Tanzania Labour Law (Sheria ya Kazi Tanzania)

Mkuu deonova Annual Leave au tuseme likizo ya mwaka inastahili malipo? Inakuwa included kwenye zile zinazoitwa paid leave?

Annual leave ni paid leave pia kwa sababu licha ya kwamba utakuwa likizo bado utastahili kupokea mshahara wako, lakini pia utastahili kupatiwa leave travel assistance (nauli ya posho ya kujikimu) unapoenda likizo; lakini hii unaliopwa once in every two years of continuous service with the same employer.
 
Asante sana. Kwa hiyo ndani ya miezi 12 ya mwaka nitakuwa na mishahara 13 au unamaanisha nikiwa leave ule mshahara wa mwezi huo ndio watakaopokea wenzangu ambao wapo kazini nami ndio huo huo?
Ni ule mshahara unaolipwa ukiwa haupo kazini. Ni mishahara 12 tuu.
 
Mwajiri anawajibika kukuruhusu kwenda likizo ya siku 28 kila mwaka na anapaswa kukulipa mshahara wakati wa likizo hiyo.

Mwajiri halazimishwi na Sheria kukulipa posho ya likzo labda km ni sehemu ya makubaliano kwenye Mkataba wenu au Mkataba wa Hari bora km upo..

Watumishi wa Umma hupewa hela ya nauli kwenda likizo makwao mara moja kwa miaka miwili. Hii ni kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu ktk Utumishi Umma. Wengine hususani kwenye Taasisi hulipwa nauli kama hii kila likizo.
KWA nyongeza. ukiwa likizo. gafla mwajili akasitisha likizo yako. basi atakulipa mshahala wako basic. sio take home.
 
deonova naomba ufafanuzi wa iwapo mfanyakazi atahamishwa kituo, mfano kutoka Mvomero kwenda Mpwapwa, mahesabu ya uhamisho wa mizigo na familia yanapigwaje kwa huo umbali!
Stahiki nyingine anazopaswa kupewa ni zipi pia?
 
Hicho ndo kimenikwamisha mkuu kwani nimeogopa kuwafuata isije kuwa bado wako ndani ya muda halafu wakanigeuzia kibao kuwa nawapangia cha kufanya, hebu nisaidie kipengere cha muda wa wao kunijibu Mara baada ya mm kuwa nimewajb
Kwenye mapambano uwoga weka pembeni
 
Unafahamu ni kwa namna gani Sheria za Ajira na Mahusiano Kazini zinaathiri wafanyakazi wa muda mfupi? Mwanasheria Emmanuel Mwesiga amefanya tafiti kuhusu hilo na ameeleza vizuri maana ya wafanyakazi wa muda mfupi, sheria za Tanzania zikoje kuwahusu ukilinganisha na nchi zingine, athari zinazoweza kusababishwa na sheria zilizopo na mapendekezo yake kwa wadau mbalimbali ikiwemo wafanyakazi wenyewe.

Bonyeza linki ifuatayo The RISACHI _ S01E08 with Emmanuel Mwesigakutazama mahojiano aliyofanya na The RISACHI
 
Sekta binafsi mkuu.

Kama ni hvo zinakuwa calculated kulingana na gharama na nauli za Sumatra za wakati huo (nauli yako na mke/mume na watoto wasiozidi 4), stahiki zingine ni kama gharama za kusafirisha mizigo (utampelekea mwajiri wako invoice ya gharama za mzigo wako, invoice utapewa na kampuni ya malory wanaosafirisha mzigo wako), utalipwa fedha ya kujikimu njiani kama unasafiri zaid ya masaa 6 na gharama za kujikimu unapofika kule point B unakohamishiwa (kama haupewi nyumba na mwajiri).
 
Samahani,mimi mbona niki download sheria ya kazi kuja kufunguka inasomeka kikorea cjui kijapani nasio English ili nielewe. Msaada jaman
 
Kwa kweli wafanyakazi wananyanyaswa sana, nipo kama inspector upande Wa client, malalamiko kutoka kwa Labourers Wa upande Wa contractor ni mengi sana, Labourer officers saidieni watz
 
Hivi sheria inasemaje kuhusu mfanyakazi anapokufa anapofariki akiwa katika kutekeleza majukumu yake ya kazi
 
Kwa kweli wafanyakazi wananyanyaswa sana, nipo kama inspector upande Wa client, malalamiko kutoka kwa Labourers Wa upande Wa contractor ni mengi sana, Labourer officers saidieni watz

Yaani hii labour Law sijui inasaidia wapi!!
Kwa sababu sheria haifuatwi na vyama vyetu kama TUIKO sijui wako wapi,

Wananchi wasio na elimu kubwa na wamepata ajira kwenye sectors binafsi kwa kweli wanaonewa sanaaaaa.

Wanafanya kazi nje ya muda husika
Mfano: wanafanyakazi siku 6 za wiki kwa masaa 8 la tisa ni lunch

Kwa maana hiyo wanafanya kazi masaa 48 kwa wiki wakati sheria inataka masaa 45 kwa wiki! Na bila overtime

Mishahara wanalipwa chini ya kima cha mishahara ilielekezwa na serikali.

Yapo madudu mengi sanaa na ukitaka evidence nitakuapa.
 
Sheria inasemaje kuhusu mtumishi wa umma asipokuwapo kazini bila taarifa kwa siku 3
Natanguliza shukran
 
Naomba kujua ikiwa mtu umeajiriwa kwa mkataba wa makubaliano ya mdomo bila maandishi( oraly contract or agreement) yakufanya kazi bila kupewa muda wa matazamio na mwajiri wako, halafu baada ya miezi mtatu tu mwajiri akakuandikia barua ya kukufukuza kazi bila hata kukupatia sitahili zako zozote, je unayo haki ya kumshitaki? Na kama utamshitaki ni kwa sheria gani utamshitaki?
 
Sheria inasemaje kuhusu mtumishi wa umma asipokuwapo kazini bila taarifa kwa siku 3
Natanguliza shukran

Hii ni masuala ya misconduct na Standing Orders itakuwa imeeleza vizuri mkuu, hebu ipitie, naamini wewe ni mtumishi wa Umma hivyo utakuwa unaijua hii
 
Back
Top Bottom