Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 10,339
- 17,862
Zaidi ya contract of employment unayopewa na Mwajiri, vile vile kuna Oral Contract ambayo unasaini na Mwajiri ana saini. Kwa Sheria za Tanzania, Mfanyakazi atafanya kazi kwa masaa 40 kwa wiki sawa na masaa 8 kwa siku mara siku 5.Msaada Kwa wajuzi wa Sheria
Niliajiriwa company flani nadhani kutokana na kutokujua Sheria au njaa zangu sula la muda wa kazi kuingia na kutoka sikuzingatia
Sasa ni kwamba nafanya kazi masaa 12 Kwa siku 6 za wiki yaani napumzika siku 1 Kwa wiki.
Nilijaribu kumdokeza mwajiri kuhusu kunilipa masaa ya ziada Ila akawa kama mbogo alie jeruhiwa.
Nataka kujua endapo nitakwenda kufungua kesi je kuna uwezekano wa kupata stahiki zangu..maana hata muda wa kuingia kazini unajulikana Ila muda wa kutoka hakuna sehemu ya sign out
Lakini Nina ushahidi wa watu wanaojua muda ninaotoka.Sina daily evidence ya muda ninaotoka labda itokee kuna kitu basi namsainisha boss namwambia weka na muda uliopokea huu mzigo
Msaada Kwa wajuzi wa
Kinacho endelea kati yako na Mwajiri ni huruma yako tu kufanya masaa hayo 60 kwa wiki ambayo ni ziada ya masaa 12 kwa wiki. Nakushauri;
1. Nenda kaangalie tena mkataba wako ujue ni masaa mangapi ulisaini
2. Kama hayajatajwa masaa ya kazi basi mkataba una mapunhufu. Muombe Mwajiri wako mupitie upya vipengele vya mkataba ili kipengele cha masaa kikae kisheria.
3. Nenda Ofisi ya Kazi Mkoa kaombe upewe mwogozo wa masaa ya kazi ambao utautumia kumuonyesha Mwajiri kwenye kupitia vipengele vya mkataba.
4. Akishaona unauelewa wa haki zako atachukua hatua. Ila ukienda kumshhataki Mahakamani au CMA huwezi kumshinda kwa vile huna ushahidi. Na baada ya hapo kutakuwa na kutoelewana au kuaminiana na wewe.