Tanzania Labour Law (Sheria ya Kazi Tanzania)

Habari !

Mi binafsi wanajamvini nilikuwa nauliza kuhusu swala mikataba ya ajira haswa kwenye sekta binafsi..

Kwanza mkataba unatakiwa uweje ?? Pili kama kunakitu iliambiwa kwenye mkataba utapewa harafu still huvioni nini cha kufanya ?? Tatu mkataba wenye mapungufu huwaga unakosa nini ??
 
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA MKATABA WA AJIRA

Mkataba wa ajira ni makubaliano ya kisheria kati ya mwajiri na mwajiriwa ambapo mwajiriwa anakubali kutoa nguvukazi yake kwa kipindi fulani kwa malipo maalumu ambayo watakuwa wamekubaliana na mwajiri. Kama ilivyo kwa mikataba mingine, uhalali wa mkataba ni lazima ujengwe katika nguzo kuu tano ambazo ni makubaliano, hiari ya kuingia mkataba, malipo halali, uwezo wa kuingia mkataba pamoja na uhalali wa shughuli yenyewe itakayofanyika.

Hata hivyo kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004, mkataba wa ajira ni lazima uonyeshe jina na anwani ya mwajiri na mwajiriwa, tarehe mliyosaini mkataba, tarehe mkataba unapoanza na tarehe mkataba utakapomalizika endapo mkataba huo ni wa muda maalumu.

Mkataba wa ajira pia ni muhimu useme mwajiriwa anaajiriwa katika nafasi gani na ikiwezekana utaje majukumu yake kama mwajiriwa pamoja na mahali atakapofanyia kazi. Itafaa pia kama kipengele cha namna ya kusitisha au kuongeza muda wa mkataba kitakuwepo endapo upande wowote utahitaji kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.

Mkataba wa ajira ni lazima uweke wazi haki na wajibu wa mwajiriwa kwa mujibu wa sheria za kazi. Mambo hayo yanaweza pia kuorodheshwa kwenye sera ya kazi ya mwajiri endapo atakuwa nayo. Haki za mwajiriwa ni pamoja na; kiwango cha mshahara stahiki, likizo na siku za mapumziko, saa za kazi, malipo ya asilimia kumi (10%) za mfuko wa hifadhi ya jamii kutoka kwa mwajiri, malipo ya muda wa kazi wa ziada (overtime), haki ya kujiunga na chama cha wafanyakazi na mambo mengine muhimu. Wajibu wa mwajiriwa hujumuisha kufanya kazi kwa bidii, usiri, kutunza muda, nidhamu, kutimiza na kufikia malengo ya mwajiri, kulipa kodi, kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii na mengineyo kwa mujibu wa sheria.

Haki na wajibu wa mwajiri ni muhimu pia ukaelezwa katika mkataba wa ajira. Kimsingi haki za mwajiriwa kwa upande mmoja ni wajibu wa mwajiri kwa upande mwingine na wajibu wa mwajiriwa kwa upande mmoja pia huwa ni haki za mwajiri kwa upande mwingine. Hivyo kila upande ukitimiza wajibu wake, kila upande utapata haki zake pasipo kikwazo chochote. Ikumbukwe kwamba, ni kosa kisheria kumwajiri mtu pasipo mkataba wa ajira


Mkataba wa ajira hulinda mustakabali wa ajira, huondoa migogoro isiyo na lazima na huweka uwazi na uwajibikaji wa pande zote mbili. Usikubali kuajiriwa au kuajiri pasipo mkataba. Ikiwezekana mtafute wakili/mwanasheria akusaidie kuandika na kupitia mikataba yako.

Hakikisha una mkataba wa maandishi wa ajira yako. Pande zote mbili zinapaswa kuwa na nakala ya mkataba huo. Ni kosa na si haki kumsainisha mwajiriwa mkataba na kumnyima kuondoka na nakala ya mkataba aliosaini. Usisaini mkataba ambao huelewi kilichoandikwa. Pata muda wa kutosha kupitia na kuelewa kila kipengele ili kulinda mustakabali wa ajira yako.
 
Mm nimwajiliwa kampun( xx) inayotoa huduma ya chakula katk mgodi wa madin hapa nchin,mwajir kasitisha ajira kwakutangaza and then akaitaj wafanyakaz twende medical ku re-check up bt wafanyakaz tumeshindwa kukubaliana nae coz anadai twende medical and then turud kazin kufanya kaz?,je hii ni sahihi na vp tunaenda medical kabula hatujapewa termination letter???
 
Mm nimwajiliwa kampun( xx) inayotoa huduma ya chakula katk mgodi wa madin hapa nchin,mwajir kasitisha ajira kwakutangaza and then akaitaj wafanyakaz twende medical ku re-check up bt wafanyakaz tumeshindwa kukubaliana nae coz anadai twende medical and then turud kazin kufanya kaz?,je hii ni sahihi na vp tunaenda medical kabula hatujapewa termination letter???
Kama amewaachisha kazi yeye medical check up itamsaidia nini?au kuna kitu sijakielewa hapo?
 
Soma tena mkataba wako wa kazi. Hapo issue ni kusitisha mkataba, nenda sasa usome masharti yaliyoweka. Au kama mnamkataba wa hali bora, staff regulation na Recruitment and selection policy..huo ndo wakati wa kuperuzi hayo makaburasha
 
Angalia mkataba wenu unasemaje,kupima afya ni lazima kila ipitapo miezi 3. Kama alikuwa amewapa ajira rasmi MNA haki zenu . Fuatilia KTK vyombo vya haki na mahakama ya kazi.
 
Kama unahisi unaonewa nenda Mamlaka ya Usuluhishi na upatanishi masuala ya kazi (CMA) ofisi ipo jengo la wizara ya kaz posta
 
Maazimio ya pamoja ya Shirika la Kazi Duniani (ILO)
  • Yanahusu zaidi kanuni za kisheria ambazo zinatoa miongozo na haki katika sehemu ya kazi
  • Kwa ufupi, miongozo na haki sehemu za haki zinahusiana na;
1. Ajira za watoto: No 138/1973; 182/1999
2. Kazi za lazima: No 29/1930;105/1951
3. Ubaguzi: No.111/1958; 100/1951
4. Uhuru wa kuungana na kuingia makubaliano ya hiari ya pamoja: No.87/1948; 98/1949

Haki za mtoto S.5
  • Inazuia ajira kwa mtoto yeyote mwenye umri chini ya miaka 14
  • Mtoto mwenye umri wa miaka 14 au zaidi anaweza kuajiriwa kufanya kazi nyepesi tu,
  • Inazuia kumfanyisha mtoto kazi nyakati za usiku.
  • Ajira zinazozuliwa hapa ni pamoja na aina mbaya za ajira za mtoto kama utumwa, usafirishaji wa watoto, uwekaji rehani kwa ajili ya deni na aina zote za ajira za shuruti, biashara ya ngono na utengenezaji filamu za ngono, kuajiri watoto kwa lazima kwa shughuli za kijeshi n.k
Tazama pia Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009

Kazi za lazima S.6
Sheria inakataza kazi za lazima lakini inatoa nafasi kwa aina fulani za kazi za lazima kama;
  • Kazi yoyote inayotekelezwa chini ya Sheria ya Ulinzi wa Taifa ya mwaka 1966, kwa kazi ambayo ni ya kijeshi.
  • Kazi yoyote ambayo ni sehemu ya wajibu wa kawaida wa kiraia kwa raia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Kazi yoyote inayotekelezwa kwa dharura au hali ya hatari.
  • Kazi yoyote inayotolewa kwa mtu yeyote ikiwa ni matokeo ya kutiwa hatiani na mamlaka ya sheria.
Kuzuia ubaguzi sehemu ya kazi

S.7 - (1) Kila mwajiri atatakiwa kuhakikisha kwamba anaendeleza fursa sawa katika ajira na kujitahidi kuondoa ubaguzi katika sera yoyote ya ajira mazoezi kwa vitendo

(2) Mwajiri atalazimika kusajili kwa Kamishna wa Kazi, mpango wa kuendeleza fursa sawa na kutokomeza ubaguzi katika sehemu ya kazi

(3)Kamishna wa Kazi anaweza kumtaka mwajiri:-
  • Kuunda mpango wa kuendeleza fursa sawa na kutokomeza ubaguzi katika sehemu ya kazi kama inavyoelekezwa katika kifungu kidogo cha (2); na
  • Kuusajili mpango huo kwa Kamishna
  • Kutokuunda mpango huo na kuusajili ni kosa kisheria

(4) Mwajiri yeyote asifanye ubaguzi wa dhahiri au usiokuwa wa dhahiri kwa mwajiriwa, katika sera au mazoea katika moja ya sababu zifuatazo:

a)Rangi
b)Utaifa
c)Kabila au sehemu anayotoka
d)Asili
e)Uasili wa Taifa
f)Asili ya kijamii
g)Maoni ya kisiasa au kidini
h)Mwanamke au Mwanaume
i)Jinsia
j)Ujauzito
k)Kuolewa ama kutoolewa au majukumu ya familia
l)ulemavu
m)VVU/UKIMWI
n)Umri; au
o)Maisha anayoishi

HAKI KUUNGANA WAAJIRIWA

S 9 - (1) Kila mfanyakazi ana haki ya;

a)Kuunda na kujiunga na chama cha wafanyakazi.
b)Kushiriki katika kazi halali za chama cha wafanyakazi.

S 9 - (3) Mtu yeyote haruhusiwi kufanya ubaguzi kwa mfanyakazi kwa sababu huyo:-
  • Ametekeleza au alitekeleza haki yoyote chini ya Sheria hii au Sheria nyingine inayosimamiwa na Waziri.
  • Ni mwanachama au alikuwa mwanachama wa chama cha Wafanyakazi; au
  • Ameshiriki au alishiriki katika kazi halali cha chama

S 9(4) Mtu yeyote haruhusiwi kufanya ubaguzi, kwa mfanyakazi wa chama cha wafanyakazi au shirikisho kwa kukiwakilisha au kushiriki katika kazi halali za chama.

S 9(5) Mtu yeyote anayekiuka masharti ya vifungu vidogo vya (3) na (4), anatenda kosa.

S 9(6) Kwa madhumuni ya kifungu hiki;

a)“mfanyakazi” inajumuisha mwombaji wa kazi;
b)“mfanyakazi wa ngazi ya juu ya uongozi” maana yake ni mfanyakazi ambaye, kulingana na nafasi ya mfanyakazi huyo-
  1. Anatengeneza sera kwa niaba ya mwajiri; na
  2. Anaruhusiwa kuingia mikataba ya hiari kwa niaba ya mwajiri.

HAKI YA KUUNGANA WAAJIRI


S. 10 - (1) Kila mwajiri atakuwa na haki-

a)Kuunda na kujiunga na chama cha waajiri;*
b)Kushiriki katika kazi halali za chama cha waajiri,

S .10 - (2) Mtu yeyote haruhusiwi kufanya ubaguzi kwa mwajiri kwa sababu mwajiri-
  • Ametekeleza au alitekeleza haki yoyote chini ya Sheria hii au Sheria inayosimamiwa na Waziri;
  • Ni mwanachama au alikuwa mwanachama wa chama cha waajiri; au
  • Ameshiriki au alishiriki katika kazi halali za chama cha waajiri.

VIWANGO VYA AJIRA

1. Mikataba ya Ajira

a). Aina za mikataba
  1. Mkataba kwa kipindi cha muda usiotajwa (mara nyingi huitwa mkataba wa kudumu)
  2. Mkataba kwa kipindi cha muda kilichotajwa
  3. Mkataba wa kazi maalumu
Kazi maalumu - maana yake ni zile zinazotokea mara chache au za msimu ambazo sio endelevu. ( ELRA Misc. Amendment No 38 of 2015; S.4)

b). Taarifa ya maelezo ya maandishi S.15
15-(1) Mwajiri anatakiwa kumpa mfanyakazi, maelezo ya mkataba kwa maandishi kama-

i. Jina, umri, anuani ya kudumu na jinsia ya mfanyakazi
ii. Mahali alipoajiriwa
iii. Kazi yake
iv. Tarehe ya kuanza
v. Muundo na muda wa mkataba
vi. Kituo cha kazi
vii. Masaa ya kazi
viii. Ujira, njia ya ukokotoaji wake, na taarifa za mafao mengine au malipo ya vitu; na
ix. Kitu kingine kilichotajwa

(2) Kama taarifa zote zilizotajwa katika kifungu kidogo cha (1) zimeelezwa kwenye mkataba wa maandishi na mwajiri amempa mfanyakazi mkataba huo, mwajiri anaweza asitie maelezo yaliyoandikwa yaliyotajwa katika kifungu cha 14.

(3) Kama mfanyakazi haelewi maelezo yaliyoandikwa , mwajiri anatakiwa kuhakikisha kwa yanafafanuliwa kwa mfanyakazi katika hali ambayo mfanyakazi anaelewa.

(4) Pale ambapo suala lililotajwa katika kifungu kidogo cha (1) litabadilika, mwajiri atatakiwa kwa kuwasiliana na mfanyakazi, kurekebisha maelezo yaliyoandikwa ili kuendana na mabadiliko na kumtaarifu mfanyakazi mabadiliko hayo kwa maandishi.

(5) Mwajiri atatakiwa kutunza maelezo ya maandishi yaliyotajwa katika kifungu kidogo cha (1) kwa muda wa miaka mitano baada ya kusitishwa kwa ajira

(6) Ikiwa katika mwenendo wowote wa kisheria, mwajiri atashindwa kutoa mkataba wa maandishi au maelezo ya maandishi yaliyotolewa kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (1), jukumu la kuthibitisha au kukanusha sharti la ajira linalodaiwa na lililotajwa katika kifungu kidogo cha (1) litakuwa ni la mwajiri.

(7) Masharti ya kifungu hiki hayatatumika kwa mfanyakazi ambaye anafanya kazi chini ya siku sita kwa mwezi kwa mwajiri.

2. Masaa ya Kazi

a) Masaa ya kazi – Masaa 9 kwa siku; Masaa 45 kwa wiki; na Siku 6 katika wiki yoyote

b) Si zaidi ya saa 50 ya ziada katika mzunguko wa wiki nne

c) Mwajiriwa hatatakiwa kufanya kazi zaidi ya masaa 12 kwa siku hata kama wamekubaliana hivyo (kifungu cha 19)

d) Kazi zitakazofanyika usiku kati ya saa 02:00 usiku na saa 12.00 asubuhi, Mwajiri atatakiwa kumlipa mfanyakazi angalau 5% ya mshahara wa mfanyakazi huyo kwa kila saa atakayofanya kazi usiku na kama saa anayofanya kazi ni ya ziada; 5% itakokotolewa katika kima cha saa za zaida za mfanyakazi. (Kifungu cha 20(4)).

NB:
Kazi za usiku haziruhusiwi kwa mwanamke mjamzito miezi miwili kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua, au miezi miwili baada ya tarehe ya kuzaa . (Kifungu 20(2))

e) Mapumziko katika siku ya kazi
S.23 - (1): Mwajiri anatakiwa kumpa mfanyakazi ambaye amefanya kazi mfululizo kwa zaidi ya saa 5 mapumziko ya angalau dakika 60. (Break given if the job can be left unattended)

(2) Mwajiri anaweza kumtaka mfanyakazi kufanya kazi wakati wa mapumziko ikiwa tu kama kazi haiwezi kufanywa na mfanyakazi mwingine.

(3) Mwajiri hatakiwi kuwajibika kumlipa mfanyakazi katika kipindi cha mapumziko isipokuwa kama mfanyakazi anatakiwa kufanya kazi au kuwepo kwa ajili ya kazi wakati wa mapumziko


3. Ujira
a) S.26 (2): Kima cha ujira kwa saa, siku au mwezi kitatakiwa kuamuliwa kwa kufuata orodha iliyotolewa katika Jedwali la Kwanza

b). Malipo ya fedha yatakuwa katika bahasha iliyofungwa kama malipo yanafanyika kwa fedha taslimu au kwa hundi (Kifungu 27 (1)(c)); au fedha iwekwe katika akaunti ya benki ambayo mfanyakazi ameichagia mwenyewe kwa maandishi.

c). Mwajiri hatakiwi kufanya makato yoyote kwenye ujira wa mfanyakazi isipokuwa tu yale ambayo yapo kwa mujibu wa Sheria ama mfanyakazi amekubali kukatwa kuhusiana na deni.

d). Malipo yafanyike katika muda wa kazi, mahali pa kazi katika siku waliyokubaliana.


4. Likizo ya mwaka

a). Anayestahili:
Mfanyakazi mwenye miezi chini ya sita kazini hatakuwa na haki ya kupata likizo yenye malipo chini ya masharti ya sehemu hii. ELRA, see Section 29 (1)

Mfanyakazi mwenye utumishi wa chini ya miezi sita na ambaye amefanya kazi zaidi ya mara moja katika mwaka, atakuwa na haki ya kupata likizo yenye malipo chini ya masharti ya Sehemu hii kama jumla ya kipindhi alichofanya kazi kwa mwajiri huyo kinazidi miezi sita kwa mwaka huo. S.29-(1) (b)

S.30-(1) (c) “Likizo yenye malipo” maana yake ni likizo yoyote inayolipwa chini ya Sehemu hii na inayokokotolewa kwa kuangalia mshahara wa kawaida wa mfanyakazi.

S.31-(1) Likizo ya Mwaka; Mwajiri atatakiwa kutoa kwa mfanyakazia angalau siku 28 mfululizo kuhusiana na kila mzunguko wa likizo, na likizo hiyo itajumuisha siku yoyote ya sikukuu ambayo inaweza kuangukia ndani ya kipindi cha likizo

Employment and Labour Laws (Miscellaneous Amendment 2015- amends sect 31 on LEAVE

(6) Kwa makubaliano na Mfanyakazi, Mwajiri anaweza kumruhusu Mwajiriwa kumfanyia kazi katika kipindi ambacho Mfanyakazi huyo alitakiwa kuwa likizo kwa sharti kwamba mwajiriwa huyo asifanye kazi mfululizo kwa miaka miwili. (yaani unamuuzia mwajiri wako likizo yako)

(7) Mwajiri atamlipa mfanyakazi mshahara wa mwezi mmoja badala ya likizo ya mwaka ambayo mfanyakazi alitakiwa kwenda ama alitakiwa na mwajiri kumfanyia kazi badala ya kwenda likizo hiyo.


5. Likizo ya Ugonjwa (Kifungu cha 32

• siku 63 za kwanza – mshahara mzima
• siku 63 zinazofuata – nusu mshahara

Jumla ya siku 126 ambazo mfanyakazi atakuwa na haki ya likizo ya ugonjwa katika kila mzunguko wa likizo (Mzunguko wa likizo katika Sehemu hii ni miezi 36)

ED zinahesabika kama sehemu ya likizo ya ugonjwa

Likizo itatolewa kwa mfanyakazi kuwasilisha kwa mwajiri cheti cha matibabu kilichotolewa na tabibu aliyesajiliwa au tabibu mwingine yeyote anayekubalika na mwajiri, ambacho kukubalika kwake hakutakiwi kukataliwa bila sababu za msingi.

6. Likizo ya uzazi

i). Taarifa (S.33(1)) Mfanyakazi mwanamke atoe notisi kwa mwajiri kuhusiana na kusudio lake la kuchukua likizo ya uzazi angalau miezi mitatu kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua na notisi hiyo italazimika kuambatana na cheti cha kitabibu.

ii). Mfanyakazi anaweza kuanza likizo ya uzazi muda wowote kutoka wiki nne kabla ya tarehe tarajiwa ya kujifungua, au tarehe ya mapema kama tabibu atathibitisha kwamba ni muhimu kwa afya ya mfanyakazi au ya mtoto wake ambaye hajazaliwa

iii). Mfanyakazi hatatakiwa kufanya kazi ndani ya wiki sita baada ya kuzaliwa kwa mtoto wake, labda tabibu awe amethibitisha kuwa anaweza kufanya hivyo. (Section 33(3)

iv). Likizo ya uzazi itakuwa siku 84 au siku 100 kama mfanyakazi atajifungua watoto zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja. (Section 33 (6)

v). Mfanyakazi mjamzito au anayenyonyesha hataruhusiwa kufanya kazi ambazo ni hatari kwa afya yake au kwa afya ya mtoto wake., mwajiri atalazimika kumpa kazi nyingine mbadala inayofaa ikiwa inawezekana, kwa masharti na mazingira ambayo si mabaya zaidi ya masharti na mazingira yake.

vi). Mfanyakazi atakuwa na haki ya masaa hadi mawili kwa siku ya kumnyonyesha mtoto wakati wa saa za kazi.

(G.N No.47 Employment and Labour Relations (General) Regulations, 201)
"Mfanyakazi mwanamke, kwa kipindi kisichopungua miezi sita mfululizo baada ya kuisha kwa likizo ya uzazi, atatakiwa kuondoka mahali pa kazi angalau kwa masaa mawili katika wakati anaoona unafaa, kwa ajili ya kunyonyesha mtoto"

7. Likizo ya Uzazi ya baba na aina nyingine za likizo

a). Angalau siku 3 za likizo ya uzazi ya baba yenye malipo kama:
  • Likizo itachukuliwa ndani ya siku 7 tangu kuzaliwa mtoto
  • Mfanyakazi ni baba wa mtoto. (Section 34 (1)(b) and 34(1)(b)).
b)Angalau siku 4 za likizo ya malipo kwa sababu zifuatazo
  • Ugonjwa au kifo cha mtoto wa mfanyakazi
  • Kifo cha mke wa mfanyakazi, wazazi, bibi na babu, mjukuu au kitukuu
Siku 3 zilizotajwa hapo juu ni jumla ya idadi ya siku ambazo mfanyakazi ana haki bila kujali watoto wangapi wa mfanyakazi wamezaliwa ndani ya mzunguko wa likizo


NAOMBA KUWASILISHA.
 

Attachments

  • Employment and Labour Relations Act No. 6 of 2004.pdf
    492.7 KB · Views: 717
  • Labour Institutions Act No. 7 of 2004.pdf
    1.7 MB · Views: 504
  • GN 47 THE EMPLOYMENT AND LABOUR RELATIONS (GENERAL) REGULATIONS, 2016.doc
    1.1 MB · Views: 916
  • LABOUR LAWS _MISc, 2015.pdf
    57.8 KB · Views: 682
  • WAGE ORDER,196.docx
    3.1 MB · Views: 592
Ongezea stahili za kuachishwa kazi kwa Aina zote za Ajira. Mkataba,kazi maalum na Ajira ya kudumu

Stahiki baada ya mkataba kuisha ama kukatishwa

1.Maana

¨Hizi ni stahiki azipatazo mwajiriwa kutokana na mkataba wake wa ajira kukatishwa na mwajiri. Stahiki hizi hulipwa na mwajiri.

¨Aidha, kipengele cha 44 cha Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini Namba 6 ya mwaka 2004 inampa mwajiriwa haki ya kulipwa stahiki mbalimbali pindi mkataba wake wa kazi unapokatishwa.

2. Aina za Stahiki
  • Malipo ya kazi yote aliyoifanya mwajiriwa kabla ya mkataba wake wa kazi kukatishwa.
  • Malipo kwa likizo yake ya mwaka ambayo atakuwa hajaenda kabla ya mkataba kukatishwa.
  • Malipo kwa likizo za mwaka zilizolimbikizwa. Hii inamaanisha katika kipindi chote cha mkataba kama kuna likizo ambazo mwajiriwa alikuwa hajachukua, basi atastahili kulipwa sawa sawa na idadi ya siku hizo.
  • Malipo yatokanayo na kukatisha mkataba pasipo kutoa/kutanguliwa na notisi. (Notice pay due). Hii ina maana kuwa, badala ya mwajiri kutoa notisi ya kukatisha mkataba kwa mwajiriwa, basi mwajiri anaweza kuamua kumlipa mwajiriwa malipo kiasi ambacho ni sawa sawa na kile ambacho mwajiriwa angekuwa anapata katika kipindi hicho cha muda wa notisi.
  • Kiinua mgongo (severance pay), kama tu mwajiriwa ametimiza vigezo vya kulipwa kiinua mgongo. (S.42, ELRA, 2004)
  • Gharama za usafiri kutoka eneo la mwajiri. Hii ni endapo mwajiriwa wanaachana na mwajiri katika sehemu ya kazi eneo tofauti na alipoajiriwa awali. Kwa mfano Mr. John anaajiriwa na kampuni A ambayo iko Dodoma, halafu baada ya muda akahamishiwa ofisi za kampuni hiyo hiyo zilizopo Arusha, mkataba wake ukikatishwa basi mwajiri atalazimika kumlipa Mr.John gharama za usafiri na kujikimu safarini kurudi hadi eneo alikoanzia ajira yake hiyo Dodoma.
  • Hati ya kazi (Certificate of service). Hii ni hati anayopatiwa mwajiriwa anayeacha/anayeachishwa kazi kutambua mchango wa nguvukazi yake katika huduma/kazi ambayo amekuwa akiifanya katika muda wote wa ajira yake katika kampuni/taasisi husika. Hati ya kazi haitakiwi kueleza sababu za kuacha/kuachishwa kazi.
Baadhi ya stahiki hizi zinatolewa kulingana na vigezo mbalimbali kama;


Ø Sababu za kukatishwa mkataba (grounds of termination)

Ø Aina ya mkataba wa ajira (type of employment contract)

Ø Muda ambao mwajiriwa amehudumu katika huduma/ajira (the length of service to your employer)


3. Ufafanuzi wa Kiinua mgongo (severance pay)

Ufafanuzi wa kipengele cha kiinua mgongo kadiri ya Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini Namba 6 ya mwaka 2004, kifungu cha 42 kinaeleza kama ifuatavyo;

  • Kama mkataba wa ajira umekatishwa na mwajiri kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu ama ukiukwaji wa miiko ya kazi, basi mwajiri halazimiki kulipa kiinua mgongo.
  • Kama mkataba wa ajira umekatishwa kutokana na mahitaji mapya ya uendeshaji wa ofisi/kazi (termination on grounds of capacity or operational requirements), ama kutokana na uanzishwaji wa teknolojia mpya inayohitaji watu wenye utaalamu zaidi, na mwajiri ametoa ajira mbadala kwa watakaoathirika na mabadiliko hayo, lakini wafanyakazi wakaikataa hiyo ajira mbadala basi mwajiri anaweza kukataa kulipa kiinua mgongo.
  • Ni lazima mwajiriwa awe amehudumia katika ajira hiyo kwa muda usiopungua miezi 12 mfululizo ndipo atakidhi kigezo cha kupata kiinua mgongo. Aidha, lazima ukatishwaji huo wa mkataba uwe umesababishwa na mwajiri (termination initiated by employer)
4. Ukokotoaji wa kiinua mgongo

Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini Namba 6 ya mwaka 2004, kifungu cha 42 kimeendelea kueleza juu ya Ukokotoaji wa kiinua mgongo. Kiinua mgongo ni kiasi ambacho ni sawa sawa na kiwango cha mshahara wa siku saba (7) kwa kila mwaka mzima ambao mwajiriwa ametoa huduma pasipo kukatisha; lakini haivuki miaka kumi (10)


Hivyo; Kiinua mgongo = kiwango cha mshahara wa siku 7 zidisha kwa miaka ambayo mwajiriwa ametoa huduma kwa mwajiri katika muda usiozidi miaka 10.


Kima cha mshahara kwa mwezi x 7 x idadi ya miaka

26
(yaani kima cha chini cha mshahara wa sekta husika, kigawanye kwa 26 (yaani siku za kazi 26) kisha zidisha kwa siku 7 halafu zidisha tena kwa idadi ya miaka uliyokaa kazini (hapa weka miaka iliyokamilika tu....mfano umekaa kazini miaka miwili na miezi minne, hapa tunachukua miaka miwili tu iliyokamilika, hiyo miez kwa sababu haijatimia miezi 12 hatuichukui)

5. Gratuiti (gratuity)

Huu ni ukokotoaji wa kiinua mgongo kwa kadirio la asilimia, kadiri ya ongezeko la mshahara wa kila mwezi kulingana na makubaliano ya mwajiriwa na mwajiri.

¨Kwa mfano, mwajiri anayelipa gratuiti asilimia 5%, maana yake kila mshahara asilimia 5% inahesabika kwenye stahiki za mafao.

Ongezeko la gratuity kwa 5% kwa mwezi


April

Mei

Juni

Julai

Mshahara

140,000

150,000

200,000

300,000

Gratuity 5%

7,000

7,500

10,000

15,000


7,000 + 7,500 + 10,000 + 15,000 = 39,500

NB; Asilimia hiyo anatoa mwajiri tu. (haitatokana na makato kwa mwajiriwa)

Samahani kidogo hii chart ya kuonesha ukokotoaji wa kiinua mgongo kwa Gratuity haijaweza kuiarrange vizuri hapa lakini angalau mkisoma mnaweza kupata concept.

Mwajiriwa hatakuwa amekidhi kigezo cha kulipwa kiinua mgongo kama mkataba wa ajira utakatishwa akiwa hajakamilisha mwaka mmoja (miezi 12) tangu alipoajiriwa. Kwa wanaolipwa gratuiti ukokotoaji utafanyika kwa miezi yote ambayo mwajiriwa amefanya kazi.

NINAWASILISHA
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom