Tanzania Labour Law (Sheria ya Kazi Tanzania)

Buswelu

JF-Expert Member
Aug 16, 2007
1,998
351
Mkataba wa ajira, kama ilivyo desturi kwa mikataba mingine kwa mujibu wa sheria, huzaliwa, huishi na kufa; kama ilivyo kwa binadamu na viumbe hai vingine.

Unazaliwa mara baada ya mwajiriwa na mwajiri kutia saini zao. Hapo ndipo wanapouanzisha, utekelezaji wake unapoanza kuchukua hatua na kifo ni pale tu yanapoanza kujitokeza baadhi ya mambo au masuala yanayoainishwa na sheria.

Aidha, zipo taratibu maalum za kumaliza au kuua mkataba wa ajira na hii ni katika mazingira yote, iwe kwa hiari na yale ya kumaliza kwa kulazimika kulingana na sababu mbalimbali.
Kumalizika au kukoma mkataba wa ajira kwa hiari au kufikia ukomo wa kazi kulingana na wepesi wa kutekeleza majukumu ya kazi yenyewe.

Kanuni ya 4 (1)-(7) na ya 5 (1)-(5), zote ni Kanuni za Ajira na Mahusiano Kazini, Kanuni za Utendaji Bora za Mwaka 2007, zinaeleza hakuna shida kama ilivyo kumaliza, kukoma mkataba wa ajira kwa kulazimika kutokana na sababu mbalimbali za kinidhamu.

Katika uhusiano kazini, jambo mojawapo linalomfukuza mtu kazi au kusababisha kukoma mkataba wa ajira, ni utovu wa nidhamu. Hiyo ni mojawapo, kati ya sababu za msingi zinazoweza kumfanya mwajiriwa au mfanyakazi kupoteza ajira yake.

Kimsingi, kanuni hizo zinaelekeza kuwa ni sahihi kumfukuza mfanyakazi kwa sababu za kinidhamu, lakini haimaanishi kuwa mwajiri amtafutie mwajiriwa kisa cha kuzusha au kupika, ili kumwondoa kazini.
Kinachosisitizwa hapa, ni lazima sababu hizo ziwe zimejitokeza na kuthibitika kweli na ziweze kuthibitishwa pale itakapotakiwa kufanyika hivyo.

Ujenzi wa hoja kwa kushikilia mkazo kuwa nilisikia au nahisi, zitasababisha tuhuma hizo kukosa mashiko mbele ya msuluhishi, hakimu au jaji kutegemeana na shauri lilikofika.

Kanuni ya 8 (1)(d) na 12 (1)-(5), zote za Ajira na Uhusiano Kazini na Kanuni za Utendaji Bora za mwaka 2007, sanjari na Kifungu cha 37 (2), Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini, 2004 Sura ya 366, zote zinasisitiza ukweli na uthibitisho wa madai yanayotolewa.

Angalizo ni kwamba, sheria inaelekeza kuwa mwajiriwa au mfanyakazi, atafukuzwa kazi mara moja, bila ya hata kupatiwa barua ya onyo kwa kosa la mara ya kwanza au “summary dismissal”.

Kwa utaratibu huo, imafanya mwajiriwa, au mfanyakazi kupoteza haki zake zote za msingi kama kiinua mgongo. Kifungu cha 42 (1)-(4) cha Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini ya mwaka 2004 Sura ya 366 inalifafanua hilo.

Hivyo basi, ni kosa kwa mwajiri kumfukuza mfanyakazi kwa utaratibu wa mara moja, yaani ‘summary dismissal, isipokuwa kama hilo litafanyika katika mazingira ambayo sheria inaruhusu wazi kufanya hivyo na siyo kinyume chake.
Kifungu cha 41 (1)-(7) cha Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini ya 2004 sura ya 366 ina ufafanuzi.

Haki ya Kusikilizwa
Kila mtu ana haki ya kusikilizwa, kabla hatua ya kisheria kuchukuliwa. Ni haki ya asili, ambayo haiwezi kuondolewa na mtu au mamlaka yoyote ile. Kwa maana hiyo, pasipo kujali ukubwa wa kosa, hata kama kosa la mwajiriwa, mhusika anapaswa kupewa nafasi ya kutoa utetezi wake.

Atajitetea na kutakiwa kuwasilisha utetezi wake, dhidi ya: “Kwanini asichukuliwe hatua za kinidhamu?” Kanuni ya 13 (1)-(13) Kanuni za Ajira na Uhusiano Kazini, 2007 inaeleza.

Ni kosa kwa mwajiri au mkuu wa kazi kumfukuza mfanyakazi, bila ya kumpatia nafasi ya kumsikiliza au kujitetea. Hii siyo hiari ya mwajiri kuamua kumpatia mwajiriwa haki husika, bali ni haki ya msingi. Hiyo ni kwa sababu, haki yenyewe ipo kwa mujibu wa sheria, hivyo utekelezaji wake ni lazima.

Haki ya Malipo Stahiki

Kifungu cha 44 (1)(a) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004, Sura ya 366, kinaelekeza haki za msingi alizo nazo mwajiriwa atakayefukuzwa kazi, kutokana na sababu za kinidhamu. Hiyo ni pamoja na kulipwa mshahara au ujira wake.

Mshahara utalipwa kwa kuzingatia tarehe ya mshahara wa mwisho mpaka siku ambayo mwajiriwa amefukuzwa, mathalan kama tarehe ya mwisho ya kupokea mshahara itakuwa Juni 30, 2019, kisha mhusika atafukuzwa Julai 17, 2019; pesa itakayotolewa ni kwa kuzingatia siku ambazo mhusika amefanyakazi. Yaani jumla ya siku 17 kuanzia tarehe 1 hadi 17 Julai. Inatajwa kuwa haki ya msingi, wala isipuuzwe kulinda maslahi ya pande zote mbili.

Ingia hapa ujisomee sheria ya ajira na mahusiano kazini

Sheria ya ajira na mahusiano kazini

==============

Michango ya wadau

Stahiki baada ya mkataba kuisha ama kukatishwa

1.Maana

¨Hizi ni stahiki azipatazo mwajiriwa kutokana na mkataba wake wa ajira kukatishwa na mwajiri. Stahiki hizi hulipwa na mwajiri.

¨Aidha, kipengele cha 44 cha Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini Namba 6 ya mwaka 2004 inampa mwajiriwa haki ya kulipwa stahiki mbalimbali pindi mkataba wake wa kazi unapokatishwa.

2. Aina za Stahiki
  • Malipo ya kazi yote aliyoifanya mwajiriwa kabla ya mkataba wake wa kazi kukatishwa.
  • Malipo kwa likizo yake ya mwaka ambayo atakuwa hajaenda kabla ya mkataba kukatishwa.
  • Malipo kwa likizo za mwaka zilizolimbikizwa. Hii inamaanisha katika kipindi chote cha mkataba kama kuna likizo ambazo mwajiriwa alikuwa hajachukua, basi atastahili kulipwa sawa sawa na idadi ya siku hizo.
  • Malipo yatokanayo na kukatisha mkataba pasipo kutoa/kutanguliwa na notisi. (Notice pay due). Hii ina maana kuwa, badala ya mwajiri kutoa notisi ya kukatisha mkataba kwa mwajiriwa, basi mwajiri anaweza kuamua kumlipa mwajiriwa malipo kiasi ambacho ni sawa sawa na kile ambacho mwajiriwa angekuwa anapata katika kipindi hicho cha muda wa notisi.
  • Kiinua mgongo (severance pay), kama tu mwajiriwa ametimiza vigezo vya kulipwa kiinua mgongo. (S.42, ELRA, 2004)
  • Gharama za usafiri kutoka eneo la mwajiri. Hii ni endapo mwajiriwa wanaachana na mwajiri katika sehemu ya kazi eneo tofauti na alipoajiriwa awali. Kwa mfano Mr. John anaajiriwa na kampuni A ambayo iko Dodoma, halafu baada ya muda akahamishiwa ofisi za kampuni hiyo hiyo zilizopo Arusha, mkataba wake ukikatishwa basi mwajiri atalazimika kumlipa Mr.John gharama za usafiri na kujikimu safarini kurudi hadi eneo alikoanzia ajira yake hiyo Dodoma.
  • Hati ya kazi (Certificate of service). Hii ni hati anayopatiwa mwajiriwa anayeacha/anayeachishwa kazi kutambua mchango wa nguvukazi yake katika huduma/kazi ambayo amekuwa akiifanya katika muda wote wa ajira yake katika kampuni/taasisi husika. Hati ya kazi haitakiwi kueleza sababu za kuacha/kuachishwa kazi.
Baadhi ya stahiki hizi zinatolewa kulingana na vigezo mbalimbali kama;


Ø Sababu za kukatishwa mkataba (grounds of termination)

Ø Aina ya mkataba wa ajira (type of employment contract)

Ø Muda ambao mwajiriwa amehudumu katika huduma/ajira (the length of service to your employer)


3. Ufafanuzi wa Kiinua mgongo (severance pay)

Ufafanuzi wa kipengele cha kiinua mgongo kadiri ya Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini Namba 6 ya mwaka 2004, kifungu cha 42 kinaeleza kama ifuatavyo;

  • Kama mkataba wa ajira umekatishwa na mwajiri kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu ama ukiukwaji wa miiko ya kazi, basi mwajiri halazimiki kulipa kiinua mgongo.
  • Kama mkataba wa ajira umekatishwa kutokana na mahitaji mapya ya uendeshaji wa ofisi/kazi (termination on grounds of capacity or operational requirements), ama kutokana na uanzishwaji wa teknolojia mpya inayohitaji watu wenye utaalamu zaidi, na mwajiri ametoa ajira mbadala kwa watakaoathirika na mabadiliko hayo, lakini wafanyakazi wakaikataa hiyo ajira mbadala basi mwajiri anaweza kukataa kulipa kiinua mgongo.
  • Ni lazima mwajiriwa awe amehudumia katika ajira hiyo kwa muda usiopungua miezi 12 mfululizo ndipo atakidhi kigezo cha kupata kiinua mgongo. Aidha, lazima ukatishwaji huo wa mkataba uwe umesababishwa na mwajiri (termination initiated by employer)
4. Ukokotoaji wa kiinua mgongo

Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini Namba 6 ya mwaka 2004, kifungu cha 42 kimeendelea kueleza juu ya Ukokotoaji wa kiinua mgongo. Kiinua mgongo ni kiasi ambacho ni sawa sawa na kiwango cha mshahara wa siku saba (7) kwa kila mwaka mzima ambao mwajiriwa ametoa huduma pasipo kukatisha; lakini haivuki miaka kumi (10)


Hivyo; Kiinua mgongo = kiwango cha mshahara wa siku 7 zidisha kwa miaka ambayo mwajiriwa ametoa huduma kwa mwajiri katika muda usiozidi miaka 10.


Kima cha mshahara kwa mwezi x 7 x idadi ya miaka

26
(yaani kima cha chini cha mshahara wa sekta husika, kigawanye kwa 26 (yaani siku za kazi 26) kisha zidisha kwa siku 7 halafu zidisha tena kwa idadi ya miaka uliyokaa kazini (hapa weka miaka iliyokamilika tu....mfano umekaa kazini miaka miwili na miezi minne, hapa tunachukua miaka miwili tu iliyokamilika, hiyo miez kwa sababu haijatimia miezi 12 hatuichukui)

5. Gratuiti (gratuity)

Huu ni ukokotoaji wa kiinua mgongo kwa kadirio la asilimia, kadiri ya ongezeko la mshahara wa kila mwezi kulingana na makubaliano ya mwajiriwa na mwajiri.

¨Kwa mfano, mwajiri anayelipa gratuiti asilimia 5%, maana yake kila mshahara asilimia 5% inahesabika kwenye stahiki za mafao.

Ongezeko la gratuity kwa 5% kwa mwezi


April

Mei

Juni

Julai

Mshahara

140,000

150,000

200,000

300,000

Gratuity 5%

7,000

7,500

10,000

15,000


7,000 + 7,500 + 10,000 + 15,000 = 39,500

NB; Asilimia hiyo anatoa mwajiri tu. (haitatokana na makato kwa mwajiriwa)

Samahani kidogo hii chart ya kuonesha ukokotoaji wa kiinua mgongo kwa Gratuity haijaweza kuiarrange vizuri hapa lakini angalau mkisoma mnaweza kupata concept.

Mwajiriwa hatakuwa amekidhi kigezo cha kulipwa kiinua mgongo kama mkataba wa ajira utakatishwa akiwa hajakamilisha mwaka mmoja (miezi 12) tangu alipoajiriwa. Kwa wanaolipwa gratuiti ukokotoaji utafanyika kwa miezi yote ambayo mwajiriwa amefanya kazi.

NINAWASILISHA
----
Katika hali iliozoeleka Tanzania watu wengi hukimbilia kazi au ajira kabla ya kujifunza na kujua sheria za kazi nchini na kimataifa ILO. Watu wengi hukimbilia pia kusaini mikataba ya ajira bila kujua mkataba unasema nini kati ya muajiriwa na muajiri.

Hali hii imepelekea watu wengi sana kupoteza ajira kwa kushindwa kumudu kasi ya ajira yake na shughuli anapaswa kufanya kila siku na kuingia na kutoka

Wengine hushindwa kusema chochote wawapo kazini kwa kuogopa kufukuzwa kazi na muajiri wake.

Jambo hili hupelekea watu hao kufanya kazi chini ya kiwango cha kazi kwa kuogopa ajira zao kuwa hatarini.

Wafanyakazi wengi husoma sheria za kazi baada ya kufukuzwa na kutaka kujua sheria inasema nini baada ya kufukuzwa au kuacha kazi.

Katika hali hii kumekuwa na uzembe wa kuwajibika kwa kutojitambua na msimamo wa ajira zao.
----
Katika madai kweny hii sheria yetu ya ajira na mahusiano kazin Na6/2004 madai yote yanayohusu ajira kisheria isipite siku 60 uwe tayar umeshapeleka kweny chombo cha sheria hapa i mean TUME

sasa kama unamishahara ya miez mitatu maan yake unamdai juu ya mwajiri wako

Swari je
Ulishawah kumkumbusha mwajiri wako kuhusu mishahara yako?
Kama ndiyo ,njia gan ulitumia ?
1.kwa mdomo au
2.kwa maandishi?
Kama kwa mdomo na alikuwa anakupa kiswahili hata ukienda mbele ya tume itakuwa vigumu ww kupata haki zako maan kama hyo mishahara yko au hayo madai yako yatakuwa nje ya siku 60

Ila kama ulikuwa unakumbusha kwa maandishi unaweza kwenda fungua kesi na kudai mishahar yako hyo ya miez 3 sababu utakuwa n evidenC ya maandishi kwamba licha ya mwajiri wangu kumkumbusha kimaandish lakn hakuna kitu alivhokuwa anafany zaid ya calenda tuu


N:B
KAMA UKO CHAMA CHA WAFANYAKAZ NAOMBA NENDA OFIS HUSIKA YA CHAMA CHA WAFANYAKAZ ILI MWAJIR WAKO AANDIKIWE BARUA YA WITO NA CHAMA AJE AELEZE JUU YA UHALALI WA MALALAMIKO YAKO YA MISHAHARA MBELE YA CHAMA NA CHAMA CHAKO NDICO KITAKACHOKUPA MWONGOZO NN CHA KUFANYA KAMA MWAJIRI N KAIDI
HUMBLY SUBMITTING
----
Ndio, ukishatimiza mwaka mmoja unastahili kiinua mgongo manake hata ktk ukokotoaji wake ni lazima uwe umefanya kazi kwa mwajiri huyo sio chini ya miezi 12 (unless otherwise iwe kwamba mlikubaliana kulipana kiinua mgongo kwa ukokotoaji wa asilimia ya kila mwezi "Gratuity")

Lakini sasa ili ustahili kiinua mgongo nilichoelezewa hapo mwanzo ni lazima;
1. Usitishwaji wa ajira yako uwe umefanywa na mwajiri. (termination has been initiated by employer). Hii ina maana ukiacha kazi mwenyewe ama endapo mkataba umeisha/umefikia kikomo basi hautastahili kulipwa kiinua mgongo
2. Uwe umefanya kazi kwa mwajiri huyo mfululizo/hata kama sio mfuliluzo basi vipindi tofauti tofauti ulivyofanya naye kazi vikunganishwa visiwe chini ya miezi 12

Kuna swali umeuliza hapo kuwa kama unasaini mkataba wa mwaka mmoja mmoja je kuna malimbikizo ya kiinua mgongo?
Jibu ni ndio manake ajira yako ilikuwa endelevu maana ulikuwa unarenew mkataba kila mwaka so itaunganishwa miaka yote uliyofanya kazi, mwajiri atakapositisha ajira yake basi ukokotoaji wa kiinua mgongo utachukulia miaka yote uliyofanya kazi.

Kitu kingine kikubwa cha kuangalia hakikisha unasoma mkataba vizuri kabla ya kuusaini, manake kuna waajiri wanaweka vifungu vya kujihami na malimbikizo mfano unakuta kipengele kinasema "Mkataba huu unafuta makubaliano mengine yoyote yaliyowahi kufanyika huko nyuma" au "kwa makubaliano hayo ninakiri sina madai mengine yoyote ya nyuma" lazima uwe makini na ikiwezekana omba ushauri/ufafanuzi kwa mwajiri au mwanasheria yoyote kabla ya kusaini mkataba wako. Kama umeandikwa kwa kiingereza na huelewi basi mwajiri ana wajibu wa kukufafanulia kipengele kwa kipengele ili uelewe. Usikimbilie tu kusaini mkataba kwa sababu uko desperate na kupata hiyo ajira.

Katika moja ya career training nilizowahi kupata nikiwa chuo miaka ya nyuma trainer alikuwa anatuambia unapoenda mahali kufanya usaili ama kusaini mkataba hakikisha hauna njaa, make sure umekula na umeshiba vizuri, kwa sababu ukiwa na njaa unajikuta unajibu maswali ya usaili hadi unatia huruma au unasaini mkataba fasta bila hata kuusoma kwa sababu una njaa. Ukiwa umeshiba unakuwa na confidence kwenye usaili na kama ni mkataba unasaini ukiwa umerelax.

BTW...sorry kwa maelezo ya zaida, nilikuwa najaribu kupanua mjadala tu.
 
Mkuu Buswelu,

Thanks very much for this.....! one of the very interesting sections is 34(1)(a)-(b) on Paternity Leave! I have just copied this;

During any leave cycle, an employee shall be entitled to-

(a) at least 3 days paid paternity leave if-
(i) the leave is taken within 7 days of the birth of a child;
and
(ii) the employee is the father of the child;

I think the law is not fair by giving just 3 days for the father to be with the new baby and its mother. The father needs enough time to stay together with the new family, help through the wife who needs to rejuvenate after many weeks of pregnancy and tough delivery job. At least the father should have been given 7 clear working days for this reason.

Mkuu Buswelu;

Nilisikia kitu kama mwaka jana kuna regulations mpya kuhusu malipo ya likizo kwa wafanyakazi wa sekta mbalimbali....vipi utakuwa na copy ya hii kitu?
 
Hii ni kati ya documents anazopaswa kupewa mfanyakazi anapoajiriwa. Sasa sijui kama ndivyo hivyo.

Mkuu,

Labda developed world....bongo sijui.....! Mimi nimeshabadilisha ajira kama mara tatu hivi tangia ni graduate, lakini hakuna hapa Employer mmoja aliye nikabidhi msahafu huu....nafikiri kwa sababu waajiri wengi hawapendi kufuata hizi sheria za kazi so sitashangaa kuona hawawapi copy waajiriwa wao!
 
wanajamii naomba kuuliza hivyi ikitokea mwajiri kakulipa msharaha kimakosa (yani kazidisha amount fulani katika mshahara wako kwa mda wa zaidi ya miezi 2) je ni sahihi mshahara wako kushushwa tena kama hilo kosa lilikuwa la mwajiri. je sheria ya kazi inasemaje kuhusu hilo wanasheria tunaomba mtutafsirie.
 
Pengine nifafanue kuwa sheria ime-provide minimun standards. na ndicho kilichoandikkwa hapo juu " at least 3 dayspaid paternity leave..."

Nini maana yake. Sheria imejaribu kutoa standards ambazo kila mwajiri atweza kuzimudu na kuzitekeleza kwa urahisi hat sisi ambao tuwa wadsaidizi wa ndani mna siku zote uwa tujajisahau ama kufikiri siyo waajiri kama makampuni.

Kwa mantiki ya sheria ni kuwa wafanyakazi kupitia vyama vyao (trade unions) au mabaraza ya mashauriano wanaweza kuongea na mwajiri wao na hiyo paternity leave kuwa siku 10 au 15 au 20 au vyovyote vile ambapo pande mbili kati ya mwajiri na wafanyakazi wataweza kuridhia.

Tatizo ninaloliona na ni la uzoefu ni kuwa wafanyazi wanachua tafsiri kuwa sheria imetoa siku 3 bila kujali ama kuangalia kuwa iko ni kiwango cha chini ambacho mwajiri endapo hatakiuka basi anaweza kuchukuliwa hatua kwa kushindwa kutekeleza mahitaji ya kisheria (minimum standard). kwa upande wa pili ni kma nilivyodokeza hapo juu, endapo sheria ingetoa siku 10, au 20 then ingekuwa tatizo kubwa kwetu sisi waajiri wa majumbani kwa mzigo wa utekelezaji wake ungekuwa mgumu hasa ukizingatia ukweli kuwa hat mimi mwenye kipato cha laki moja nikiwa na hoseboy ni mwajiri ya tayari, sasa ikiwa nimpatie 20 days paid paternity leave sidhani kam nitaweza au wote wenye kipata cha aina hiyo tutaweza kutekeleza sheria husika.
 
wanajamii naomba kuuliza hivyi ikitokea mwajiri kakulipa msharaha kimakosa (yani kazidisha amount fulani katika mshahara wako kwa mda wa zaidi ya miezi 2) je ni sahihi mshahara wako kushushwa tena kama hilo kosa lilikuwa la mwajiri. je sheria ya kazi inasemaje kuhusu hilo wanasheria tunaomba mtutafsirie.

Hapa swali lako limekaa kimtego kidogo. Lakini kama nimekuelewa vizuri, unazungumzia makosa ya payroll tu. Na sio kwamba mwajiri amekupa kabisa barua ya increment then anataka kushusha mshahara after two months. Kama ni overpayments due to payroll errors, mwajiri anaruhusiwa kukukata hiyo overpaid amount provided that the total deductions does not exceed one quarter of your salary.

Section 28(5) of the ELRA 2004 states that; An employer shall not require or permit an employee to (a) repay any remuneration except for overpayments previously made by the employer resulting from an error in calculating the employee's remuneration.

So, deductions zinaruhusiwa kisheria kama kweli kuna kosa la overpayments.
 
Hii inabidi kuwa nayo kwenye hali tete kama kule North Mara kwa sasa wanavyo punguza wafanyakazi kwa kisingizio cha GFC, huwezi jua wanatumia kigezo gani..wakati wanaacha expart 12 kwenye kitengo kimoja.

Wa nini..kwa kawaida Expart moja anatakiwa kuwa na watu wa chini yake 6 mpaka nane, sasa department ina wafanyakazi 30 Expart 12 wa nini?Harafu unataka punguza nationals..
 
Asante sana Mkuu Buswelu. Ni leo asubuhi tu, nilikuwa natafuta hii Labour Law bila mafanikio.

Shukrani sana Mkuu.

JF forever.

wandugu, msihangaike kutafuta sheria. sheria zote za tz kuanzia mpya hadi za zamani, zipo kwenye website ya parliament of tz. nenda kule utaipata kwenye pdf. nashangaa wengine wanasema walikuwa wanatafuta sheria hizi, wakati ziko wazi sana, tena mno.
 
Mkuu,

Labda developed world....bongo sijui.....! Mimi nimeshabadilisha ajira kama mara tatu hivi tangia ni graduate, lakini hakuna hapa Employer mmoja aliye nikabidhi msahafu huu....nafikiri kwa sababu waajiri wengi hawapendi kufuata hizi sheria za kazi so sitashangaa kuona hawawapi copy waajiriwa wao!

kukabidhiwa is one thing....na kuusoma je?

nani hata huwa anjisumbua kusema nikatafuta sheria ya kazi ili nijue haki na wajibu wangu kama mwaajiriwa??
Of coz hata wewe ungekuwa mwajiri ungetumia viudhaifu vya dizaini hiyo kuwabania watu
ukweli ni kwamba wengi wetu hatupendi kujishughulisha hata kwa mambo ambayo ni ya manufaa kwetu...
after all mwajiri hana obligation ya kukupa huu msaafu anapokuajri, unabaki kuwa wajibu binafsi tu.......
 
kukabidhiwa is one thing....na kuusoma je?

nani hata huwa anjisumbua kusema nikatafuta sheria ya kazi ili nijue haki na wajibu wangu kama mwaajiriwa??
Of coz hata wewe ungekuwa mwajiri ungetumia viudhaifu vya dizaini hiyo kuwabania watu
ukweli ni kwamba wengi wetu hatupendi kujishughulisha hata kwa mambo ambayo ni ya manufaa kwetu...
after all mwajiri hana obligation ya kukupa huu msaafu anapokuajri, unabaki kuwa wajibu binafsi tu.......

Lakini iko haja ya kuijua sheria ya kazi
hapa nilipo Contract ya job na msaafu unakabidhiwa ..
 
Lakini iko haja ya kuijua sheria ya kazi
hapa nilipo Contract ya job na msaafu unakabidhiwa ..

haja ipo my dear tena bila kupingwa

duh hiyo ya kukabidhiwa msaafu ofisi chache zinafanya......safi sana
 
Mkuu Buswelu,

Thanks very much for this.....! one of the very interesting sections is 34(1)(a)-(b) on Paternity Leave! I have just copied this;
During any leave cycle, an employee shall be entitled to-
(a) at least 3 days paid paternity leave if-
(i) the leave is taken within 7 days of the birth of a child;
and
(ii) the employee is the father of the child;
I think the law is not fair by giving just 3 days for the father to be with the new baby and its mother. The father needs enough time to stay together with the new family, help through the wife who needs to rejuvenate after many weeks of pregnancy and tough delivery job. At least the father should have been given 7 clear working days for this reason.

Mkuu Buswelu;

Nilisikia kitu kama mwaka jana kuna regulations mpya kuhusu malipo ya likizo kwa wafanyakazi wa sekta mbalimbali....vipi utakuwa na copy ya hii kitu?

Just wanted you to know that the law you menitioned (see my highlight) says that you are entilteld to at least 3 days. This is the minimum number of days. Each organisation is entitled to increase the number. I know of organisation here in TZ who have seven days partenity leave and other who have 14 and even some embassies which have 28 days.

Ni vizuri sana wakati wafanyakazi wananegotiate voluntary agreements to argue for more inclusion of the days.
 
kukabidhiwa is one thing....na kuusoma je?

nani hata huwa anjisumbua kusema nikatafuta sheria ya kazi ili nijue haki na wajibu wangu kama mwaajiriwa??
Of coz hata wewe ungekuwa mwajiri ungetumia viudhaifu vya dizaini hiyo kuwabania watu
ukweli ni kwamba wengi wetu hatupendi kujishughulisha hata kwa mambo ambayo ni ya manufaa kwetu...
after all mwajiri hana obligation ya kukupa huu msaafu anapokuajri, unabaki kuwa wajibu binafsi tu.......

In actual sense you are supposed to demand it. Hawewezi tu kukupa unless wanafollow employment best practices.
 
Jamani nisaidieni kupata "Public service Regulations 2003 nimeangalia website ya bunge haipo.
Natanguliza shukurani
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom