Tanzania: Leteni mastaa wa soka wainue soka letu

Big Dady

Member
Nov 10, 2009
59
2
Baadhi ya nchi zimewahi kutumia wachezaji wa kigeni kuinua soka lao. Nina mifano ya Pele wa Brazili, aliwahi kucheza mpira Marekani wakati anaelekea kustaafu, lengo la nchi hiyo ilikuwa ni kuleta chachu na hamasa kwa wachezaji wa ndani ili kuupenda zaidi mpira. Na kweli hiyo ilisaidia sana kuinua kiwango cha mpira Marekani, nchi inayotamba zaidi kwa mchezo wa basketball.

Wajapani waliwahi kumwajiri Zito kwa lengo hilo hilo. Hapa nyumbani mfano ni timu ya majimaji ambayo iliwahi kumwajiri Abdala Kibadeni, na kweli hali ya mpira kwa timu ilipanda sana kiasi cha kuwa tishio nchi nzima.

Sasa kwa nini nchi yetu isiige mbinu hizo kwa kuwaleta wachezaji wakongwe na waliowahi kutisha kwa soka hapa Afrika kama vile Austin 'Jay Jay' Okocha, Daniel Amokachi, Lukas Radebe, Kalusha Bwalya, n.k. ili kuongeza hamasa kwa wachezaji wetu. Niliwataja hapo juu labda wameshastaafu kabisa, lakini naamini wapo wengine wa aina yao wanaoweza kuleta hamasa kwa wachezaji wetu.

Tutaendelea kwa WASHANGILIAJI WA KIMATAIFA hadi lini. Maana wakati nchi za wenzetu wanajiandaa kupambana kwenye Kombe la Dunia, sisi tunajinadaa kuwa WASHANGILIAJI WA KIMATAIFA. HII HALI HADI LINI?
 
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=e6pfwAJT91w[/ame] tutaishia kucheza taarabu kama watoto wa kiislamu wafanyavyo mara baada kuhitimu mafunzo ya madrasa
 
Hizi chuki zako zinahusiana vipi na hii mada ?

¬K

MSamehe kwani namfahamu huyu jamaa ana mtindio wa akili,tumpeleke mirembe kule dodoma akatibiwe.Mie nitatoa usafiri wa kumpeleka na kumrudisha pindi atapotoka!
 
Back
Top Bottom