Tanzania: Mhariri wa gazeti lililofungiwa Simon Mkina, atishiwa maisha

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,721
2,000
94443397e1acc7d67df5790ea3c74ce8.jpg


Simon Martha Mkina

Mhariri mkuu wa gazeti moja la Tanzania lililofungiwa na Serikali juma lililopita baada ya kuchapisha habari iliyowahusisha maraisi wa zamani kwenye sakata la mikataba ya madini, amesema toka wakati huo amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka kwa watu wasiofahamika.

Wizara ya habari nchini Tanzania tarehe 14 ya mwezi wa 6 ilitangaza kulifungia gazeti la kila wiki la MAWIO kwa muda wa miaka 2 kutokana na hatua yake ya mara kwa mara kuandika habari zinazoikosoa Serikali, ambapo liliandika habari iliyowataja maraisi wastaafu Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete kuhusika kwenye mikataba ya madini.

Uchunguzi wa hivi karibuni ulioagizwa na rais John Pombe Magufuli, umekadiria kuwa kiasi cha dola za Marekani bilioni 84 ambazo ni tozo za kodi zilipotea kutokana na makampuni hayo ya uchimbaji madini yaliyoanza toka mwaka 1998 kukwepa kodi lakini uchunguzi huu haukuwataja popote maraisi hao.

Licha ya onyo lililotolewa na rais Magufuli, gazeti la MAWIO lilichapihs amaoni yaliyotolewa na mbunge wa upinzani Tundu Lissu, ambaye aliliambia bunge kuwa rais Kikwete na rais Mkapa wanahusika pakubwa na utata wa mikataba iliyotiwa saini katika kipindi cha mwaka 1995 hadi 2005 na 2005 hadi 2015 na kwamba walipaswa kuhojiwa na kamati zilizoundwa na rais.

Simon Mkina mhariri wa gazeti hilo ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP kuwa amekuwa akipokea vitisho vya simu kutoka kwa watu wasiofahamika toka gazeti lao lilipofungiwa.

“Baada ya gazeti kufungiwa, nimepokea takribani simu tatu za vitisho kwa maisha yangu. Niliuliza ninani aliyenipigia lakini alinikatia simu.

“Simu nilizopigia hazikuonesha namba. Kwahivyo nilishindwa kumpigia huyo mtu tena,” alisema muhariri huyo.

Mkina amesema kuwa tayari ametoa taarifa kwa bodi ya gazeti hilo pamoja na jeshi la Polisi ambalo limemjibu kuwa itakuwa vigumu kufanya uchunguzi kwakuwa simu zenyewe hazikuwa na namba.

Timu ya wachunguzi iliyoundwa na rais ilibaini kuwa hasara ambayo Serikali ya Tanzania imeipta ilitokana na makampuni ya kigeni yanayofanya kazi ya uchimbaji madini barani Afrika na amabayo ni ya nne kwa uzalishaji barani humu ilishindwa kutangaza faida miaka yote ya uchimbaji wake nchini Tanzania.

Rais Magufuli aliituhumu kampuni ya Barrick Gold kwa kuiibia nchi yake kupitia njia ya televisheni juma lililopita, lakini alikubali mjadala na mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo John Thornton aliyesafiri kutoka Canada kuja kuona na rais.

Gazeti hili tayari lilikuwa limeshawahi kukutana na zuo wakati wa uchaguzi mkuu uliopita visiwani Zanzibar lakini adhabu hiyo iliondolewa na mahakama.

Mkina amesema gazeti lao limepanga kwenda mahakamani kupinga hatua ya Serikali kulifungua gazeti lao.

Chanzo: RFI
 

chuwaalbert

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
3,599
2,000
Mhariri mkuu wa gazeti moja la Tanzania lililofungiwa na Serikali juma lililopita baada ya kuchapisha habari iliyowahusisha maraisi wa zamani kwenye sakata la mikataba ya madini, amesema toka wakati huo amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka kwa watu wasiofahamika.
Kama haya ni kweli basi demokrasia Tanzania inaelekea MACHWEO....
 

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
16,373
2,000
Kubenea hana tena credibility ya kuzungumzia ufisadi ....hiki kichaka cha upinzani kinatumika vibaya sana .....kutishiwa maisha ni kitu kibaya lakini wametengeneza mazingira ya kutoaminika hata kwenye issues za msingi ....
 

KANYAMA

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
1,008
2,000
Aseme tu nae kama anataka kujiteka kama Ben saa 9..Image ya Demokrasia ya Tanzania kimataifa haiwezi kuharibiwa na wahariri wapumbafu kama hawa wenye kuvunja katiba kwa kutaka kuwadhalilisha wazee wetu huku wakiyakumbatia madude ya mafisadi waliyonayo.
 

MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,933
2,000
Kubenea hana tena credibility ya kuzungumzia ufisadi ....hiki kichaka cha upinzani kinatumika vibaya sana .....kutishiwa maisha ni kitu kibaya lakini wametengeneza mazingira ya kutoaminika hata kwenye issues za msingi ....
Kuwa wazi sasa, wewe uko upande upi kwa sasa? waoneaji au waonewaji?
 

Ntolonyonyo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,191
2,000
Kama ni kweli kuna vitisho..sio kitu kizuri na hao watu wanaotisha wenzao wakome wanatuaribia nchi yetu na demokrasia yetu
 

sibusiso dlomo

JF-Expert Member
Apr 23, 2016
681
500
Kubenea hana tena credibility ya kuzungumzia ufisadi ....hiki kichaka cha upinzani kinatumika vibaya sana .....kutishiwa maisha ni kitu kibaya lakini wametengeneza mazingira ya kutoaminika hata kwenye issues za msingi ....
Kama ipi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom