Tanzania Kwa Yenyewe ni Moja ya Maajabu Saba ya Ulimwengu

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,732
jamani badala ya Watanzania kuhamasishwa wapigie kura vivutio vya utalii viingizwe kwenye maajabu saba ya dunia ni afadhali tuipigie Tanzania kura iingie kwenye maajabu hayo kwani hatutatoka haba maana Tanzania yenyewe ni moja ya maajabu kutokana na yanayoendelea na yatakayoendelea kama unabisha fuatilia hapa chini
1. Ni wapi isipokuwa Tanzania utamsikia waziri wa Nishati na madini akijiapiza kwa miungu yake kwamba hakuna mgawo wa umeme wakati kila siku tunaona umeme ukikatika sehemu tofauti kwa muda mrefu za ukiuliza unaambiwa wanarekebisha miundo mbinu wakati kwa akili ya kitoto tu huo ni mgawo wa umeme, kwetu mgawo ni mgawo tu iwe wameshindwa kuilipa DOWANS au iwe ukarabati wa miundombinu, iwe hitlafu ya mitambo au kushuka kwa kina cha maji.

2. Ni Tanzania pekee ambako utakuta wanafunzi hawana madawati wanakaa chini na wengine kwenye vyumba visivyostahili kuitwa vyumba kwa ubovu na uchakavu pia hata umeme hakuna lakini ukasikia ahadi ya kila mwanafunzi kupewa Komputa(Laptop)

3. Haijawahi kusikika popote ulimwenguni kwamba kuna mhitimu aliyefaulu mtihani wake tena wa maandishi huku yeye hajui kusoma wala kuandika isipokuwa Tanzania.

4. Ni wapi duniani Kiongozi wa chama tawala atawaambia wananchi wake hajui chanzo cha umasikini wao kisha akarudi katika uchaguzi na kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtu halafu akapeta katika huo uchaguzi, hii ipo Tanzania pekee ambapo watu wanakichagua chama hicho kwa miaka dahari licha ya ukweli chama hicho hakijajua sababu ya umasikini wao.

5. Hakuna sehemu duniani ambako watu kusahau ni sehemu ya maisha yao ni Tanzania pekee yanaweza yakatokea kama yaliyomkuta Dr. Ulimboka watu wakajidai kupata kiwewe halafu ndani ya mwezi mmoja watu wamesahau kabisa wengine kudai kujiuliza Dr. Ulimboka ni nai?

6. Hii ipo Tanzania tu anaweza kuibuka babu akawaambia nimezungumza na Mungu na amempa dawa na watu wakapanga foleni kama wasio na akili nzuri kwenda kupata muujiza wa mungu unaouzwa kwa shilingi 500 mungu wa wapi anafanya biashara zama hizi.

7. Ni wapi duniani unakuta barabara iliyotengenezwa kwa minajiri ya njia mbili yaani kwenda na kurudi lakini serikali inaamua zigeuzwe ziwe njia tatu yaani mbili za kwenda na moja ya kurudi bila upanuzi wa barabara hiyo kama unabisha nenda Dar ukatembelee barabara ya Ali H.Mwinyi ujionee siasa zinavyoweza kufanya kazi ya kitaalamu hakuna anayeshangaa licha yaugumu kwa magari kushindwa kupishana njia ya kati, pia nauliza ni wapi duniani utakakokuta njia rahisi na salama inayokubalika na askari wa usalama barabarani kuruhusu magari yapite njia zote mbili kuelekea upande mmoja?

8. Maajabu yapo mengi mno na ya kushangaza bado hatujaingiza yale ya Chenji ya RADA, Twiga kupakiwa kwenye ndege kwenda ughaibuni, Polisi kutuhumiwa kuua kisha wenyewe kuunda tume kuchunguza na wakati tume inachunguza mtuhumiwa yuko mahakamani, nyingine ya kushangaza waziri kuunda tume baada ya kuambiwa hana mamlaka anasema ameunda kamati na vyombo vya habari viko kwenye usingizi wa pono, biashara inaendelea kama hakuna lililotokea hii ni Tanzania na Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.
 
Sawa kabisa Mkuu.
Naunga mkono na mguu kwa asilimia 200.
 
Petrol kampala wanauza 3500 kwa tanzania sawa na 2258 change ni 1.55 . mwanza wanauza 2450.na malori yanachukulia dar,hili tu ajabu tosha la dunia
 
Sawa kabisa Mkuu.
Naunga mkono na mguu kwa asilimia 200.

Sikubaliani na wewe kwenye ajabu la kwanza kuhusu umeme. Tofautisha kati ya mgao wa umeme na kukatwa au kuharibika (fault) ya umeme. Ila nakubaliana na maajabu mengine ikiwa ni pamoja na yafuatayo:- Wanaotajirika kupitia wizi,ufisadi na ujambazi wanatukuzwa wakati waadilifu masikini wanabezwa.,
 
Mkuu yapo maajabu zaidi ya hayo haswa kwa awamu hii !
 
Sikubaliani na wewe kwenye ajabu la kwanza kuhusu umeme. Tofautisha kati ya mgao wa umeme na kukatwa au kuharibika (fault) ya umeme. Ila nakubaliana na maajabu mengine ikiwa ni pamoja na yafuatayo:- Wanaotajirika kupitia wizi,ufisadi na ujambazi wanatukuzwa wakati waadilifu masikini wanabezwa.,

Sawa nakubaliana nawe kwa marekebisho. Hivyo naunga mkono kwa asilimia 150. Halafu hao wezi wetu tunaowabaini huwa tunawapa muda kurejesha fedha walizoiba jambo ambalo hata hivyo hawalitekelezi, na maisha yanasonga tu.
 
Ajabu jengine pia muungano wake aina yake haiko dunia nzima na wapiga kura kuhadaiwa kwa matenge na wali
 
Nimelipenda na kulifurahia ajabu NAMBA 7,,,,,INGAWA NA MENGINE YANA MANTIKI,,,jaman njia tatu enzi ya TIBAIGANA IMEUA WATU HIII,,,,,,,,
 
Kweli hapa kazi ipo

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Ajabu, makamu wa rais kutembea na mkasi mfukoni.
_bunge lenye wasomi darasa la saba eg lakairo,lusinde
 
Nchi ina madini, hifadhi, na bandari lakini ni maskini. Hili nalo ajabu wadau!
 
Nchi ina madini, hifadhi, na bandari lakini ni maskini. Hili nalo ajabu wadau!

nchi ya wakazi million 40 kupimiwa viwanja vya makazi nchi nzima viwanja laki moja toka uhuru miaka 50 .na kuwacha watu wakichakura paku jenga kama kuku wa kienyeji ,hili pia ajabu lipo tanzania
 
Duh! kwa hiyo tunastahili kuja kutazamwa na watalii toka dunia yote na kulipwa kwa hilo?!
 
Watu wawili wamelazwa hospital kubwa nchini.Mmoja anaumwa mguu mwingine anauvimbe kichwani.Operation inafanyika.Mwenye uvimbe kichwani anafanyiwa operation ya mguu na wa mguu afanyiwa operation ya kichwa.HII NI KALI KULIKO ZOTE DUNIANI NA imefanyika ndani ya bongo pekee
 
Back
Top Bottom