Tanzania Labour Law (Sheria ya Kazi Tanzania)

Posho ya kukaimu ni difference ya mshahara wako na amount iliyokuwa attached kwenye hiyo nafasi unayoishikilia. Sijui kama nimeeleweka....mfano

Cheo unachokaimu ni cha meneja
Na salary ya meneja ni 900,000
Wewe ukiwa kama HR mshahara wako ni 700,000 na umetakiwa kukaimu nafasi ya meneja.

Hivyo acting allowance utalipwa difference ya salary yako na ile iliyokuwa attached kwenye cheo cha meneja (900,000 - 700,000 = 200,000) so utalipwa laki 2
Habari,

Naomba mtu anielekeze jinsi ya kukokotoa acting allowance

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau naomba kujua sheria ya kazi inasemaje kwasasa hivi kuhusu
1.Notice of termination.
2.severance pay.
 
Swali lako nitalipa ufafanuzi kama ifuatavyo na wajumbe wengine watachangia pale nitakapopungukiwa

masuala yote ya kazi yanasimamiwa na sheria na kanuni zinazojulikana kama ( SHERIA YA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI YA MWAKA 2004 na KANUNI ZA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI MWAKA 2007) sasa tuanze kufafanua kwa mujibu wa maswali yako.

Notice of termination.
Kwa kutumia Sheria ya ajira na mahusiano kazini ya Mwaka 2004 kifungu cha 41 kinaeleza wazi ni siku 28 ndio pande zote mbili zinatakiwa kutoa taarifa za Notice of termination. ikieleza sababu na muda pia kuna masharti ya utoaji wa Notice of termination haiwezekani mtu yupo likizo alafu umpe Notice of termination pia mfanyakazi hutakiwi kukataa kufanya kazi kipindi cha Notice of termination

Lakini katika Notice of termination kwa mfano una mkataba wa muda maalumu Notice of termination itatolewa ikikupa taarifa kwamba hautaongezewa mkataba pindi pale mkataba wako utakapofika mwisho maana yake mkataba wako utakoma wenyewe pale muda utakapofika mwisho hii ni kwa mujibu wa KANUNI ZA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI YA MWAKA 2007 kifungu cha 4

Notice of termination hutegemea sababu maana yake kuna sababu kama 4 za kupewa Notice of termination na kila sababu inautaratibu wake wa kufatwa 1. Mwenendo mbaya 2. Kutohitajika 3. Kupunguzwa kazini 4. Kutokuwa na uwezo au kukosa uwezo baada ya kuajiriwa hizi sababu zote Notice of termination hutolewa kwa kufatwa taaribu tofauti tofauti sasa hapo inategemea wewe umeangukia wapi

severance pay
Hii kwa kiswahili tunaita kiinua mgongo
mahesabu yake huwa ni mshahara wa siku 7 kwa idadi ya miaka uliyotumikia kampuni husika mfano mshahara wako kwa siku ni 10,000 na umekaa kwenye kampuni miaka 2 itakuwa hivi 10,000*7*2=140,000 hivyo kitakachobadilika ni iyo idadi ya miaka uliyotumikia kampuni husika sasa sheria ipoje ili uweze kupata

SHERIA YA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI MWAKA 2004 kifungu cha 42 ipo hivi unatakiwa kutumikia angalau miezi 12 kampuni husika, pia usiwe umeachishwa kazi kwa mwenendo mbaya kama Wizi na makosa mengine ya utovu wa nidhamu

Ila unapolipwa kiinua mgongo unatakiwa malipo mengine uwe umeshalipwa bila kupunjwa kama likizo na je kuachishwa kazi kwako kulifatwa taaratibu halali za kisheria

Natumaini hata wengine watakuja kuongeza nilichochangia mimi natanguliza shukrani
 
Mkuu asante sana kwa ufafanuzi wako lkn nina maswali mawili hapo kutokana na maelezo yako.
1.ulisema kuna sababu kama nne ambazo zinaweza kutumika kama kigezo cha termination na ukataja kigezo kimojawapo ni kutotakiwa,sasa hii kutotakiwa inakuwaje au inakuwa na vigezo gani?ina maana kama muajiri hanipendi ana uwezo wa kuniachisha kazi bila sababu na sheria inamruhusu?
2.Napenda kujua pia kwenye kipengele cha mwenendo mbaya kazini,ni vitu gani ambavyo mfanyakazi akivifanya vinatafsiriwa kama mwenendo mbaya kisheria?

Kutohitajika hiki kiswahili chake ndio changamoto ila naamini tutaelewshana tu kifungu cha 22 kanuni za ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2007 ipo hivi mfano una mahusiano mabovu na wafanyakazi wenzako tunakuweka kundi la kutohitajika kuna hii ipo sana sehemu kama CASINO Kuna wale wateja wakubwa wanaocheza kamari hata za milion 200 anaweza kusema kwa meneja wako kwamba kila nikija hapa nikimuona huyu muhudumu sijisikii amani nazani unaelewa kinachofuata au kuna ile kampuni ina utamaduni wa team work sasa ikaonekana wewe huendani na huo utamaduni inakuwa ngumu kuendelea kuhitajika kwenye kampuni hiyo au wewe unafanya kazi microfinance na tunajua zina riba kubwa ila huwezi kuja kusikia mfanyakazi wao kakanusha kwa chochote ukifanya hivyo tunasema huendani na utamaduni wa kampuni. hapo ndo point ya kutohitajika inapokuja.

mfanyakazi akivifanya vinatafsiriwa kama mwenendo mbaya kisheria? 1. KUCHELEWA 2 DHARAU 3. ULEVI WA KUPINDUKIA 4. KUPIGANA 5. KULETA HASARA KUBWA KWA KAMPUNI 5. MAKOSA MENGINE YA KINIDHAMU
 
Mkuu sawa nimekuelewa kwenye hilo swali namba 2 sawa halina utata,lakini kwenye majibu ya swali namba moja bado linanitatiza yaani kwa mfano umeajiriwa kwenye kampuni halaf ukawa huendani nayo labda kwenye team work au ktk mambo mengine uliyoyataja,sasa swali linalonitatiza ni kwamba watawezaje kupata evidences za kupeleka kwenye mahakama ili ikubalike kwamba kweli huendani na team work yao?
 
mfano unamahusiano mabaya na wafanyakazi wenzako kinaitishwa kikao cha pamoja na wafanyakazi yataandikwa maudhurio ya wafanyakazi na maridhio ya kikao kimaandishi alafu unaondolewa ili kutohatarisha usalama eneo la kazi sasa
 
hapo kweli hakuna ujanja,japo kwa mazingira ya kitanzania hao watu wanaweza kutengenezwa tu
mfano unamahusiano mabaya na wafanyakazi wenzako kinaitishwa kikao cha pamoja na wafanyakazi yataandikwa maudhurio ya wafanyakazi na maridhio ya kikao kimaandishi alafu unaondolewa ili kutohatarisha usalama eneo la kazi sasa
 
Sheria ya Kazi.. inasemaje kuhusu

WAFANYAKAZI walioweka nia ya kugombea.. nafas mbalimbali serikalini

Kisha

Kuzuiliwa MISHAHARA yao..

Je .. Hii ishu inaingia ktk kipengele kipi kisheria.. tukizingatia ni haki kikatiba Mtanzania yeyote mwenye sifa stahiki agombee Uongozi.
IMG-20200722-WA0047.jpg
 
Wanasheria Kukiwa na mgogoro Kati ya kampuni ya Kiribo na Mgodi wa Barrick hapa Sheria ya kazi inasemaje kuhusu wafanyakazi ambapo wafanyakazi wamesitishiwa ajira zao tangia mwezi wa sita na mpaka wa leo hawajalipwa stahiki zao zozote na mwajiri Kama mkataba wa kusitishiwa ajira unavyoonesha hapa chini na mkataba huo wafanyakazi karibia wote wameshausaini na wanasubiria tu hela zao Ila mpaka Muda huu hamna maelezo yoyote ya kupewa haki zao kwa kisingizio kwamba hajalipwa na Mgodi wa Barrick ambao wameshikilia pesa zake,,

1.Kama Ni hivyo Nini kifanyike hapa ili wafanyakazi walipwe stahiki zao au watasubiria mpaka pale Mgodi wa Barrick utakapomlipa pesa mwenye kampuni ili alipe wafanyakazi wake.
2.Na kama wafanyakazi karibia wote wameshausaini mkataba wa kusitishiwa ajira na fedha zao hawajalipwa Hadi Muda huu hapa sheria ya kazi inasemaje.
IMG_20200810_132038.jpg
 
HABARI WAKUU,
NAOMBA KUULIZA

Ni haki/stahiki gani napaswa kupata kutoka kwa mwajiri wangu endapo endapo amenipunguza kazini?

Niliajiriwa rasmi mwezi wa 10 mwaka jana 2019, baada ya miezi mitatu yaani mwezi wa 01 mwaka 2020 nikabadiliishiwa kitengo kutoka kitengo "A" kwenda kitengo "B" ambacho mshahara wake kidogo upo vizuri kutokana na utendaji wangu wa kazi.

Ila wakati nabadilishiwa kitengo sikupewa mkataba badala yake nikapewa "barua ya promosheni) ambayo inaonesha allowances na kiwango cha mshahara mpya (basic salary), nilipohoji kuhusu mkataba mpya nikaambiwa kuwa, nitatumia mkataba ule niliopewa awali, ila mshahara na allowances mpya ndio vimeandikwa kwenye barua ya promosheni, mpaka ukiisha mkataba wa awali ndio nitapewa mpya ambao utajumuisha yote kwa pamoja katika mkataba huo mpya.

Sasa siku ya leo tumepewa barua za wito wa kwenda kukutana kwenye kikao cha pamoja na mwajiri kwaajili ya kujadili kuhusu kupunguzwa kwa wafanyakazi.

Jumla ya muda niliofanyakazi tangu niajiriwe ni miezi 10,
Na Jumla ya muda ambao nimefanyakazi kwenye hiki kitengo nilichohamishiwa ni miezi 8 tu, na sikupewa mkataba katika hiki kitengo isipokuwa barua ya promotion tu.

Je, kuna stahiki gani ambazo natakiwa kupewa na mwajiri wangu kama mfanyakazi maana anapunguza wafanyakazi kwa madai kuwa kampuni inajiendesha kwa hasara hivyo ameona ni bora kupunguza wafanyakazi wake nikiwemo na mimi.
Naombeni ushauri na majibu .
Ahsanteni.
 
Scenario ya case kama hii.
...unafanya interview then unaambiwa umefaulu na wanakupa offer letter.
Ndani ya offer letter inaandikwa umechanguliwa kujiunga na kampuni xxx,..ila utakuwa chini ya uangalizi(profanation) kwa miezi mi3 inaweza ongezwa mpaka miezi 6..inaandikwa kipindi cha probation utakuwa unafanyiwa performance review kila week na supervisor wako.

Ndani ya mwezi huo huo (kama week 3 hivi) unashtukia unapewa barua ya kuachishwa kazi.Hakuna siku yoyote umewahi itwa au fanyiwa performancy reviews au kuonywa kwa kosa lolote.
Unajaribu kuwauliza sababu ya wao kukusimamisha kazi-wanasema uko kwenye probation period hivyo mwajiri anaweza kukufukuza wakati wowote akiamua na sheria inamruhusu.
(Baadaye unagundua amempata mfanyakazi mwingine aliyekubali kulipwa mshahara mdogo kuliko mliokubaliana ndio maana kaamua kukufukuza)

Hii imekaaje kwa jicho la sheria za kazi ?!
 
Scenario
1. Mtumishi wa umma anashtakiwa mahakamani kwa kosa la jinai linaloihusisha ofisi anayofanyia kazi (Mfano: Wizi wa pesa za ofisi)
2. Muajiri wake anamsimamisha kazi na kumlipa nusu mshahara
3. Mtumishi anashinda kesi hiyo ya jinai mahakamani
4. Muajiri anaendelea kumlipa nusu mshahara mtumishi huyo na hamrudishi kazini zaidi ya mwaka mmoja tangu kesi kuisha

Maswali
1. Ni halali kisheria muajiri kumlipa nusu mshahara mtumishi wa umma katika mazingira hayo? Kabla na baada ya kesi kuisha
2. Ni muda gani muajiri anatakiwa kisheria awe ameshamrudisha kazini mtumishi husika?
3. Ni muda gani muajiri anatakiwa awe amesharejesha mshahara wa awali?
4. Ni muda gani muajiri anatakiwa awe ameshalipa hela yote ya mshahara aliyomkata mtumishi husika?
5. Je kuna fidia yoyote mtumishi husika anaweza kumdai muajiri wake?

bora uhai Petro E. Mselewa
 
Back
Top Bottom