzia mbolea iliyojaa mchanga na serikali ipo, bei haileweki sokoni nashauri serikali itoee elimu kuhusiana na kilimo kuna hawa maafisa kilimo waajiriwe wasambazwe vijijini kumbuka kilimo ndo sekta mama pia kuanzisha kilimo cha umwagiliaje kwa maeneoo yenye changamoto ya mabadiliko ya halia ya hewa .

N.B mtu mtaani akiiba hata kuku anapigwa hadi kufa lakini ripoti ya CAG inakuja na wezi wanabainishwa lakini hakuna hatua yoyote inayochukuliwa hakuna haja sasa ya kuwa na CAG mtu akitenda kosa sheria zipo wazi zifatwe lakin kama hakuna ufatiliaji hakuna haja ya kuwa na CAG ni bora hela anazolipwa CAG zipelekwe kwa watu masikini pia kama kuna muungano hakuna haja ya mtanzania kutoka bara kuwa na passport size ili aingie Zanzibar.
 
mtoto kupata mimba hafu akijifungua anarudi shule wakati aliyemupa mimba kama nae alikuwa ni mwanafunzi yupo jela anatumikia kifungo cha miaka thelathini hapana siioni hamsini kwa hamsini(50/50) kama atarudi shule basi na mtoto wa kiume arudi yaani wasubiliane kama hatarudi shule basi kijana wa kiume aendelee kukitumikia kifungo cha miaka thelathini.
Tunataka haki, si vinginevyo asiangaliwe mtu jinsia ndio tuone adhabu. La. Kama haimfai huyu na yule haimfai sio sawa. Tunataka HAKI itawale.


SIASA: Pia katika TANZANIA tuitakayo kwenye siasa tunahitaji tume huru ya uchaguzi sio tu kwa jina bali kwa vitendo mfano RAIS wa nchi asishiriki kuteua kamati ya tume huru ya uchaguzi tuhitaji kiwe chombo kinachojiendesha chenyewe pia baadhi ya nyazifa kama mkurugenzi wa wilaya, halmashauri watu waombe kama ajira na sio kuteuliwa na RAIS pia ukuu wa wilaya, ukuu wa mkoa watu wagombee kama wanavyofanya wabunge ili apatikani kiongozi anaejua eneo vizuri pia kupunguza rushwa,undugu na kuongeza ufanisi wa kazi na hii inapunguza makosa mfano mtu anaweza kuwa mkuu kitengo fulani akakosea huko kwa kuharibu mali za wananchi kwa sababu yupo karibu na RAIS anahamishwa kitengo pia kupunguza hela wanazopokea mke wa RAIS hizo 60% hadi 20% ili hela ziende kwingine kwa wananchi masikini na pia sio sahihi kiongozi mkuu wa nchi kuendelea kulipwa baada ya kutoka madarakani wakati alikuwa analipwa wakati anafanyaa kazi pia anamafao URAIS ni kazi kama kazi zingine atumie mafao yake.
Kila mmoja apate stahiki zake wakati akitimiza wajibu wake..... rahisi tu.


HABARI NA MAWASILIANO: Pia kwa sasa vyombo vingi vya habari vimekuwa chawa kwa serikali havitaki kuibua matatizo yanayowakumbuka wananchi masikini kila kukicha ni kusifia serikali hata kama hakuna cha maana kilichofanyika sidhani kama waandishi wa habari wanahitaji elimu ya kazi zao
Hapa umejumuisha mambo ambayo hayana utafiti kuyathibitisha.

Japo ninakubali vyombo vya habari na burudani vyooote vinapaswa kuwa na ajenda na falsafa ya kitaifa✔
ripoti ya CAG inakuja na wezi wanabainishwa lakini hakuna hatua yoyote inayochukuliwa hakuna haja sasa ya kuwa na CAG mtu akitenda kosa sheria zipo wazi zifatwe lakin kama hakuna ufatiliaji hakuna haja ya kuwa na CAG ni bora hela anazolipwa CAG
CAG ijitahidi tu kufanya mambo yake kama makala zaidi kuliko habari. Yaani ziwe ni docunentaries kuliko breaking news maana tunapaswa kuelewa muenendo wa mafungu ya serikali na sio kushitushwa na habari zake kama nchi
 
Back
Top Bottom