Tanzania Kwa Yenyewe ni Moja ya Maajabu Saba ya Ulimwengu

Duu hilo ajabu la kiongozi kutojua chanzo cha umaskini wa wananchi wake hakika linge leta watalii wengi maana kila mtu lazima ashangae sana, maana si jambo la kawaida kabisa hapa chini ya mwezi.

Na swala la watu walio kwiba pesa kupewa muda wa kurejesha nalo lingetangazwa lingevuta watu wengi maana kila mtu ange tamani ku kaa nchi kama hii inayo jali wezi kuliko wananchi wake! Na sina uhakika kama hizo pesa zimerudi hadi sasa.

Kwakweli Tanzania yenyewe ni moja ya maajabu ya dunia.

Vijijini hakuna inflations-Malecela
 
Nadhani ni Tanzania tu ndy unaweza kupata rais dhaifu kama huyu tulienae tangu nimeanza chekechea hadi sasa sijawahi kuongozwa na mamonita,viranja macr vilaza kama huyu mkuu wa kaya!..
 
natamani watanzania wote wange yaona maajabu haya. kama mmoja wetu ange-compile maajabu haya na mod kufanya thread iwe permanent hapa jf. Niushauri wangu tu.
 
Tanzania ni nchi tajiri sana, tena ingetakiwa kuwa mojawapo ya nchi tajiri duniani. kila mkoa una madini katika ardhi yake ukiachilia mbali vivutio tulivyonavyo. cha ajabu sisi watanzania hatunufaiki na madini tuliyonayo bali tunanyanyasika na kuuwawa mf. nyamongo na bulyankulu. madini pekee yangetosha kuifanya Tanzania kuwa mojawapo ya nchi tajiri lakini ndo nchi ya tatu kwa umaskini.
 
Nimelipenda na kulifurahia ajabu NAMBA 7,,,,,INGAWA NA MENGINE YANA MANTIKI,,,jaman njia tatu enzi ya TIBAIGANA IMEUA WATU HIII,,,,,,,,

Nilipoona hlo ajabu, nimecheka sana , watu walikula sana mizinga enzi zile.
 
waziri anayejua mpaka idadi ya dagaa na mayai yao.
Mawaziri wasiojiuzuru ng'o hata kama hawafanyi kazi.
Dawa za arv bandia ili kuboresha hali za wananchi.
Chandarua zinazotunza watoto wa bata na kuku.
 
Hilo ajabu namba tatu (3) limenifurahisha na kunihuzunisha. Na hili ajabu ndo linazalisha hayo mengine. Think critically utapata majibu
 
Mkuu umenena, naunga mkono hoja. Tanzania kweli kuna maajabu mengi.

Hili la Rais kutokujua umasikini wa nchi yake ni sawa na baba asiyejua hali ya kipato cha familia yake!

Wanafunzi (si mwanafunzi maana walikuwa wengi) kufaulu pasipo kusoma hii ni kali kuliko yote. Mungu atunusuru maana wengine tunaweza kukosa kazi za kimataifa wakifikiria juu ya hili.

Na hii ya kumbaini mwizi na kumpa muda wa kurudisha alichokuibia, zaidi sana mwizi kujipangia mwenyewe muda wa kurudisha na mwisho ukamwambia, asante baba usiibe tena na sasa waweza kuishi kwa amani, nayo ni kali.

Maajabu mengine:
1.Kutotangaza vivutio vya nchi yako, Kilimanjaro, mpaka jirani yako atangeze, Kenya, ndio unashtuka.

2.Nchi yenye kuzalisha madini pekee ya Tanzanite huku lakini kwenye soko la dunia yanapelekwa na nchi nyingine.

3.Nchi ambayo wananchi wanazuiwa kuuza mazao yao nje badala ya kuwezeshwa kuzalisha zaidi ili kuongeza pato lao na nchi kwa ujumla.

4.Wasomi wengi ni wabinafsi badala ya kuisaidia nchi.
 
1.Ni Tanzania pekee ambapo muungano wa Zanzibar na Tanganyika unawanufaisha wazanzibar pake yao. Maana unanunua mzigo Zanzibar ukifika hapa unambiwa ulipie ushuru wakati nchi ni moja.

2.Ni Tanzania pekee ambapo mnalazimishwa kununua au kulipia vitu kwa dollar na serekali imefumbia macho.

3.Ni Tanzania pekee ambo rais anatamuka wazi kwamba anawajua wauza unga lakini hawezi kutaja majina yao na anaomba waache hiyo biashara.

4.Ni Tanzania pekee kupata kazi bila kuwa na mtu wa kukushika mkono ni kikwazo kikubwa hata kama una qualifications nzuri. na ukiwa binti unajua nini kinafwata.

guys go on and disvover how Tanzania it self is seventh wonders of the world leave alone Serengeti, mt. kilimanjaro etc.
 
Nimelipenda na kulifurahia ajabu NAMBA 7,,,,,,,,


Nimecheka kama mtoto anatekenywa kwa ajabu namba 7, maake nilipata shida sana kuelewa nini kilikuwa kinaendelea nilipokuwa naendesha katika hiyo barabara ya Ali hassan Mwinyi. ha ha ha.
Polisi wanaamini ni uamuzi wa busara kabisa du!!!!!!
 
Tanzania ni nchi tajiri sana, tena ingetakiwa kuwa mojawapo ya nchi tajiri duniani. kila mkoa una madini katika ardhi yake ukiachilia mbali vivutio tulivyonavyo. cha ajabu sisi watanzania hatunufaiki na madini tuliyonayo bali tunanyanyasika na kuuwawa mf. nyamongo na bulyankulu. madini pekee yangetosha kuifanya Tanzania kuwa mojawapo ya nchi tajiri lakini ndo nchi ya tatu kwa umaskini.


Tatizo kubwa ni kwamba viongozi wanakatiwa kidogo wanasaini mikataba na ndo imetoka hiyo. hawakusanyi ushuru wala kufuatilia mapato au kujua ni kiasi gani kinazalishwa katika hiyo migodi. what a waste we have in our beautiful, richest country!!!!!!
 
7. Ni wapi duniani unakuta barabara iliyotengenezwa kwa minajiri ya njia mbili yaani kwenda na kurudi lakini serikali inaamua zigeuzwe ziwe njia tatu yaani mbili za kwenda na moja ya kurudi bila upanuzi wa barabara hiyo kama unabisha nenda Dar ukatembelee barabara ya Ali H.Mwinyi ujionee siasa zinavyoweza kufanya kazi ya kitaalamu hakuna anayeshangaa licha yaugumu kwa magari kushindwa kupishana njia ya kati, pia nauliza ni wapi duniani utakakokuta njia rahisi na salama inayokubalika na askari wa usalama barabarani kuruhusu magari yapite njia zote mbili kuelekea upande moja.

This is actually common in some places than you might imagine, nitakujia sehemu chache nilizoona mimi, Hartford , Ct na Washington DC.
 
Ni Tanzania pekee, ambako mafisadi wanapewa muda wa kurudisha kile walichoiba kwa condition ya kusamehewa!
 
Jaji asiye na shahada ni ajabu linaloweza kutuletea wataliii wengi.
 
Back
Top Bottom