Tanzania mgombea Urais huru inawezekana kama ilivyowezekana Rwanda. Tujitafakari!

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
20,208
31,844
Salaam, Shalom!

KATIBA yetu ya nchi IPO wazi kabisa kuwa, HAKI ya kuchagua inaenda sambamba na HAKI ya kuchaguliwa.

Yaani HAKI ya mgombea nafasi yeyote katika ngazi yeyote kisiasa, haipasi kuminywa ndani ya vyama vya siasa pekee.

Jambo hili la kuminya HAKI ya kuchaguliwa, ndio hasa kitu kinachokwamisha watu makini kushindwa kuanzisha vyama vya siasa Kwa haraka, tumeona vyama kadhaa vikijaribu kupata usajili wasiweze.

Tumeshuhudia Rwanda Nchi inayopigiwa kelele kuminya DEMOKRASIA ikifanikiwa kuruhusu Mgombea binafsi katika nafasi ya Urais. Hii ni hatua kubwa tupasayo kujifunza.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
 
Mgombea binafsi hatokuwa rahisi kununuliwa au kuwa mtu wa system, kwahio atakuwa tashio kubwa kwa watawala.

Vyama vya Tanzania ni tawi la ccm lenye jina tofauti tu.
 
Mgombea binafsi hatokuwa rahisi kununuliwa au kuwa mtu wa system, kwahio atakuwa tashio kubwa kwa watawala.

Vyama vya Tanzania ni tawi la ccm lenye jina tofauti tu.
Hiki kitu kipo kikatiba,

Mgombea huru apewe nafasi katika ngazi zote za uongozi,

Njia Gani atapata pesa na ufadhili ,wananchi wataamua.
 
Back
Top Bottom