Tanzania moja bei ya sukari toka Sh. 1,700 hadi 2,500

Ehud

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
2,685
337
Gazeti la serikali la Daily News la leo lina habari kuwa bei ya sukari nchini itapanda zaidi hadi kufikia kati ya Tshs 2500/- Tshs 3000/- kwa kilo moja. Habari hizi mbaya zinakuja wakati tayari vitu vingine muhimu kama umeme,maji,chimvi na nauli vikipanda bei kwa kasi ya ajabu! Tufika kweli namna hii!

Daily News | Sour news as sugar prices soar
 
Gazeti la serikali la Daily News la leo lina habari kuwa bei ya sukari nchini itapanda zaidi hadi kufikia kati ya Tshs 2500/- Tshs 3000/- kwa kilo moja. Habari hizi mbaya zinakuja wakati tayari vitu vingine muhimu kama umeme,maji,chimvi na nauli vikipanda bei kwa kasi ya ajabu! Tufika kweli namna hii!

Daily News | Sour news as sugar prices soar

Watanzania tunatakiwa tutume ujumbe nchini Zambia kwenda kuwauliza raia wao sembe ikipanda bei huwa wanafanya nini kuzuia nyongeza hiyo. Napendekeza kiongozi wa msafara awe Nicholas Mgaya
 
Napenda kutoa taarifa kwamba sukari imepotea mjini Arusha/Moshi ila sijui maeneo mengine. Ukitaka kununua mfuko wa sukari lazima uwe unajuana na wahindi wenye maduka ( Arusha sundries, Dalia, Ataula etc) na pia hata kama unajuana nao hauwezi kuuziwa zaidi ya mifuko mitano. Bei pia ime shoot toka shs62,000 mpaka 80,000.

Naona tunarudi zile enzi za mwaka 1984.
 
Asante sana mkubwa, inaonekana we mwenzangu unatumia sugar sachets so you are not a victim.
 
Muda wa kutumia Asali umefika.hata hivyo asali ni bora zaidi ya sukari.mimi nilisha acha kutumia sukari kila siku
 
Poleni sana wapendwa wetu wa `A` city, jana nilikuwa dodoma nao pia ni vivyo, sijui shida ni nini? wenzetu mnaojuwa sababu tupeni taarifa, nilikuwa najiuliza kwamba wakuu wa nchi wanajuwa hali hii? na wanasema nini?
 
:embarrassed::embarrassed::embarrassed:Mambo ya JK naona tunarudi enzi za maduka ya kaya kila kitu kinauzwa kwa idadi kamili siyo uwezo wa kununua
 
Baadhi ya wakazi wa vijiji vilivyopo kando kando ya Ziwa Nyasa, Wilaya mpya ya Nyasa mkoani Ruvuma, wameiomba serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara kuona umuhimu wa kuwaruhusu wafanyabiashara wa hapa nchini kununua sukari nchini Malawi na kuingiza kuuza nchini.
Wamesema lengo la ombi hilo ni kupunguza tatizo la uhaba wa sukari ambao umesababisha bei ya bidhaa hiyo kupanda kati ya Sh. 2,000 na 2,500 kwa kilo katika vijiji vyao.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na NIPASHE, baadhi ya wakazi wa vijiji vya Kilosa, Ndengere, Chinula, Zambia, Lundo na Liuli, walisema kutokana na sukari ya Tanzania kutopatikana katika maeneo yao, hulazimika kutumia sukari ya kutoka Malawi ambayo huingizwa nchini na wafanyabiashara kwa njia za panya na kusababisha kuuzwa kwa bei kubwa.
Hamis Yusuf, mkazi wa kijiji cha Kilosa, alisema kwa muda mrefu sukari wanayoitumia kijijini kwao hutoka nchini Malawi ambayo kilo moja huuzwa kati ya Sh. 2,000 na Sh. 2,500 wakati serikali hivi karibuni iliagiza bidhaa hiyo iuzwe kwa bei ya Sh. 1,700 kwa kilo moja.
Rehema Challe, mkazi wa mji mdogo wa Mbamba bay, alisema kama mipaka ingeruhusu kuvusha sukari kutoka Malawi, basi bei ya bidhaa hiyo ingeuzwa kati ya Sh. 1,200 na 1,500 kwa kilo moja.
Challe alisema sukari ya Tanzania katika mji mdogo wa Mbamba bay haijawahi kuletwa kwa muda mrefu wala kuonekana na kuimba serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, ichukue uamuzi wa haraka wa kutoa vibali vya kusafirisha bidhaa hiyo kutoka nchini Malawi ili kupunguza kero inayowakabili wakazi wa maeneo ya mwambao mwa Ziwa Nyasa.
Naye John Katumbi, mkazi wa kijiji cha Ndengere, alieleza kuwa sukari imekuwa ikiadimika sana hasa kati ya Desemba na Aprili ambayo ndiyo kipindi cha Kiwanda cha Sukari nchini Malawi kusafisha mashamba ya miwa na kukifanyia ukarabati.
Alisema kutokana na hali hiyo, kiwanda hicho husimamisha uzalishaji wa sukari na kusababisha uhaba mkubwa wa sukari katika vijiji vilivyopo kando kando ya Ziwa Nyasa.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mbamba bay, Fidelis Duwe, alipohojiwa na NIPASHE kuhusiana na kero inayowakabili wakazi wa vijiji hivyo, altihibitisha kuwa sukari huuzwa kwa bei kubwa kutokana na wafanyabiashara kuipata kwa njia zisizo za halali.
Hata hivyo, alisema iwapo sukari hiyo ingeruhusiwa kuingiZwa nchini kwa njia halali, bila shaka itauzwa kwa bei ya chini.
Alisema nafuu hupatikana pale meli ya MV Songea inapofika Mbamba bay ikitokea Itungi Kyela mkoani Mbeya na kuelekea Nkata Bay nchini Malawi.
Alisema meli hiyo hufika Mbamba bay mara mbili kwa mwezi.
Alieleza kuwa wakazi wa kijiji hicho kwa muda wote hutumia sukari ya kutoka nchini Malawi ambayo pia huuzwa kwa bei kubwa.
Baadhi ya wafanyabiashara wa mji mdogo wa Mbamba bay ambao waliomba majina yao yasitahwe, waliiambia NIPASHE kuwa sukari ya kutoka Malawi huletwa Mbamba bay kwa kutumia boti kuwakwepa maafisa forodha wa Mamlaka ya Kodi nchini (TRA).
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Kanali Mstaafu Edmund Mjengwa, alithibitisha sukari kuuzwa kwa bei kubwa lakini akasisitiza kwamba jambohilo linafanyiwa kazi.
Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba, alisema kilio hicho cha wananchi cha kuuziwa sukari kwa bei kubwa ni cha muda mrefu lakini tayari alifanyia kazi kwa kuwasiliana na Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye wakati wowote atatoa majibu ambayo yatakuwa ni faraja kwa wakazi wa vijiji vilivyopo kando kando ya Ziwa Nyasa.
SOURCE: NIPASHE Ghala ya sukari
 

Attachments

  • sukari(2).jpg
    sukari(2).jpg
    16.6 KB · Views: 48
Inavyoonekana VIONGOZI WENYE DHAMAN NA HILI wameshindwa kulisimamia vyema . hali kama hii inaendelea kulalamikiwa na wapiga kura kisha wao wanaendelea na semina na kugawana posho tu. wakiwa majukwaani utawakuta wakaliiii kukemea hali hii, wengine waliisha tao na hukumu ATAKLAYE KAMATWA AKIUZA SUKARI ZAIDI YA tsh 1700/= ATAKIONA CHA MTEMA KUNI. sheria zipo zinakosa wasimamizi. lakini jambo la kusikitisha uchaguzi ukikaribia hizi kero hutozisikia ingawa nina hakika maisha yatakuwa juu zaidi ya leo. ni jukumu letu sisis wananchi badala ya kulalamika sasa nadhani tuwakamate wenyewe wauzaji na kuwapeleka ktk vyombo husika hiki CHAMA CHA MAGAMBA wamechanganyikiwa hawaelewi lipi waanze lipi lifuatie.
 
Nimepata taarifa kuwa bei ya sukari imeendelea kupaa huko kanda ya ziwa

je wabunge wapige mkwara kama issue ya mafuta?
 
KANA KWAMBA AWAJATOSHEKA NA MGAO WA UMEME SERIKALI YA TANZANIA IKAHAMIA MGAO WA MAFUTA YA PETROL
NA DIESEL NA SASA WAMERUDI NAMMGAO WA SUKARI JIHADHARI KAMA UNA KIASI KIDOGO SUKARI INAENDA KUUZWA ALFU 2 NA 500 MPAKA
ALFU TATU WENI NDUGU WA KARIBU MTAARIFU NAMWENZAKO
IMG_0758.jpg
 
Tukitoka hapo tunafuatia na mgao wa nini tena?
Nataka nijiandae nao pia
 
Tukitoka hapo tunafuatia na mgao wa nini tena?
Nataka nijiandae nao pia


Unafuata mgao wa Kitimoto. Wale wapenda kitimoto wanunue cha kutosha wahifadhi kwenye mafridge yao au wakaushe kwa moshi!
 
Kama bado upo upo kuna uwezekano kinachofwata mgao wa akuingiza ile mipira yetu
sishauri usitumie lakini sipendi uiache akili kichwa chako
 
Back
Top Bottom