Kinadharia, Tanzania ina mihimili mitatu ya utawala, SERIKALI, BUNGE NA MAHAKAMA.
Kuanzia awamu ya 5, kimamlaka, mihimili yote mitatu imekufa, umezaliwa mhimili mmoja tu, wa RAIS.
Ndiyo maana unasikia Rais ametoa hela, Rais ameiagiza mahakama, Rais amilikemea bunge.
Ukiona kuna mradi mzuri umejengwa kuwahudumia wananchi, ujue ni Rais.
Ukiona watu wasio na hatia wanapigwa virungu, ujue ni Rais.
Ukiona watu wanafutiwa kesi za kubambikiziwa, uje ni Rais.
Ukiona watu wanabambikiziwa kesi na kusoteshwa mahabusu, ujue ni Rais.
Ukiona viongozi wakubwa au wanafungwe au kusoteshwa mahabusu, ujue ni Rais.
Uhuru wa mahakama umeachwa kwa wezi wa kuku, vitunguu na nyanya.
Uhuru wa Bunge, umeachwa katika kuipongeza Serikali tu!
Rais aliagiza akina Rugemarila, wakae ndani, wakaa ndani. Rais mwinhine akaagiza akina Rugemarilla watolewe, wakatolewa. Kama tungekuwa na mahakama, Rugemarilla na wenzake ama wasingesoteshwa mahabusu, au kama wangekuwa wana kesi, basi wasingetolewa kwa vile tu Rais amebadilika.
Kwa sasa hakuna linalofanyika, liwe jema au baya, bila hiari ya Rais. Na juzi jaji mkuu akakazia kuwa majaji wanapotoa hukumu wasiangalie tu sheria inasema nini bali waangalie pia mahitaji ya mihimili mingine, na kwa vile mihimili yote practically imekufa, alimaanisha majaji waangalie Rais anataka nini.
Mbowe atafungwa au kuachiwa, kutegemea Rais, kama mhimili, atataka nini. Majaji na mahakimu wamekuwa visemeo tu vya mhimili mpya, wa RAIS.
Taifa lipo kwenye hali ngumu sana kwa sababu lipo kwenye maamuzi ya mtu mmoja ambaye kikatiba wala siyo miongoni mwa ile mihimili mitatu, yeye ni kiongozi tu wa mhimili mmoja.
Tupiganie tupate katiba mpya au tuishi kama mbwa au paka anayependwa au kuchukiwa na bwana wake.
Umenena vema MKUU.
Hii nchi inabidi tukubaliane UPYA namna gani tunapswa iendeshwe.
Hi mihimili tuipange UPYA kila mmoja ukae kwa Heshima katika nafasi yake pasipo kuingilia mhimili mwingine.
MIHIMILI ITENGANE NA IONEKANE KUWA IMETENGANA.
Kwa sababu hiyo TUNAHITAJI KATIBA MPYA!